Kama hutojali, tupe siri yako ya kupata usingizi haraka usaidie wenye tatizo hili

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,014
Anayesimulia mvua ujue imemnyeshea, yawezekana kwa wengine ikawa ni mshangao wanaposikia kuna watu hawapati usingizi kirahisi, lakini hili tatizo linawasumbua watu kiukweli. Mtu anaweza kuingia kitandania saa nne usiku ila usingizi ukampata saa sita usiku.

Binafsi njia nayotumiaga ni kusikiliza kinanda laini kwa kutumia ear phones, kile kinanda laini hakika kwangi hakijawai kuniangusha
 
Kuna msemo kwamba "Mafundi seremala ndio wanaoongoza kwa kupata usingizi mzuri." Jiulize kwa nini? Usingizi ni sehemu ya burudani kwa mwanadamu. Burudani yoyote ile inahitaji maandalizi ili mwili uifurahie.

1. Hakikisha mwili umelishwa vizuri na kuchoshwa kwa kazi halali ya kipato
2. Hakikisha akili imelishwa chakula chake bora na cha kiafya
3. Hakikisha moyo wako umesafishwa na hauna mzigo wa husda, chuki, wivu, na negatives kama hizo

Hapo dakika 5 tu ushasinzia sana tu, wanaweza kukuhamisha hadi Kongo bila kujua
 
Kipindi nasoma Kunguni Mbu na joto, vilinifanya niende kitandani kwa lengo moja tu, kusinzia.

Naenda nikiwa nimechoka, Nikifika tuu Nazima.

Tofauti na hilo Mimi ni mmoja wapo wa wanaoutafuta usingizi kwa tochi,

Nina jamaa yangu ni kiboko,
Yaani akiona tu kitanda anaanza kukoroma.
 
Kuna msemo kwamba "Mafundi seremala ndio wanaoongoza kwa kupata usingizi mzuri." Jiulize kwa nini? Usingizi ni sehemu ya burudani kwa mwanadamu. Burudani yoyote ile inahitaji maandalizi ili mwili uifurahie.

1. Hakikisha mwili umelishwa vizuri na kuchoshwa kwa kazi halali ya kipato
2. Hakikisha akili imelishwa chakula chake bora na cha kiafya
3. Hakikisha moyo wako umesafishwa na hauna mzigo wa husda, chuki, wivu, na negatives kama hizo

Hapo dakika 5 tu ushasinzia sana tu, wanaweza kukuhamisha hadi Kongo bila kujua
Upo sahihi mkuu na hii mada ineshafungwa!

Hakuna kitu kibaya kama stress! Huwezi kupata usingizi wakati una vitu kibao unawaza
 
Kuna msemo kwamba "Mafundi seremala ndio wanaoongoza kwa kupata usingizi mzuri." Jiulize kwa nini? Usingizi ni sehemu ya burudani kwa mwanadamu. Burudani yoyote ile inahitaji maandalizi ili mwili uifurahie.

1. Hakikisha mwili umelishwa vizuri na kuchoshwa kwa kazi halali ya kipato
2. Hakikisha akili imelishwa chakula chake bora na cha kiafya
3. Hakikisha moyo wako umesafishwa na hauna mzigo wa husda, chuki, wivu, na negatives kama hizo

Hapo dakika 5 tu ushasinzia sana tu, wanaweza kukuhamisha hadi Kongo bila kujua
Nadhani baada ya swali kuulizwa na hili jibu kupatikana hapa ndio ingekuwa mwisho wa comments
 
Bahati mbaya mnashindwa kujifunza kwa watoto wenu wadogo.kwanini ikifika saa moja mtoto anasinzia mpaka akiamshwa analia!

Jibu ni uchovu wa mwili, usafi wa nafsi.

Watu wazima tumachoka akili,nafsi zimejaa mizigo.

Huwezi lala kirahisi hapo lazima nguvu itumike.

Kuna somo la meditation humu,lifuatiliwe.,ni njia bora ya kusafisha nafsi,kisha mazoezi ili kuuchosha mwili.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom