Kama kweli Mungu hayupo, who organized haya mambo duniani?

Hili swali ndilo nililouliza mwanzo kabisa mwa machango wangu katika mada hii.

Kusema kweli swali hili nimeshalijibu katika michango mingi kwenye mada hii.
Michango mingi haina namba?

Kila post ina namba, weka link hapa au toa namba ya post.

Umesema Mungu ni nguvu, hii complex order iliyopo haiwezi kujitokeza yenyewe tu.

Nikakuambia hii hoja yako itataka hiyo nguvu nayo iwe na muumbaji wake/ chanzo chake, isiweze kutokea tu, na kwa hivyo, katika ulimwengu huo ambao kila kitu kitahitaji kuwa na muumbajinwake, hapo hakuna Mungu muumba vyote.

Sijui kama hata ulielewa hii hoja yangu, na sioni ulipoijibu.
 
Uko sahihi...Kila kitu ni Mungu, just different manifestations of the same phenomenon.
Kama maji,barafu na mvuke vyote kuwa ni kitu kimoja ila katika manifestations tofauti.

Mipangilio yote imewekwa na Mungu kwa ajili ya Mungu na ni Mungu pia.

Lakini kama ambavyo bila Giza huwezi kuwa na Mwanga, na kama ambavyo bila empty space huwezi kuwa na solid yoyote, ndivyo Hivyo Mungu alihitaji kuwa na ubaya (shetani) ili aweze kuwa na uzuri
Ubaya ulikuja baada ya binadamu kuletwa duniani kuishi karibu na shetani, ndo inabidi tupambane tukifa tukaishi edeni.
 
Kwa sababu ni contradictions, hazina logical consistency. Inaonekana ni hadithi za kuungwa ungwa tu, hapa unaambiwa kitu kimoja, pale unaambiwa kitu kingine kinachopingana na kile cha awali kabisa.

Ukiuliza kwa nini hapa kuna contradiction, unapewa maelezo ambayo yanakuja kuharibu kabisa badala ya kusawazisha.
Kwenye mchango wangu nimesema kwamba biblia yote ni teolojia. Watu lazima wajue hilo kwamba biblia ni teolojia.

Kama tutaiangalia biblia nje ya teolojia, hiyo sio biblia ni kitabu tu cha kawaida.

Sasa katika misingi ya teolojia, biblia ina hicho unachoita logical inconsistency?
 
Teolojia ni nini na kwa nini ni muhimu kuliko physics na mathematics katika kuuelewa ulimwengu halisi ulivyo?

Teolojia ina maana gani kama Mungu hayupo?

Ikiwa Biblia inatuambia Mungu alimuumba Adamu na Hawa, wakati Mungu hayupo na wala hakumuumba Adamu wala Hawa, hii ni hadithi ya kale sana ya Wayahudi tu ya kujimwambafy na kujaribu kuelezea ngano za utamaduni wao na safari yao kama taifa duniani (ambazo zipo katika kila utamaduni), halafu wewe ukaja ukasoma hizo ngano za Wayahudi na kuzifanya kuwa ndiyo ukweli wa Mungu (wakati hata kabila lako lina ngano hizo, labda wewe huzijui tu) huoni kwamba kuamini kuwa Biblia ni neno la Mungu ni tatizo hapo?
 
Hebu nijaribu kukueleza tena.

Ukiwa na mchele wenye mchanga, halafu unataka kuchuja uondoe mchanga ubaki na mchele, kwa chujio, lakini chujio ulilochagua lina matobo madogo kuliko mchanga, hutaweza kuuchuja huo mchanga, hivyo, uchaguzi wako wa chujio unaweza kukupa matokeo tofauti na ukweli halisi. Unaweza kusema huu mchele safi hauna mchanga kwa sababu nimeuchuja, kumbe bado una mchanga kwa sababu umetumia chujio lisilo na ufanisi katika kuchuja.

Watu waliofanya research za kisayansi wanajua kuhusu "selection bias". Labda weee hujasima. Ndiyo maana watu wa computer science na IT leo wanasisitiza models za Artificial Intelligence ziwe na diversity zisije kuwapa matokeo yenye bias za mifumo ya wazungu tu.

