Kama hutojali, tupe siri yako ya kupata usingizi haraka usaidie wenye tatizo hili

Kuna msemo kwamba "Mafundi seremala ndio wanaoongoza kwa kupata usingizi mzuri." Jiulize kwa nini? Usingizi ni sehemu ya burudani kwa mwanadamu. Burudani yoyote ile inahitaji maandalizi ili mwili uifurahie.

1. Hakikisha mwili umelishwa vizuri na kuchoshwa kwa kazi halali ya kipato
2. Hakikisha akili imelishwa chakula chake bora na cha kiafya
3. Hakikisha moyo wako umesafishwa na hauna mzigo wa husda, chuki, wivu, na negatives kama hizo

Hapo dakika 5 tu ushasinzia sana tu, wanaweza kukuhamisha hadi Kongo bila kujua
Upo sahihi100 % watu hawafanyi kazi ipasavyo, hawali wamejawa husuda kutazama ya watu ndo maana usingiz inakua tabu mm niingiapo kitandani siwez zid dakika kumi hadi kumi na tano nipo fofo.
 
Kuna msemo kwamba "Mafundi seremala ndio wanaoongoza kwa kupata usingizi mzuri." Jiulize kwa nini? Usingizi ni sehemu ya burudani kwa mwanadamu. Burudani yoyote ile inahitaji maandalizi ili mwili uifurahie.

1. Hakikisha mwili umelishwa vizuri na kuchoshwa kwa kazi halali ya kipato
2. Hakikisha akili imelishwa chakula chake bora na cha kiafya
3. Hakikisha moyo wako umesafishwa na hauna mzigo wa husda, chuki, wivu, na negatives kama hizo

Hapo dakika 5 tu ushasinzia sana tu, wanaweza kukuhamisha hadi Kongo bila kujua
Awamu ya 5 hili tatizo linawakumba wengi na kwa maelezo yako ni vigumu kukidhi vigezo vyote.

1.Hivi unapataje usingizi wakati ajira yako inaweza kuota nyasi muda wowote?

2. Unapataje udingizi huu mwaka wa 5 unatafta ajira ila hata ajira ya kujitolea umeshindwa kupata.

3. Unapataje usingizi TRA wanaweza pita na pesa yako iliyotunza bank?

4. Unapataje usingizi jina lako lipo kati ya wadaiwa sugu wa HESLB na hujaajiriwa mpaka sasa?

5. Unapataje usingizi kabiashara kako TRA wanakavizia kukapiga ushuru mkubwa?

6. Unapataje usingizi kwa kuka mlo mmoja?

7. Unaoataje usingizi watoto wanadaiwa school fee?

Hayo ni baadhi tu
 
NI MUNGU TU.ila katika binadamu tunaolala vizuri Mimi nipo.

Yaani saa 1 usiku nimelala, tena usingizi mzito.nikishtuka saa 8 usiku nazuga kidogo nalala Tena mpaka saa moja asubuhi.

Nikiamka bado Nina usingizi
 
Kipindi nipo a level nilikuwa nalala sana yaani kile kitendo cha vipindi kuisha ni kula na kutafuta wapi kitanda kilipo nilikuwa nashangaa sana watu wanaocha usingiz na kuamka usiku kusoma. Ila siku hizi kutoka na majukumu hata mda wa kulala usiku naweza nisapate
 
Anayesimulia mvua ujue imemnyeshea, yawezekana kwa wengine ikawa ni mshangao wanaposikia kuna watu hawapati usingizi kirahisi, lakini hili tatizo linawasumbua watu kiukweli. Mtu anaweza kuingia kitandania saa nne usiku ila usingizi ukampata saa sita usiku.

Binafsi njia nayotumiaga ni kusikiliza kinanda laini kwa kutumia ear phones, kile kinanda laini hakika kwangi hakijawai kuniangusha
Ukipanda kitandani tu zima internet,fungua Biblia uanze kuisoma,utakuja kunishukuru baada ya wiki moja...
 
Ikifika saa 4 usiku nimelala ubavu kitandani Nina peruzi JF dakika 10 nyingi sana nishaangusha gari Hadi kushtuka saa 8au 9 usiku ndio mpaka kesho Tena

Yaani huwa naamka saa 9 usiku naperuzi tu mitandao
 
Kweli tupo wengi tunafanana tabia, yaani hata mimi nikilala ubavu na kuanza kusoma post za jamiiforums yani nastukaga asubuhi sijui simu ipo sehem gani 😂😂
 
Namkumbuka marehemu Ruge aliwahi kusema, yaani unakuta mtu anaenda kwa Dr anamwabia anakosa usingizi wakati kuna watu wanatamani kusingekuwepo usiku ili wafanye mambo ya maendeleo
My friend usingizi ni bomu la umasikini kuliendeleza

Acha kupenda kulala ovyo hebu angalia bill gate alanalala masaa 2 tuu, baraka Obama analala masaa 6 jiulize hayo mengine anafanya nini

Anafanya mambo ya maendeleo na si vingine.
 
Saa 6 YES
saa 2 PURE LIE
 
NI MUNGU TU.ila katika binadamu tunaolala vizuri Mimi nipo.

Yaani saa 1 usiku nimelala, tena usingizi mzito.nikishtuka saa 8 usiku nazuga kidogo nalala Tena mpaka saa moja asubuhi.

Nikiamka bado Nina usingizi
Haha. Hilo jina lako tu aisee. Nakushauri kamwone Dr mapema
 
Awamu ya 5 hili tatizo linawakumba wengi na kwa maelezo yako ni vigumu kukidhi vigezo vyote.

1.Hivi unapataje usingizi wakati ajira yako inaweza kuota nyasi muda wowote?

2. Unapataje udingizi huu mwaka wa 5 unatafta ajira ila hata ajira ya kujitolea umeshindwa kupata.

3. Unapataje usingizi TRA wanaweza pita na pesa yako iliyotunza bank?

4. Unapataje usingizi jina lako lipo kati ya wadaiwa sugu wa HESLB na hujaajiriwa mpaka sasa?

5. Unapataje usingizi kabiashara kako TRA wanakavizia kukapiga ushuru mkubwa?

6. Unapataje usingizi kwa kuka mlo mmoja?

7. Unaoataje usingizi watoto wanadaiwa school fee?

Hayo ni baadhi tu
Sasa kuna faida gani kuwa macho mchana na usiku while huleti solution yoyote, ya leo bora ya jana??? Nilisikiaga wakisema akili ni mali. Naona kwa baadhi, akili ni wali.
 
Back
Top Bottom