Kama kutakuwa na mapitio ya Intergovermental Agreement (IGA) kuhusu DP World mapitio hayo yapelekwe bungeni baada ya uchaguzi wa 2025

Next in Line

Member
May 16, 2023
31
33
Nimemsikia Waziri Mkuu Majaliwa akizungumzia uwezekano wa kufanya mapitio(review) ya azimio lililopitishwa bungeni Intergovermental Agreement(IGA) inayohusu uwekezaji wa DP World hapa Tanganyika. Bunge la sasa hivi la chama kimoja-1) lililipitisha azimio hilo "kwa kishindo" kama ilivyo kawaida yao kwa kura za NDIYOOO!

Kama alivyosema Professor Tibaijuka azimio zito na nyeti kama hili si la kupitisha kwa kura za NDIYOOOOOOOO! kama ilivyofanyika. Kwa misingi hiyo kama kutakuwa na mapitio (review) ya azimio hili basi lipelekwe bongeni kujadiliwa baada ya uchaguzi wa 2025 ambapo inategemewa kutakuwa na mjadala wenye uweledi kutokana na kuwa composition ya wabunge itakuwa si ya chama kimoja tena.

Kwa bunge la sasa hivi hamna kitu.
 
Back
Top Bottom