Nakwambia hivi, ukitaka kumuangalia mtu kwa macho matupu uone mifupa ya ndani ya mwili wake, utashindwa.

Ukitaka kumuangalia mtu uone mifupa ya ndani ya mwili wake utahitaji kutumia x-ray machine.

Njia unayotumia kupimia mambo inaweza kukupa matokeo tofauti na ukweli wa mambo.

Unaweza kusema mtu hana mifupa, mbona nimemuangalia sijaiona hiyo mifupa? Kumbe umemuangalia kwa macho matupu, hujatumia x-rays, ungetumia x-rays, ungeona mifupa ilivyokaa.

Ukitaka kuujua ulimwengu kiundani kabisa kwa kuuangalia kwa macho tu kijuu juu simply, utaishia kusema dunia ni flat na jua linaizunguka dunia. Hitimisho ambalo si sahihi.

Ukitaka kuujua ulimwengu kwa ndani inabidi ujifunze hesabu na physics. Na hapa ndipo kuna tatizo kwetu. Watu wanataka kuujua ulimwengu kwa kusoma Quran na Biblia, bika kuangakia hesabu na Physics.

Yani, lile chujio wanalotumia lina matatizo tayari, hivyo hawawezi kuupata ukweli.

Hapa tumeanza kwa kumuongelea Mungu specific, mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.

Tunaweza kukubaliana nguvu haiwezi kuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote?

Nguvu ya asiki haina uwezo wa kupandisha maji kutoka baharini, kufuata mto, kupanda juu mpaka juu ya mlima Kilimanjaro.

Nguvu ya asili haina ufahamu wa kukujua wewe.

Nguvu ya asili haina upendo, ndiyo maana majanga ya asiki yanaua watu.

Tunaweza kukubaliana kwamba, kwa kuanzia, nguvu hii haiwezi kuwa Mungu mjuzi wa yote, muweza yote na mwenye upendo wote?
Sasa nguvu ya asili hiyo imeumbwa na Muumbaji, na hata ukitumia vitabu vya dini bila sayansi Bado Mungu ataoneka, Sasa tutumie logic ya dini, Mungu aliumba mwanadamu akamweka sehemu isiyo na ubaya wowote iliitwa edeni baada ya uasi akatolewa edeni na Sasa yupo sehemu yenye shida anahitaji kupambana kutenda wema ili aushinde uovu arudi edeni, hivyo universe inabaki kuwa chini ya Mungu, kuhusu dini Mungu dini yake ni wema, ndo maana kila mtu anayetenda wema wa dini yoyote hata kama ameamua kuabudu chochote atahesabiwa kwa wema wake, kuhusu dini kuandikwa na watu ndiyo zimetengenezwa na watu zikiwa zimekopi Sheria za Mungu na kuongezea maisha ya zamani yajinsi vizazi vya zamani vilivyoishi chini ya Mungu au shetani, na hapo kumbuka Kuna vitabu vya walimu ndo hivyo vinafomula zote za hivyo vitabu vya dini vinavyotumika na wanafunzi wa hizo dini, hivyo vitabu vya walimu ndo vimetengeza hizi formula za sayansi na hesabu na maarifa yote yanatoka humo, Sasa wewe umejifungia kwenye vitabu vya wanafunzi vya dini ndo maana huoni huyo Mungu na wakati hao wanayansi wao wanakwambia Mungu yupo maana maarifa wanakopy kwake.
 
Uko sahihi...Kila kitu ni Mungu, just different manifestations of the same phenomenon.
Kama maji,barafu na mvuke vyote kuwa ni kitu kimoja ila katika manifestations tofauti.

Mipangilio yote imewekwa na Mungu kwa ajili ya Mungu na ni Mungu pia.

Lakini kama ambavyo bila Giza huwezi kuwa na Mwanga, na kama ambavyo bila empty space huwezi kuwa na solid yoyote, ndivyo Hivyo Mungu alihitaji kuwa na ubaya (shetani) ili aweze kuwa na uzuri
Mungu muweza wa yote, Kwa nini ahitaji ubaya kudhihirisha uzuri wake?

Alishindwaje kujidhihirisha uzuri wake, Pasipo ubaya?

Mungu huyo anaweza yote kweli?

Kama mpaka atumie ubaya kudhihirisha uzuri wake anaweza yote kweli?
 
