Sitaki kuamini kwamba Genge la Wasiojulikana lipo ndani ya TISS. Ila ni kwanini TISS imenyamaza na inaendelea Kuyanyamazia haya Matukio?

Mzukulu

JF-Expert Member
Feb 14, 2020
1,403
2,000
Kama nitakuwa nakosea Wabobezi na Wajuvi zaidi mtanirejebisha na nitawashukuruni sana tu. Nijuavyo Mzukulu ni kwamba kama kuna Idara au Taasisi ambayo ipo nchini Tanzania na ina uwezo mkubwa mno wa Kunusa kila baya, kuliwahi na hata ikiwezekana kulikabili Kimedani kwa ama kushirikiana na Jeshi la Polisi au hata Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa Ustawi wa Amani na Usalama

Kuna Matukio kadhaa ya Kusikitisha yanayojumuisha Utekaji, Kujeruhi na hata Kuuliwa kwa Watu, Wanasiasa ( hasa wa Upinzani ) na Wanaharakati kwa Kipindi hiki cha Miaka hii Minne Mitano ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Kuna minong'ono ya kila aina ama hapa Mtandaoni ( Mitandaoni ) na Mitaani inayoihusisha moja kwa moja Idara ya Usalama wa Taifa nchini ( TISS)

Mzukulu bado sijaiamini hiyo minong'ono kwakuwa bado sijathibitisha lakini kinachonipa Mashaka na taratibu nami kuanza Kushawishika kuwa huenda yasemwayo yana ukweli ndani yake ni Kitendo cha Wahusika Wakuu wa Usalama nchini Tanzania ( TISS ) kukaa kimya wakati wanajua kuwa Wanachafuliwa kutwa lakini pia Wao kama Idara Nyeti wana Dhamana ya Kuyadhibiti haraka.

Nadhani kama kuna Jukumu Kubwa alilonalo Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa ( TISS ) nchini Bwana Diwani Athuman Msuya ni Kuwaaminisha na Kuwathibitishia Watanzania tena kwa Hoja thabiti na ikiwezekana hata Ushahidi wa Kitaaluma na Kimedani kuwa Idara yake haihusiki na hili Genge la Wahuni lililobatizwa Jina la Wasiojulikana.

Kuendelea kukaa Kwake kimya kama ambavyo Mtangulizi wake Bwana Modestus Kipilimba alikuwa ni kuendelea kuifanya Idara ya Usalama wa Taifa nchini siyo tu ichukiwe bali sasa izidi Kudharaulika na baadhi ya Wananchi ( japo siyo wote ) kitu ambacho Kiuweledi kina Athari kubwa ya Kiutendaji Kwao kwakuwa 100% ya Ufanisi wako Kijasusi unategea Wananchi Kiushirikiano wao

Sasa ni wakati muafaka kabisa wa ama TISS kujitokeza na Kukemea hadi Kuwataja hao Wahuni Wapumbavu au inyamaze iendelee Kuhusishwa.

Akhsanteni.

Wenu Mtanzania Mwaminifu, Mzalendo na Mtiifu

Mzukulu a.k.a Brainy Chap.
 
Ramea

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
2,041
2,000
Uzi kama huu wasiojulikana wanacheck tu comments. Muda wote utakuta wapo online. Alafu wanakufata PM kukutishia. Kuna wasengerema kama wawili humu wana kawaida ya kufatana Pm na kutishiana. Hi nchi siyo ya kwenu peke enu umbwa nyie.
 
shamajengo

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
1,216
2,000
Endelea kutokumini hivyo hivyo maana. CHADEMA inonekana wametengeneza movie tu hawa wanawake.
Unawachukuliaje wanawake mpuuzi mkubwa,, mwanamke ndo amekuzaa wewe leo unakuja kuleta kejeli zako hapa juu ya wanawake..unaangalia tumbo lako mpaka unasahau hata usataarabu juu ya wanawake amabao ndiyo chanzo Cha vizazi vyote...mama yako angebana mapaja wakati unazaliwa si ungekufa wewe ebu kuwa mstaarabu bwana siasa zisikufanye usahau utu....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
RAYAN THE DON

JF-Expert Member
Aug 21, 2019
666
1,000

Just relax, calm down dada yangu. I take full responsibility for what happened since sikuwa na maana hiyo but nimechanganya post. Please accept my apology sister.
 
Ndama dume

JF-Expert Member
Nov 1, 2019
860
1,000
Hivi Tiss ni hawa hawa ambao siku hizi hata akiwa anatongoza lazima ajitambulishe ndio wawe na medan duuuh
 
albab

JF-Expert Member
Jul 6, 2018
571
1,000
umeshawahi kusikia TISS inamsemaji Kama ilivyo kwa majeshi mengine?? Umeshawahi kujiuliza kwanini??
Ulishawahi kusikia mkurugenzi wa TISS kaitisha vyombo vya habari??
Unalolitamani HALIWEZEKANI.
 
Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
52,695
2,000
Uvccm akiwepo kwenye ajira yoyote anatanguliza maslahi ya chama kwanza,

sasa kama ajira yake ina connection na
kifaa chochote cha moto atahakikisha anatumia kifaa hicho kumfitini mpinzani wa ccm
 
konyola

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
2,162
2,000
Kuna kipndi flani ilikuwa 2017 kuna mrembo mmoja matata alinifuata inbox na kuniomba tuwe frienda kama pen pals baadae akanambia amenikubali kutokana koment flani kwamba imemkuna.

Hakuishia hapo aliendelea kuni inbox kila wakati akinijulia hali. nikampiga vocal akakataa nami nikapotezea baada ya muda flani kupita alinisalimu na kunambia mbona nimekata tamaa mapema akaomba na mba ya simu au emal nikamgomea.

Siku moja nikamwomba tuonane mimi nilikuwa SUA Campus ya mazimbu. Akasema yeye anasoma IFM na kwamba atakuja wikiendi iliyokuwa inafuata.
Nikampotezea kwa upeo wangu nilidhani ni WANAOJULIKANA
 
Proved

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
11,160
2,000
umeshawahi kusikia TISS inamsemaji Kama ilivyo kwa majeshi mengine?? Umeshawahi kujiuliza kwanini??
Ulishawahi kusikia mkurugenzi wa TISS kaitisha vyombo vya habari??
Unalolitamani HALIWEZEKANI.
Mbona mwaka 2010 waliitisha mkutano kukanusha madai ya Slaa kwamba ''walichakachua kura" ?
 
Makande 26

Senior Member
Jul 23, 2019
128
250
Uzi kama huu wasiojulikana wanacheck tu comments. Muda wote utakuta wapo online. Alafu wanakufata PM kukutishia. Kuna wasengerema kama wawili humu wana kawaida ya kufatana Pm na kutishiana. Hi nchi siyo ya kwenu peke enu umbwa nyie.
 
C.T.U

JF-Expert Member
Jun 1, 2011
5,022
2,000
Tukio la Mbowe kitaalamu ni Felony ... sasa nikusaidia chukua simu yako ingia Google then angalia kuna Felony ngapi Marekani ambako kuna CIA, FBI, NSA, Homeland Security etc
Kama nitakuwa nakosea Wabobezi na Wajuvi zaidi mtanirejebisha na nitawashukuruni sana tu. Nijuavyo Mzukulu ni kwamba kama kuna Idara au Taasisi ambayo ipo nchini Tanzania na ina uwezo mkubwa mno wa Kunusa kila baya, kuliwahi na hata ikiwezekana kulikabili Kimedani kwa ama kushirikiana na Jeshi la Polisi au hata Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa Ustawi wa Amani na Usalama.

Kuna Matukio kadhaa ya Kusikitisha yanayojumuisha Utekaji, Kujeruhi na hata Kuuliwa kwa Watu, Wanasiasa ( hasa wa Upinzani ) na Wanaharakati kwa Kipindi hiki cha Miaka hii Minne Mitano ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Kuna minong'ono ya kila aina ama hapa Mtandaoni ( Mitandaoni ) na Mitaani inayoihusisha moja kwa moja Idara ya Usalama wa Taifa nchini ( TISS )

Mzukulu bado sijaiamini hiyo minong'ono kwakuwa bado sijathibitisha lakini kinachonipa Mashaka na taratibu nami kuanza Kushawishika kuwa huenda yasemwayo yana ukweli ndani yake ni Kitendo cha Wahusika Wakuu wa Usalama nchini Tanzania ( TISS ) kukaa kimya wakati wanajua kuwa Wanachafuliwa kutwa lakini pia Wao kama Idara Nyeti wana Dhamana ya Kuyadhibiti haraka.

Nadhani kama kuna Jukumu Kubwa alilonalo Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa ( TISS ) nchini Bwana Diwani Athuman Msuya ni Kuwaaminisha na Kuwathibitishia Watanzania tena kwa Hoja thabiti na ikiwezekana hata Ushahidi wa Kitaaluma na Kimedani kuwa Idara yake haihusiki na hili Genge la Wahuni lililobatizwa Jina la Wasiojulikana.

Kuendelea kukaa Kwake kimya kama ambavyo Mtangulizi wake Bwana Modestus Kipilimba alikuwa ni kuendelea kuifanya Idara ya Usalama wa Taifa nchini siyo tu ichukiwe bali sasa izidi Kudharaulika na baadhi ya Wananchi ( japo siyo wote ) kitu ambacho Kiuweledi kina Athari kubwa ya Kiutendaji Kwao kwakuwa 100% ya Ufanisi wako Kijasusi unategea Wananchi Kiushirikiano wao.

Sasa ni wakati muafaka kabisa wa ama TISS kujitokeza na Kukemea hadi Kuwataja hao Wahuni Wapumbavu au inyamaze iendelee Kuhusishwa.

Akhsanteni.

Wenu Mtanzania Mwaminifu, Mzalendo na Mtiifu

Mzukulu a.k.a Brainy Chap.
 
joseph1989

JF-Expert Member
May 4, 2014
7,277

Huyu nae anaingia ktk group la WASIO JULIKANA.
images (13).jpeg
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom