Mkenya aliyetekwa na watu wasiojulikana Tanzania ni nani?

comrade_kipepe

JF-Expert Member
Jun 25, 2019
2,732
2,477
Wiki moja imetimu toka mfanyabiashara raia wa Kenya na mshirika wa Zitto Kabwe kutekwa Tanzania.

Leo Jumatatu Julai 1, 2019 inatimia wiki moja toka wanaoitwa watu wasiojulikana kumteka na kutokomea kusipojulikana mfanya biashara raia wa Kenya ambaye amelowea jijini Dar es Salaam.
Raphael Ongangi alitekwa Jumatatu usiku katika viunga vya mitaa ya Oysterbay jijini Dar es Salaam na watu wenye silaha akiwa na mke wake Veronica Kundya.

Kwa mujibu, wa taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari nchini Kenya na Tanzania, watu wasiojulikana waliwafuatilia wanadoa hao na kisha kulizuia gari yao na kumchukua bwana huyo na kuondoka naye, awali bi Veronica anasema alimriwa na watu hao ambao anadai walijatambulisha kama maafisa usalama kuwa asiseme chochote mpaka atakapotaarifiwa nao, na baada ya takribani saa moja akapokea simu kutoka kwa mumewe iliyomtaka kurejea nyumbani na wala asiripoti tukio hilo mahali popote.

Hata hivyo, ameripoti tukio hilo katika kituo cha polisi Oysterbay na ubalozi wa Kenya nchini Tanzania.

Mpaka sasa, si familia yake wala mamlaka za Kenya na Tanzania ambao wameripoti juu ya chanzo cha utekaji huo na endapo watekaji wanataka kikombolea ama laa.

*Ongangi ni nani?.

Taarifa zilichapishwa kwenye mitandao ya kijamii zinaripoti kuwa Ongangi aliingia Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 2000 kwa masomo ya elimu ya juu katika moja ya vyuo vikuu nchini humo.

Baada ya masomo alibaki nchini humo na kuanza biashara na inaripotiwa kuwa ana miliki na kuendesha biashara ya kusafirisha mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam kwenda Rwanda, Zambia na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Tukio la Ongangi kutekwa lilichukua sura mpya baada ya Kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe kuhusianisha kushikiliwa kwake mateka na kudukuliwa kwa mitandao yake ya kijamii.

Taarifa zinaonesha kuwa Ongangi na Zitto wana usumwahiba na mfanyabiashara huyo ameshawahi kuwa msaidizi wa Kabwe.

Zitto aliwaambia waandishi jijini Dodoma wiki iliyopita kuwa waliomteka Ongangi wamedukua mitandao yake ya kijamii.

Uongozi wa ACT-Wazalendo baada ya hapo ukatoa taarifa kuwa mfanyabiashara huyo alihusika kwa kiasi kikubwa katika kufunguliwa kwa mitandao hiyo, na ndiye mtu pekee ambaye alikuwa na nywila (pasword) ukiacha Zitto mwenyewe.

Baada ya kutekwa Ongangi na kabla ya Zitto kutoa taarifa hiyo, mitandao hiyo ya kijamii ya Zitto ilichapisha maudhui ambayo yalistaajabisha wengi.

Zitto anafahamika kwa kuwa na msimamo mkali wa kuikosoa serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais John Magufuli, lakini maudhui yanayotiliwa shaka yalionesha kulegeza kamba kwa mwanasiasa huyo.

"ni kweli tumekuwa tukiikosoa Serikali kwa muda mrefu lakini lazima nikiri kuwa kuna mabadiliko makubwa yamefanywa na serikali hii ya JPM, Japokuwa ninajua kuna baadhi ya viongozi aliowateua wanamuangusha kiuhalisia MAGUFULI amefanya mengi," ndivyo ujumbe wa kwanza kupitia akaunti ya Zitto ya Twitter uliandika Alhamisi ya wiki iliyopita.

Kisha ukafuata huu: "Nilisema tangu mwanzo sitashiriki siasa za kupinga maendeleo yanayofanywa na serikali hii ya @MagufuliJP na sasa nimeamua kwa moyo wa dhati kabisa ninaamua kuunga mkono kwani ni kwa maendeleo ya wote, kiongozi mbinafsi kwa vyovyote hawezi kuona haya yanayofanyika kwa sasa."