Umeandika "Jinsi ulimwengu ulivyo na unavyofanya kazi haiwezekani kwamba sio tokeo la Uwepo wa Hali ya Juu Wenye Akili."

Unajuaje hili? Unalithibitishaje? Umetumia njia gani kujua hili? Unajuaje njia uliyotumia ni sahihi?

Kama kila kilicho na complex order ni lazima kiwe kimeumbwa na kingine chenye complex order na akili kubwa zaidi, huo uwepo wa hali ya juu wenye akili nao umetoka wapi? Umekuwapo vipi? Umeanzaje?

Huoni kwamba hii kanuni yako itatukataza kuwa na chanzo cha kwanza kilichoanzisha yote, kwa sababu kila kilicho complex order kitahitaji muumbaji wake, na hivyo, katika ulimwengu huo, Mungu hawezi kuwepo?

Kuhusu Biblia, kama kweli Biblia ni kitabu cha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kwa nini kiwe kitabu kigumu hivyo kukielewa kinachohitaji elimu maalum?

Kwa nini huyo Mungu hakukifanya kiwe kitabu rahisi kinachoeleweka na kila mtu?

in fact, kwa nini huyo Mungu aweke habari zake kwenye kitabu, teknolojia hafifu, yenye matatizo mengi ya tafsiri za lugha na tamaduni? Kwa nini huyo Mungu asiweke habari zake zote kwenye DNA ili kika mtu akizaliwa tu awe anamjua vizuri kabisa, bila utata, katika namna ambayo hata Biblia haihitajiki?

Biblia ina contradictions nyingi sana zinazoonesha ni kitabu kilichoandikwa na watu tu, chenye makosa mengi tu, nikikuwekea hapa hizo cintradictiins huwezi kumaliza kuzitatua.

Kama unabisha, nibishie nikuwekee hapa nikuoneshe contradictions lukuki zilizopo kwenye Biblia.
Wewe hujui kizazi kilichopo Sasa kinaanzia kwa nuhu? Na ndo maana ujenzi wa dunia ulianza upya? Na kadri muda unavyokwenda habari nyingine zinabaki kuwa historia na maandiko yanabaki kuwa msaada wa kujua wema na ubaya ni njia inayoelekea wapi na siyo mashindano ya kukalili hiyo biblia na kushindania kukalili vitabu, hao walioandika hivyo vitabu huoni wamebaki na msimamo wa kutenda haki na kutenda wema na ubaya wanakwambia tenda ubaya ukiwa unajua mwisho wako ni wapi.
 
Sasa nguvu ya asili hiyo imeumbwa na Muumbaji, na hata ukitumia vitabu vya dini bila sayansi Bado Mungu ataoneka, Sasa tutumie logic ya dini, Mungu aliumba mwanadamu akamweka sehemu isiyo na ubaya wowote iliitwa edeni baada ya uasi akatolewa edeni na Sasa yupo sehemu yenye shida anahitaji kupambana kutenda wema ili aushinde uovu arudi edeni, hivyo universe inabaki kuwa chini ya Mungu, kuhusu dini Mungu dini yake ni wema, ndo maana kila mtu anayetenda wema wa dini yoyote hata kama ameamua kuabudu chochote atahesabiwa kwa wema wake, kuhusu dini kuandikwa na watu ndiyo zimetengenezwa na watu zikiwa zimekopi Sheria za Mungu na kuongezea maisha ya zamani yajinsi vizazi vya zamani vilivyoishi chini ya Mungu au shetani, na hapo kumbuka Kuna vitabu vya walimu ndo hivyo vinafomula zote za hivyo vitabu vya dini vinavyotumika na wanafunzi wa hizo dini, hivyo vitabu vya walimu ndo vimetengeza hizi formula za sayansi na hesabu na maarifa yote yanatoka humo, Sasa wewe umejifungia kwenye vitabu vya wanafunzi vya dini ndo maana huoni huyo Mungu na wakati hao wanayansi wao wanakwambia Mungu yupo maana maarifa wanakopy kwake.
Unajuaje kuwa nguvu ya asili imeumbwa na muumbaji na kwamba hiyo si hadithi tu unayoiamini?

