Kama huwezi kudeal na wanawake zaidi ya mmoja, pambana na huyo huyo!

FourTwoNet

JF-Expert Member
Aug 4, 2022
1,235
2,497
Wakuu!!!

Akyanani...ata salamu haiji, naenda straight kwenye format ya leo. Kama unataka anzisha familia ya wife zaidi ya mmoja....wanaume naomba jamani kama wewe ni ule ukipewa kachumbari na mwanamke utie muhogo afu unapoteza fahamu za kiume....yani unasimp....unakuwa tena huna maamuzi na kila itakapokupelekesha iyo kachumbari unaenda tu kichwa kichwa(kichwa chenyewe unachotumia ni icho cha down stairs), please....mmoja anakutosha.

Maanake ii mambo ya unaanza vizuri na mke wako...baadae unavuta ingine inaelewa kabisa una familia na watoto...lakini inawachukia iliowakuta, mpaka watoto wako...yani inaamini inaweza kuwa mke wako wa kwanza, kitu ambacho ni sawa na mtoto wa pili kutaka kuwa first born...hiyo mambo hapana tambua.

Na wewe ulivyo pimbi unaendekeza ujinga, unaendekeza matabaka, unaendekeza upendeleo, unaanza kutamani usingekuwa na mke wa kwanza...afu unavyo endelea kujifanya kidume, kumbe fahamu zishakuwa za kike. Tafadhali...kwa heshma yako, elewa uwezo wako. Shenz type.

Kama unataka zaidi ya mmoja, hapana pelekeshwa, kwanza kila mmoja anafaa awe na nyumba yake na wewe uwe na yako kivyako....sio unaishi na mmoja mwingine ajiskie ni wa pembeni. Iyo ni ujinga. Si umeamua ni wawili, kama hauwezi lala nao kitanda moja, basi kila mmoja awe na space yake....na wewe uwe na yako. Unapojiskia, unatembelea pande zote kwa usawa...kitakachofanywa huku, kifanywe kule. Ata kama una wake saba...si umeamua? Basi balance muhimu.... kama ni sherehe, sjui birthday ya mtoto, sjui birthday ya mke wako flani, sjui ubarikio, au kitu cha kufanya pamoja...basi wote waje wakifanyie kwako...kila mtu ashirikishwe...na hafla ikiisha kila moja ana kwake. Na ukiona anaetaka kuleta upuuzi, unamuonya haraka ipasavyo...

Maanake vitu vingine tunafanya kibishi kibabe, kumbe tunajivuruga wenyewe kuwaletea watoto wetu psychological problems...matokeo yake unaweza ona umetumia ela kupeleka mtoto shule kumbe wewe ndo unamvuruga na stress, alafu pombe na bangi ndio iyo. Au sjui mtoto wako mmoja anasoma international...mwingine shule ya serikali kiatu alivaa iyo moja kutoka class 1 mpaka 7. Iyo ni ujinga...na ni kujitakia laaana.

Ndo maana wazee wa zamani ilikuwa ni kila wife ana nyumba yake, na mzee ana yake...na kila kitu kilikuwa kinafanywa kwa usawa.

Kama mfuko haiwezi ruhusu iyo mpangilio basi tuliza mshono, kanywe maji, tafuta mchepuko, tandika iyo kitanda mpaka shuka ipande...alafu rudi home kwa wife yako huyo mmoja. Ala!!!!

Hapana laumu mwanamke hapa.
 
Hivi kweli waliiooa mke zaidi ya mmoja hua hawana upendeleo kwa mke mmoja????
 
Hivi kweli waliiooa mke zaidi ya mmoja hua hawana upendeleo kwa mke mmoja????
Kuna wazito wanaoelewa wanafanya nini kama Kunguru wa Manzese apo ivyo....ila kuna wengine ni vibendera fuata upepo...ndo maana utaskia oooh queen darlene kamchamba sjui mke wa kwanza wa isihaka....mara sjui mke wa isihaka kamchamba queen darlene kwa sababu mumewe karudi kwake....ukiona ivyo, jua tu uyu Isihaka ndo mwanamke mkubwa kati ya hao wake zake.
 
Back
Top Bottom