Kama kuna Polisi mwenye Division One, basi vyeti si vyake

Kama kuna Polisi mwenye Division One, basi vyeti si vyake

Pamwanya

Senior Member
Joined
Jun 19, 2013
Posts
173
Reaction score
23
Nimejaribu kufanya utafiti na kufuatilia msingi wa elimu ya Askari police nikajua hakuna mwenye div.1 ya O level wala Advanced level.

Ndipo nikabain kuwa ndio maana wanafanya mambo hovyo, kumbe hata uwezo wao wa kuelewa mambo ni mdogo sana kutokana na msingi mbovu wa elimu zao. Vile inatokana na wengi kusoma shule za ajabu ajabu kutokana na vipato vibovu vya wazazi wao.

Wanaishi kwenye makazi mabovu eg Buguruni sokoni,lakini hawezi kohoji makazi kama mabanda ya nguruwe, Na bado wanafanya maamuzi ya kijanga jinga,kama waliyofanya kwa Prof.Lipumba, UDOM, mwenyekiti wa wafanyabiashara,mwangosi na wengine wengi.

Muulize rafiki yako askari matokeo yake ya shule yakoje?
 
Nilishawahi sikia kuwa mapolisi waliostaafu wakiwa na vyeo vya juu huwa hawapewi ubalozi na vyeo vingine kama wakuu wa mikoa n.k kama ilivyo kwa wenzao wastaafu wa JWTZ kwasababu wengi wao huwa elimu yao ni ndogo sana. Kuna ukweli ktk hili?
 
Nimejaribu kufanya utafiti na kufuatilia msingi wa elimu ya Askari police nikajua hakuna mwenye div.1 ya O level wala Advanced level. Ndipo nikabain kuwa ndio maana wanafanya mambo hovyo, kumbe hata uwezo wao wa kuelewa mambo ni mdogo sana kutokana na msingi mbovu wa elimu zao. Vile inatokana na wengi kusoma shule za ajabu ajabu kutokana na vipato vibovu vya wazazi wao. Wanaishi kwenye makazi mabovu eg Buguruni sokoni,lakini hawezi kohoji makazi kama mabanda ya nguruwe, Na bado wanafanya maamuzi ya kijanga jinga,kama waliyofanya kwa Prof.Lipumba, UDOM, mwenyekiti wa wafanyabiashara,mwangosi na wengine wengi.muulize rafiki yako askari matokeo yake ya shule yakoje?

wengi wao wanavyeti feki na wanajulikana kabisa wachache sana waliowasafi.
 
Siku ukingia anga zao ndio utajua kama wajinga ama werevu.

ni werevu kwa kula rushwa kusaidia majambazi na kubambikia watu kesi tushaingia anga zao tunawajua na ndio maana wanaporwa smg kwa kutishiwa visu na ni majinga sana hasa kwa kulinda raia na mali zao.
 
division one ya kukimbiza wezi labda na kusachi watu wakati wa maandamano
 
Ni uzembe wa kufikiri kukiri kuwa Polisi woote hakuna ambaye alipata Division One kwenye mtihani wa Form Four or Six.
Tunao wengi askari wenye character hizo.............
Pia ni upofu na ulemavu kweli wa akili kufikiri na kuamini kuwa polisi wanayafanya yale wayatakayo wao....No thank you.
Polisi ni jeshi, Jeshini unafanya kazi kutokana na orders from your superior hata kama una division one with 9A's na your superior ni std seven leaver you have to obey his/her order... That what we call displine..........
 
mentor div ii mzumbe o level pts 18, div i a level hapo hapo mzumbe. point 7, udsm upper 2nd class hons.

na ni polisi na bado ni polisi.

cv ya mtu, haina uhusiano na kazi anayofanya. kama uko smart, je umefanikiwa kuliko nape?

leta matokeo tuone na kazi uifanyayo maana hujielewi.

pia fuatilia cv ya dk enos lukyaa PhD
 
Ila asilimia kubwa wengi ni failures na wanatumia vyeti sio vyao kwa hili ninalifahamu msiulize kwa Nini, ila suala la utendaji kazi wao nadhani ni upuuzi wa wengi wa viongozi wao, wanadhana za upolisi wa kizamani na tactics za kishamba sana
 
Nakuunga mkono, na wengi wameingia huko kwa vimemo !!
 