Na huyo muumbaji chanzo chake nini?
 
Wewe hujui kizazi kilichopo Sasa kinaanzia kwa nuhu? Na ndo maana ujenzi wa dunia ulianza upya? Na kadri muda unavyokwenda habari nyingine zinabaki kuwa historia na maandiko yanabaki kuwa msaada wa kujua wema na ubaya ni njia inayoelekea wapi na siyo mashindano ya kukalili hiyo biblia na kushindania kukalili vitabu, hao walioandika hivyo vitabu huoni wamebaki na msimamo wa kutenda haki na kutenda wema na ubaya wanakwambia tenda ubaya ukiwa unajua mwisho wako ni wapi.
Kizazi cha sasa hakianzii na Nuhu.

Kizazi cha sasa kimeanzia kwa Waafrika, si kwa Wayahudi. Waafr8ka walikuwapo kabla ya Wayahudi, kwa maelfu na maelfu ya miaka.

Kuna ushahidi wa kibaiolojia wa DNA kuonesha hilo.

Mpaka hapo ushakosea.

Unatumia Biblia kuhitimisha mambo, wakati Biblia ni kitabu cha hadithi za Wayahudi, si kitabu cha scientific facts.
 
Unajuaje kuwa nguvu ya asili imeumbwa na muumbaji na kwamba hiyo si hadithi tu unayoiamini?

Na huyo muumbaji chanzo chake nini?
Chanzo chake anakijua yeye ila kipo katika mfumo wa upepo, moto, udongo na maji, anajifunua tu kwa mtu anayekubali kuwa yeye ndo chanzo chake.
 
Chanzo chake anakijua yeye ila kipo katika mfumo wa upepo, moto, udongo na maji, anajifunua tu kwa mtu anayekubali kuwa yeye ndo chanzo chake.
Ukisema chanzo chake kipo ila anakijua yeye umekubali hata wewe humjui. Unabumbabumba tu.

Ukiongelea mambo ya upepo, moto, udongo na maji unajionesha kuwa hujui physics.

Ulimwengu ulikuwepo kabla ya upepo, moto, udongo na maji kuwepo.

Na kqma Mungu wako kaanzishwa na hivyo vitu, hiyo si Mungu.

Kwa sababu kaanzishwa na hivyo.
 
Kizazi cha sasa hakianzii na Nuhu.

Kizazi cha sasa kimeanzia kwa Waafrika, si kwa Wayahudi. Waafr8ka walikuwapo kabla ya Wayahudi, kwa maelfu na maelfu ya miaka.

Kuna ushahidi wa kibaiolojia wa DNA kuonesha hilo.

Mpaka hapo ushakosea.

Unatumia Biblia kuhitimisha mambo, wakati Biblia ni kitabu cha hadithi za Wayahudi, si kitabu cha scientific facts.
Hiyo sayansi inatumia mifumo ya Mungu yote nakuhakikishia hakuna sayansi iliyo nje ya mfumo wa Mungu, Tena ukomo wake unamipaka unabaki kuzunguka mulemule kwa kuboresha tu, mfano udongo aliotumia Mungu kuumba mwanadamu ni wa kipekee hakuna sayansi imeupata, maji nje ya mfumo wa Mungu huwezi kutengeneza, kufikia vitufe vya mbinguni sayansi haiwezi, mfano kitufe Cha kuwasha jua Kuna mwanasayansi anacho? Uniletee? Sayansi wamekopi kwa kutengeneza umeme na kitufe Cha kuwasha umeme lakini mifumo ya Mungu asipotaka mwanadamu aiguse basi huwezi kugusa.
 
Basi hao waafrika waumbe mtu mpya maana kizazi kimetoka kwao, Mtu ameubwa na Mungu na mwanadamu hawezi kufikia huo uumbaji, zaidi wewe unaangalia mwili wa nyama na damu, lakini huo unatoka kwa viuno vya wazazi wako, ila pumzi yako inatoka kwa Mungu.
 
Teolojia ni nini na kwa nini ni muhimu kuliko physics na mathematics katika kuuelewa ulimwengu halisi ulivyo?
Physics na Mathematics ni lazima katika kuelewa Teolojia. Kwa kweli mtu ambaye hajui sio tu Physics na Mathematics bali pia Biology, Chemistry, Georgraphy na au History, hawezi kujua au kuelewa Teolojia.