Ujumbe wa mwisho uliotumwa saa 7.26 mchana wa siku hiyo uliwalenga wabunge wa chama tawala CCM ambao wanaonekana kuwa ni wakosoaji wa ndani wa serikali yao: "Nawakaribisha pia @HusseinBashe na @Nnauye_Nape ambao wameshachukua kadi za uanachama ACT Wazalendo na wanaosubiri ni kuvunjwa tu kwa #Bunge na bila kumsahau mdogo wangu @JMakamba.

Hakika ACT Wazalendo itaitikisa Chadema ambayo inatamba kuwa Chama Kikuu cha Upinzani."

Mwanasiasa huyo amesema mara ya mwisho kutumia akaunti zake ilikuwa Juni 11, 2019 baada ya kukamatwa na kuwekwa kizuizini na Idara la Uhamiaji Zanzibar ambao walimzuia kusafiri kwenda Kenya.

Mara baada ya kumwachia, Zitto hakupewa simu yake ya mkononi na kompyuta mpakato 'laptop.'

Mtandao huo wa Twitter wa Zitto tayari umeshafungwa baada ya kutokea tukio hilo.

Hat hivyo ujumbe huo uliwaibua Bashe na Nape ambao walionekana kuwarushia lawama wahusika ambao hawakuwataja majina,
wanaharakati wa mitandao wapaza sauti
Taarifa rasmi juu ya tukio hilo ni haba.

Gazeti la Mwananchi limemnukuu Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Musa Taibu akisema askari polisi wamesambazwa mtaani ili kufuatilia mtu aliyemteka Ongangi.

Taibu amesema walipokea taarifa kutoka kwa mke wake Veronika Kundya akidai mumewe Rafael wakiwa kwenye gari lao walikingwa na gari mbele yao na kumchukua mume wake huku wakimueleza ana mazungumzo naye.

Wakati watu hao wakizungumza na Rafael hakuweza kusikia maneno yaliyokuwa yakizungumzwa kwa kuwa walimuingiza kwenye gari jingine.

"Bahati mbaya hakujua namba ya gari na aina ya gari kwa bahati mbaya jeshi la polisi hatuna vithibitisho hivyo, tunaendelea na uchunguzi kama ni kweli ametekwa na tuna imani tutafanikiwa kwa kuwa tumewasambaza askari polisi mtaani ili kufuatilia," Taibu amenukuliwa akisema na Mwananchi.

Balozi wa Kenya nchini Tanzania Dan Kazungu amenukuliwa na Gazeti la The Standard wiki iliyopita akikiri kupokea taarifa hizo na kusema wanashirikiana na mamlaka za Tanzania.

Lakini katika mitandao ya kijamii, wanaharakati na watumiaji wa kawaida kote Kenya na Tanzania wamekuwa wakipaza sauti zao kupitia anuani mtandao (hashtag) #FreeRaphaelOngangi na #BringBackRaphaelOngangi.

Na leo hii wengi wameonesha kusikitishwa kwa kesi hiyo kufikia siku ya saba bado ikiwa ni kitendawili kisicho na jibu.

Baadhi ya Watanzania wametaka serikali yao ilishughulikie suala hilo kama serikali ya Kenya ilivyoshughulikia kwa haraka suala la kutishiwa wafanyabiashara wa Tanzania nchini humo.

Matukio ya utekaji, hasa unaofanywa na watu wanaoitwa wasiojulikana nchini Tanzania umeendelea kuzua hofu kwa miaka ya hivi karibuni.

Hivi karibuni, mwanaharakati wa upinzani na mkosoaji wa rais Magufuli mitandaoni Bwana Mdude Nyangali maarufu kama Mdude Chadema, alitekwa na wasiojulikana na kisha kutelekezwa siku chache baadae akiwa amepigwa na kuonesha dalili za kuteswa.
 
Tuombee apatikane akiwa hai tu uhai wa MTU ni kitu cha thamani sana kuliko Mali na dhahabu

Tupige kelele kama tulivyopiga wakati amepotea Mo
 
Hivi huyo mkenya na ACT wanamahusiano gani? Ninaona kama tunachanganya mambo. Ninadhani ingebakia tu kuwa ni mshirika wa kibiashara na bwana Zitto.
 
Mtu anayetamani malaika washuke chini na kufunga mitandao ya kijamii anatekeleza matamanio yake, mtu muovu hawezi kujificha
 
Wakenya wanapenda na wanamudu sana revange, sijui kitakachofuata ikiwa raia wao hatapatikana kwa mfano wa kina Ben saanane na Aziron!!
 
Watu wasiojulikana katika ubora wao! Wengine utakuta wapo tu humu wanatusanifu na kuwavutia kasi wale watu wao wanao wahitaji.
 
Back
Top Bottom