  • Thanks
Reactions: amu
Nimejaribu kufanya utafiti na kufuatilia msingi wa elimu ya Askari police nikajua hakuna mwenye div.1 ya O level wala Advanced level. Ndipo nikabain kuwa ndio maana wanafanya mambo hovyo, kumbe hata uwezo wao wa kuelewa mambo ni mdogo sana kutokana na msingi mbovu wa elimu zao. Vile inatokana na wengi kusoma shule za ajabu ajabu kutokana na vipato vibovu vya wazazi wao. Wanaishi kwenye makazi mabovu eg Buguruni sokoni,lakini hawezi kohoji makazi kama mabanda ya nguruwe, Na bado wanafanya maamuzi ya kijanga jinga,kama waliyofanya kwa Prof.Lipumba, UDOM, mwenyekiti wa wafanyabiashara,mwangosi na wengine wengi.muulize rafiki yako askari matokeo yake ya shule yakoje?

Lazima tuwe wakweli. Hiyo ilikuwa zamani kidogo. Miaka ya hivi karibuni hali imebadilika kufuatana na ukosefu wa ajira.

Zamani ilikuwa failures wote wanaenda ualimu (Div IV karibu na zero). Waliobaki ndio hao walienda polisi. Ndio maana kulikuwa na usemi - umekosa hata ualimu?

Siku hizi graduate wazuri wa fani zote wanaenda polisi na magereza.
 
Ila asilimia kubwa wengi ni failures na wanatumia vyeti sio vyao kwa hili ninalifahamu msiulize kwa Nini, ila suala la utendaji kazi wao nadhani ni upuuzi wa wengi wa viongozi wao, wanadhana za upolisi wa kizamani na tactics za kishamba sana

Kweli mkuu leo mchana nimepigiwa simu jamaa yangu amekamatwa jana usiku na yuko mahabusu kituo kidogo.Nimeenda nikakuta kweli nikauliza amefanya kosa gani? nikajiniwa aliyemkamata ni mkuu wa kituo na yeye ndiye anayejua kosa lake, ila uje baadae maana muda huu bosi ameenda kulala. Nikauliza tena kwa hiyo mtu amekamatwa jana usiku mpaka leo mchana kosa lake halijulikani? Sikupata majibu.
 
Kama uliyoyaandika yana ukweli basi ndio haya mambo yanayofanya polisi kuonekana shuleless maana mtu ambaye upstairs yupo sawa hawezi kufanya kazi kwa mazoea tu. Tatizo la polisi hawataki kubadilika kabisa yani tatizo polisi wenye weledi ni wachache sana so wanamezwa na mang'aa walio wengi zaidi. Tumekuwa tukilalamika hawa polisi wa pikipiki 'voda fasta' wasiwe wanakagua magari huku wamebeba bunduki ikaonekana kama hatujui kazi zao Sasa imagine kilichotokea Tanga polisi kunyang'anywa bunduki kwa kisu tu nadhani kama wana akili basi watalifanyia kazi. Wanazifahamu rules za ubebaji bunduki sasa sijui kwa nini wanaruhusiwa kukagua magari tena anainama kabisa anakuuliza swali huku kaegemea gari. Elimu yahitajika sana kwa viongozi wao maana wanaweza kuwa wasomi wazuri tu ila bado wakawa wanafanya kazi kwa kufuata mfumo wa zamani sana. Waige JWTZ hakuna mboyoyo kama huna elimu cheo subiri kwa ukakamavu wako ila kama una shule unalamba uofisa kwanza maana askari aliyeenda shule ni mtaalamu mpe kazi za kitaalamu halafu hawa failures peleka wakapige jalamba wasubiri wataalamu wawape maelekezo huo ndio weledi katika jeshi sio mtu anafanya kazi kwa mazoea halafu unamuita askari.
 
usiwachezee hawa jamaa waache kama walivyo ,wanaweza kukutafututa ulipo wakakupa kichwa ukasota nacho. japo ulichokiongea ni ukweli mtupu huwezi kuta proff au doc huko.
 
usiwachezee hawa jamaa waache kama walivyo ,wanaweza kukutafututa ulipo wakakupa kichwa ukasota nacho. japo ulichokiongea ni ukweli mtupu huwezi kuta proff au doc huko.

Hapana, kuna jamaa ana PHD namfahamu yupo vizuri sana ila hata yeye yupo kule kimaslahi PHD yake anaitumia kwa mambo mengine kabisa na hawamtumii kabisa kama mtaalamu wa ndani, hiyo ndiyo tatizo kwa sekta nyingi za serikali yetu.
 
Back
Top Bottom