Teolojia ndio elimu ya juu kabisa sio tu kuhusu kuuelewa ulimwengu halisi ulivyo lakini pia kuelewa maisha baada ya kifo na au lengo la maisha.

Kama wewe unaelewa vizuri Physics, Mathematics, Biology, Chemistry na Geography utaelewa kwamba elimu hizi zinafafanua vizuri Teolojia (Biblia) kwa lugha au kwa namna inayoweza kueeleweka na kila mtu
 
Ukisema chanzo chake kipo ila anakijua yeye umekubali hata wewe humjui. Unabumbabumba tu.

Ukiongelea mambo ya upepo, moto, udongo na maji unajionesha kuwa hujui physics.

Ulimwengu ulikuwepo kabla ya upepo, moto, udongo na maji kuwepo.

Na kqma Mungu wako kaanzishwa na hivyo vitu, hiyo si Mungu.

Kwa sababu kaanzishwa na hivyo.
Hebu niumbie mtu kama wewe anayekula na kwenda choo, na ukimaliza uniumbie Galaxy Moja tu kwa njia ya sayansi uniwekee maji, jua, mwezi na asili zote uje unikabithi, hivi hujiulizi hao wanasayansi kama wanauwezo wa kuumba galaxy Sasa kwanini waishi katika huu mfumo wa shidashida? Si wangetengeneza edeni Yao nje ya huu mfumo unaojiendea wenyewe tu bila kusema Kuna future kulingana na matendo ya mtu? Tena wamekaa tu eti wanasubiri hiyo nature iwaletee majanga, jamani hii zawadi tuliyopewa tujifunze jinsi ya kuitumia tupate Neema.
 
Hiyo sayansi inatumia mifumo ya Mungu yote nakuhakikishia hakuna sayansi iliyo nje ya mfumo wa Mungu, Tena ukomo wake unamipaka unabaki kuzunguka mulemule kwa kuboresha tu, mfano udongo aliotumia Mungu kuumba mwanadamu ni wa kipekee hakuna sayansi imeupata, maji nje ya mfumo wa Mungu huwezi kutengeneza, kufikia vitufe vya mbinguni sayansi haiwezi, mfano kitufe Cha kuwasha jua Kuna mwanasayansi anacho? Uniletee? Sayansi wamekopi kwa kutengeneza umeme na kitufe Cha kuwasha umeme lakini mifumo ya Mungu asipotaka mwanadamu aiguse basi huwezi kugusa.
Hujathibitisha kwamba Mungu yupo.

Thibitisha kwamba Mungu yupo kwanza.
 
Basi hao waafrika waumbe mtu mpya maana kizazi kimetoka kwao, Mtu ameubwa na Mungu na mwanadamu hawezi kufikia huo uumbaji, zaidi wewe unaangalia mwili wa nyama na damu, lakini huo unatoka kwa viuno vya wazazi wako, ila pumzi yako inatoka kwa Mungu.
Hujathibitisha Mungu yupo, usharukia kusema mtu kaumbwa na Mungu?

Thibitisha Mungu yupo kwanza.
 
Physics na Mathematics ni lazima katika kuelewa Teolojia. Kwa kweli mtu ambaye hajui sio tu Physics na Mathematics bali pia Biology, Chemistry, Georgraphy na au History, hawezi kujua au kuelewa Teolojia.

Teolojia ndio elimu ya juu kabisa sio tu kuhusu kuuelewa ulimwengu halisi ulivyo lakini pia kuelewa maisha baada ya kifo na au lengo la maisha.

Kama wewe unaelewa vizuri Physics, Mathematics, Biology, Chemistry na Geography utaelewa kwamba elimu hizi zinafafanua vizuri Teolojia (Biblia) kwa lugha au kwa namna inayoweza kueeleweka na kila mtu
Nimekuuliza, hiyo teolojia ni nini?

Hujanijibu.

Mpaka sasa unatajataja kitu ambacho huja ki define.

Kanuni za kujieleza vizuri ni kuanza na definitions.

Narudia.

Teolojia ni nini?
 
