Kama kuna watu wameisoma na watazidi kuisoma namba basi ni walimu

CK Allan

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
2,729
5,923
anaandika mwalimu wangu

"Binafsi kama kuna watu walimpigia debe Ndalichako awe Waziri Wa Elimu basi nami nilikuwa mmojawapo
nilidhani sasa Yale Elimu na walimu vitarudi katika ubora wake lakini hadi sasa tunajuta zaidi ya usajili Wa "Pogba"
kwa mambo kadhaa tu yafuatayo utajua sasa tumepata Waziri ambaye hatukutegemea kabisa tangu kuumbwa misingi ya Dunia..
1.kufuta mtihani Wa form II
2.Mkanganyiko Wa udahili TCU
n.k

sasa nirudi kwenye mada kama kuna kundi lililosomeshwa namba effectively basi ni hawa maticha..

1.Suala la uhamisho...
kuna walimu walishakamilisha mambo ya uhamisho na wakauza vitu vyao wakitaraji majina na vibali kutoka mwezi Wa 7 as usually.. sasa ni mwezi Wa 10 hali zao huko walipo wanatia huruma..wanaishi kama mazombi sio mashetani..
2.kushushwa madaraja
kuna walimu walipanda madaraja kwa tabu sana na wakaanza kupokea mishahara ya madaraja yao baadae wakashushwa kupisha uhakiki (siku hizi umepewa jina jipya la utambuzi)
3.Nyongeza za mishahara..
hili sisemi maana wote tunajua umuhimu Wa nyongeza kwa mwalimu ambae hana posho yoyote sasa kuzunguuka na mshahara huo huo kwa miezi 15. plus mfumuko Wa bei hebu jaribu kuvaa viatu vyake..
4.Kufutwa kwa posho za kusahihisha mitihani..
hii ilikuwa ni fursa kubwa kwa walimu kupata hela mbali na mshahara mwalimu akitoka marking walau anaweza kununua hata godoro kwenye chumba cha watoto... sasa Leo imefutwa kwa madai eti wanafanya majukumu yao...vipi kuhusu wabunge wao wanafnya majukumu ya nani?.. hivi umkalishe mwalimu mwezi mmoja nje na familia yake halafu usimlipe posho?

mfano Mimi kila jioni nikitoka shule namchukua mke wangu Mariamu na watoto wangu watatu Imma,Joan na Cassandra tunaenda kwenye bustani Yetu ya mboga mboga hadi saa 12 jioni tunaweza kurudi na 3000-5000 sasa Leo hii unichukue ukanifungie huko nisahihishe mitihani miezi miwili halafu usinilipe?? hapana.
5.Elimu bure..
kiukweli swala hili ni pigo lingine kwa walimu...tofauti na mtazamo Wa wengi kuwa walimu walikuwa wanakula hela lakini ukweli utabaki kuwa kufutwa kwa michango kumewasononesha walimu...
mwalimu alikuwa na uwezo Wa kuagiza mchango Wa dawati kwa 35000 na yeye akabagain na Fundi akapata ile 5000 Mtoto akapata dawati mwalimu akapata ile 5000 sasa Leo hakuna michango na watoto wanakaa chini kwa asiyeamini hili aje pm nitampeleka shule NNE za wanafunzi wanaokaa chini..

mwisho..
Ukimya huu Wa mheshimiwa Raisi juu ya maslahi bora ya walimu unaashiria mambo mawili..
1.anaaply ile theory ya ni upepo tu utapita...yaani wapige kelele tu lakini hakutakuwa na nyongeza zaidi ya kutoa 2% za kodi.. AU
2.Anaandaa big surprise kuwainua walimu kutoka hali ya kudharauliwa hadi kwenda katika hali ya kuheshimiwa..hii inaitwa "chemical change"

nimeandika haraka haraka maana huwezi jua lini malaika atashuka.
 
Embu kaa na namba mbili.

Ukweli hata kwa kuangalia mkuu, anayo nia ya dhati kuifanya tanzania kuwa ya tofauti kabisa.

Na ndipo hali ya kukusanya nguvu mpaka kuumiza wengine inapotokea.
 
Walimu huhadaiwa na serikali kama uchaguzi unakaribia ili watumike kufanikisha malengo ya ccm,
Hapo umesema mambo mawili unayodhani, lakini la msingi na sekondari ni moja tu "ni upepo tu"
 
Tatizo wengi wenu mliingia na vyeti feki na serikali inalijua hlo ndo maana inawatumia kama chombo cha majaribio,mkizngua tu wanazuga kukagua vyeti feki.
 
Waalimu huwa ni watu wa kuteseka vipindi vyote lakini ukifika wakati wa uchaguzi unaweza kujiuliza kama taaluma yenu mmeisomea au mlienda kuichukua huko vyuoni !!!!!......

Huwa mnarubunika kirahisi katika kufanikisha matakwa ya kisiasa lakini baada ya hapo huwa hamkumbukwi na hii ni kama cycle mliyoizoea.....
Vyama vyenu ni simba asiye na meno ya ncha Kali serikalini

Wengine walimchagua kikwete kwa sababu ya mama salma ni mwalimu mwenzao hivyo, mazingira yenu yangeboreshwa ..
sasa nikajiuliza huwa mnafundisha ujinga gani huko mashuleni hadi logic ya kawaida inawashinda !!!!.....

Siwalaumu ila Endeleeni kuvumilia hadi akili itakapowakaa sawia
 
walimu wanafki sana likija swala la uchaguzi wanatumika kama big g uchaguzi ukiisha wanatemwa na cwt yao hawa watu ni ccm B kipindi cha kampeni waliitwa lumumba kupitia chama chao cwt katika ukumbi wa shule ya msingi lumumba kujipanga kufanya kampeni na kuhamasisha walimu wenzao waipigie kura chama kikuu wakapewa elfu ishirini wakaitwa tena mananyamala wakapewa buku tano leo mnalalamika nini anzeni kwanza kuilalamikia cwt sio chama cha kuwasaidia walimu ila ni chama chakinyonyaji kupitiliza walimu hawa hawajiamini kabisa
 
Hapa kuna hatari la kutokea kwa anguko la elimu.Mh.waziri kama serikali haiwezi kulipa gharama,bora michango ya mitihani irudi. Yawezakuwa bajeti haitoshi ila kwa maamzi ya kufuta posho ni hatari zaidi ya kuwachangisha wazazi fedha ya mitihani.
 
Ni kweli kabsa uku kwetu mitihani ya mock form 4 wamesahisha siku mbali tu, kukata tu majibu nahisi hata mtihani wa taifa watakao enda kusahisha kukata hakuna kusoma jibu word to word, ni bora kumaliza mapema kuwahi kurudi nyumban kutafuta pesa kuliko kukaa ughaibun bila posho
 
Back
Top Bottom