Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,180
- 7,356
Ni jambo la kawaida kwa marafiki walioshibana kutambulishana wapenzi wao. Mara kadhaa, rafiki yako au ndugu yako anaweza kukutambulisha kwa mtu wake na baadaye kukuliza, unaonaje.. unadhani ananifaa kuwa mwenza wa maisha?
Sometimes unaweza kuingia mkenge na kuanza kumchambua mtambulishwa, na kama kuna dosari zilizogundulika kufikia hata hatua ya kushauri kuwa aachane naye kabisa, hamfai... na maneno kama hayo.
Hakuna kosa kubwa kama hilo, uzoefu unaonyesha kuwa wengi wanaishia kwenda kuwaambia hao watambulishwa jinsi walivyopondwa na wewe... na hapo unaonekana mbaya, wivu, hasidi na maneno yote mabaya...
Kama mtu kaona yeye kuwa anamfaa, bora usitie neno, na kama kuna walakini atakuja kuuona. Sana sana kama unaona kuna kasoro kubwa, tumia ushawishi wako kuchelewesha pingu za maisha baina ya wawili hawa ili mwenyewe apate nafasi ya kuziona dosari zenyewe...
Hata hivyo ushauri huu hauapply pale unapotakiwa kumuokoa rafiki/ndugu yako na miwaya...