Hebu niumbie mtu kama wewe anayekula na kwenda choo, na ukimaliza uniumbie Galaxy Moja tu kwa njia ya sayansi uniwekee maji, jua, mwezi na asili zote uje unikabithi, hivi hujiulizi hao wanasayansi kama wanauwezo wa kuumba galaxy Sasa kwanini waishi katika huu mfumo wa shidashida? Si wangetengeneza edeni Yao nje ya huu mfumo unaojiendea wenyewe tu bila kusema Kuna future kulingana na matendo ya mtu? Tena wamekaa tu eti wanasubiri hiyo nature iwaletee majanga, jamani hii zawadi tuliyopewa tujifunze jinsi ya kuitumia tupate Neema.
Wapi nimekwambia wanasayansi wanaweza kuumba galaxy?

Mbona unaleta fallacies za logical non sequitur hapa?

Nikishindwa kuumba galaxy, hilo linathibitisha Mungu yupo?
 
Mimi hapo ndipo nakupendea Kate.

Wewe mkweli ukipata sintofahamu huoni vibaya kukubali. Watu wengine unawaona kabisa hapa wakitumia mantiki lazima wapate sintofahamu, halafu unaona kabisa wanajitoa akili kutetea kitu ambacho hakina mantiki.

Huwezi kumuelewa huyo Mungu.

Kwa sababu hayupo.

Habari za kuwapo kwake ni habari zilizotungwa na watu tu walioamua kupambana na hali zao.

Wakaweka sheria, wakaona hizi sheria tukitaka watu wazifuate, tuseme ni za Mungu, hawa watu walivyo wabishi, tukisema ni za watu tu, hawatazifuata.

Ndiyo maana ukichunguza sana, imani ya dini/Mungu inaendana sana na tawala kubwa. Serikali. Mesopotamia/Misri/Uyahudi, Uchina, Ugiriki, Roma, Ufaransa, Uingereza mpaka leo Marekani.

Hata leo utasikia watawala wanajinasibu na dini.

Rais Mkapa alikuwa haendi kanisani. Kanisa lake lilikuwa Palm Beach Hotel na sakramenti yake ilikuwa Scotch Whisky.

Baada ya kupata urais tukawa tunamuona kanisani pale St. Immaculata Upanga. Alivyomaliza urais, tukawa hatumuoni tena kanisani.

Slijua kuwa ili kuonekana kiongozi mzuri, ilimbidi akae karibu na dini, na yeye Mkatoliki, ikabidi aonekane kanisani.

Dini na imani ya kuwapo Mungu ni hadithi tu za tungo za watu kupambana na hali zao.

Watu wana uwezo mkubwa sana wa kutunga uongo na kuufanya uwe ukweli.

Wamechukua kipande cha karatasi, wamekichorachora na kukiwekea picha, na kupiga saini za watu fulani, na kupitisha sheria, wanakwambia hii ni fedha, US $ 100. Ukiwa nazo 2000 hizi, thamani yake ni sawa na nyumba.

Na tumekubaliana hilo.

Wakati kiukweli, ukiwa kwenye kisiwa kidogo, hakina watu, unakaribia kufa kwa njaa ukapewa uchaguzi uchukue US $ 200,000 au sahani ya wali kwa maharage, utachagua sahani ya wali kwa maharage, kwa kuwa hizo $200,000 haziwezi kukusaidia kumaliza njaa. Hazina inherrent value, value yake inatokana na makubaliano ya jamii tuliyojiwekea.

Muandishi nguli wa vitabu kama "Sapiens: A Brief History of Hunmankind" na "Homo Deus: A Brief History of Tomorrow" , Profesa Noah Yuri Harari anaita hii habari "manufactured reality".

Yani watu tuna uwezo mkubwa wa kutengeneza uongo tukaufanya uwe ukweli. Tumetengeneza nchi (stste, si land), tumetengeneza hela, tumetengeneza corporations, tumemtengeneza Mungu, mpaka tumejiaminisha kuwa hivi vitu vipo kweli.

Wakati ni sisi watu tu tumevitengeneza, kabla ya sisi kuvitengeneza havikuwapo.

Manufactured reality.

See some excerpts here.

Mungu kama kweli yupo nna mengi sana ya kumuuliza
Na kama hayupo basi liwalo na liwe
 
Back
Top Bottom