GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,551
- 108,888
Hili halipingiki kabisa na wala halihitaji sijui akina TWAWEZA wala akina Professor Mruma na Professor Osoro kulifanyia Utafiti kuwa 95% ya Wakazi wa Dar es Salaam ( ukiondoa Mimi tu Mjanja ambaye nipo huku Kwetu Mkoani Gisenyi nchini Rwanda ) chakula chao / chenu Kikuu ni Chips tena kuna wengine huanza kuzila na Chai ya asubuhi.
Hivyo basi kwa Utafiti / Uchunguzi wa kitaalam kabisa ambao majibu yake yapo katika Gazeti la The Guardian la leo tarehe 17th June 2017 naona kuna Fursa moja kubwa mno inakuja hasa Jijini Dar es Salaam ya Kuuza Majeneza kwani muda wowote kuanzia sasa Wakazi wengi wa Mkoa wa Dar es Salaam wataanza Kupukutika kwa Kufa.
The Guardian la leo wameandika hivi katika front page yao nami nanukuu tu Headline yao " Eating Chips twice a Week can double your chance of death " mwisho wa Kunukuu. Ukitaka ujue ni jinsi gani utakavyoanza Kufa kwa kupenda Kwako kula Michips hovyo hovyo basi tafuta nakala yako ya The Guardian ili utiririke na userereke nalo vizuri.
Mnaokula Chips hovyo hovyo na 24/7 nawatakieni Vifo vyema na hakikisheni tu kuwa huko mnapotutangulia basi mnatuwekea pia na sisi Wajanja ambao hatuli Chips na hatufi leo wala kesho na kama ikitokea tumekufa basi huo pia ndiyo utakuwa mwisho wa dunia.
Nawasilisha.