Kama January Makamba ana mpango wa kugombea Urais 2030, namshauri akabatizwe kwa maji mengi mapema

Hujui unaloliongelea wewe...hivi unamjua Kigogo alikuwa nani?...umesikia tena Kelele za Kigogo baada ya Mwendazake kuondoka?
Baada ya kupata teuzi Mkuu ndio akatulia, aliendelea kutukana na kupinga serikali hata mwendazake alivyotutoka Mpaka alipopata teuzi ndio akaja kutulia

Sasa hivi anapost kusifia wakina Nape na Mzee Makamba Mungu alivyomkali anamdhalilisha

Amefuta post zote za Zamani kabla teuzi zile za kumtukana mama. Jk na serikali yote kwa ujumla

January na dada yake Walikua na ugomvi na mange sasa hivi wamepatana na kwa hivyo anamtumia Mange Kimambi na alimuaminisha Mange kua Mwigulu atatumbuliwa na Kimei anaenda wizara ya Fedha, Mange akapost hakuna kilichotokea Mungu alivyomkali























 
Kuna mmoja kati ya hao mkimchagua atakuwa zaidi ya JPM hasa upande ule wa hasi.

Mungu alishayafunua na kuonesha wazi.

Tumshukuru sana Mwenyezi Mungu hilo.
 
Kuwa kiongozi wa watu siyo jambo la lelemama wala majaribio.

Lazima uwapende kwanza watu wote bila kujali tofauti zao.

Na siyo chuki na kuumiza watu na hata kutaka kuwaangamiza kwa sababu mbali mbali.
 
Daah umenikumbusha mbali....maskini deo...mkewe mzuri kaishia kuliwa na zito
 
Ngoja tuone....nje ya baraza la mawaziri atoke rais? Haaa sijui
 
Kwa post hii ndipo ndugu yangu Pascal Mayalla uibuka na kauli ya "Duh!". Si kwa ufungukaji huu!
 
Ww mbona muongo hivi....toka lini january akawa mvaa rozari......mchekini mwigulu vizuri ndio material tegemewa upande wa kaisari....hatujapata mtu mwingine....nyie endeleeni kumzarau hivyohivyo lakin kuna jambo kwake
Acha kutaja wajinga wajinga kwenye mambo serious
 
Miaka 10 ijaya atakuwa na 75 years...unadhani watu watakuwa wanamuelewa?
Wahusika wamtunze kijana fulani atakaye livusha taifa. Lakini, ni jambo la kusikitisha muda huu kujadili uchaguzi wakati watanzania bado hawaoni muendelezo wa kuwavusha kutoka utegemezi....!!!!
 
Awe mgalatia asiwe mgalatia wasaka urais kwa mtindo wa makamba kawaida ni wapigaji hawafai. Kwa wengi tunataka magufuli mpya 2025 sio 2030. Nchi inahitaji iwe chini ya mtu anavaa viatu size ya magufuli ili twende mbele.
Inshalah mama atatuvusha salama.
 
Yule uliyekuwa unamuabudu jpm alivyokufa ulinuna au ulitaka kujinyonga!? Naona umeisaliti Sukuma gang . Sasa hivi timu MAMA..Mgeni Aje Machinga Afukuzwe
Mimi ni mtanzania halisi msimamo wangu unakwenda na Rais aliye hai anayepewa manifesto ya CCM.

Sina ushamba wa kuwa team fulani ya Kiongozi fulani huko nimeshavuka siku nyingi.

Mama Samia unae mpaka 2030 tukiwekwa hai.
 
Mimi ni mtanzania halisi msimamo wangu unakwenda na Rais aliye hai anayepewa manifesto ya CCM.

Sina ushamba wa kuwa team fulani ya Kiongozi fulani huko nimeshavuka siku nyingi.

Mama Samia unae mpaka 2030 tukiwekwa hai.
Manifesto ya chama ni ipi!? Kuna corona au hakuna corona!? Machinga wafanye biashara mpaka ikulu au machinga ni wezi wanaibia wageni wetu wanaotupa mahela!? Hiyo manifesto bila shaka ni upuuzi mtupu. Hata jpm tulijua atatawala milele.
 
M
Mkuu hivi unaelewa maana ya maendeleo? We unajichanganya sana. Umesema mama anaomba ha na anapewa sasa hayo si ndo maendeleo. Au ulitaka tuzokatae hizo hela ili maendeleo yajilete yenyewe automatically bila hela. Labda mi sijakupa vozuri!!
 
Manifesto ya chama ni ipi!? Kuna corona au hakuna corona!? Machinga wafanye biashara mpaka ikulu au machinga ni wezi wanaibia wageni wetu wanaotupa mahela!? Hiyo manifesto bila shaka ni upuuzi mtupu. Hata jpm tulijua atatawala milele.
JPM yupo kaburini huu mwezi wa saba unakwenda wa nane. Wewe ni wale wenye machungu, hueleweki. Unamchukia JPM, unamchukia Samia, akija mwingine pia utamchukia.

Punguza unyonge usio na sababu.
 
Hizi ndo mada pendwa kwa CCM na Wafuasi wao...

Mkitoka kwenye Ukristo, mtahamia kwenye dhehebu....

Mkitoka kwenye dhehebu mtahamia kwenye ukanda...

Mkitoka kwenye ukanda mtahamia kwenye kabila...
 
Ni nani alieweka huo utaratibu? Ccm kila muda mnafikiria uchaguzi tu yaani uchaguzi mkuu umefanyika mwaka jana ila bado akili zenu zipo katika uchaguzi
 
Hizo ramli mnazopiga humu hazina kabisa maana hiyo 2030 unaweza kukuta tuko kama Ethiopia au Sudan sasa hivi. Chezeni hamjui dunia hii ilivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…