Kama hukuzaliwa mwaka 2000

1.Hakuna (mpira) kutoka nje wala refa hakuna

2. hakuna offside wala sheria za mpira

3.hakuna idadi maalum ya wachezaji ilimradi sawa kwa sawa au timu moja kuzidi mchezaji mmoja

4.wakati idadi haijafika kiasi cha kuunda timu mbili (wachezaji 5+ each team) basi kunachezwa gombania goli kwanza huku tukiendelea kusubiri wadau wengine

5.mgawanyo wa wachezaji (pale kati wakati wa kuita) unaweza kufuata njia moja kati ya
(a)kuita kwa kuzingatia usawa katika kila kitu mfano kimo, nguvu, ufundi, ubabe, umbo, hali ya maisha- watoto wa vibopa au wa mahohehahe nk AU
(b) kupanga mstari kisha kuitwa kwa muundo wa "JUU, CHINI" ambapo wa kwanza akienda goli la upande wa juu anayefuata ataenda goli la chini hivyohivyo mpaka mnaisha timu zimepatikana na hapa ndo ilikuwa kimbembe pale kunapokosekana uwiano

6.mpira ukiwa unaendelea basi kila wanaokuja wataingia kwa mtindo uleule wa mmoja akiingia timu A anayefuata ataingia timu B

7.ikiwa mmekuwa wengi sana mpaka mnashindwa kuucheza mpira vizuri basi wengine mnajiengua na mnafanya mawili kati ya
(A) kuunda timu kutoka (yaani mnakaa benchi kisha timu itakayofungwa inatoka ili na nyinyi muingie- mara nyingine timu kutoka zinafika hata tatu na hapo ndo kutoka ni goli moja tu)
Au
(B)kuunda timu mbili nyingine na kukianzisha kwa kando (yaani mechi zinakuwa mbili katika viwanja viwili kwenye eneo moja kwa wakati mmoja)

8.mwamuzi ni muda (giza/jua) lakini muda mwingine mwamuzi anaweza kuwa "Mpira wa Buti" ambao unapelekea ngumi au mwenye mpira wake kuutia kwapani na kukimbia kama akiweza

9. Hakuna kumkata buti mwenye mpira utatafuta matatizo (mwenye mpira mara nyingi anakuwa m'babe au ana mafungamano na wababe)

10.jioni jioni kuna mtindo wa uchezaji unaitwa "mpira wa buti" au "kata buti" au "mpira wa kukatana" ambapo huo muda ukifika wachovu wote mnatahadharishwa kabisa mkae kando (maana muda huo hauchezwi mpira bali mwenye mpira - yaani ukiwa na mpira unawahi kuupasi kwa mwenzio ukichelewa tu au kuzubaa utajikuta upo chini saa nyingi sana na mpira huna)

11. Hakuna kupiga dochi (ndole/ndochi) na ukifanya hivyo mara kadhaa unaweza kutolewa mara moja maana utafumua mpira

12.kuna muda wa kucheza butua butua ambapo unapiga mishuti unavyoweza hata dochi ruksa lakini kuwa makini kwamaana ukisikia butuabutua ndo muda ambao wahuni wanaingiza uwanjani mipira yenye mawe ndani

13.hakuna mtoto wa kike maeneo unapochezwa mpira huo ( wao utawaona kwa kando tu wakicheza rede zao- japo kuna majike dume mda mwingine mnacheza nayo)

14.mwezi wa RAMADHAN hakuna kata buti- ni dhambi

15.saa nne (short break) ni muda wa one touch kwa wale wasioenda nyumbani, saa 6-7 (break) ni muda wa chenga na kuanzia saa 9 ni mchanganyiko sasa mpaka jioni
*Ufafanuzi kwa yule asiyejua one touch ni mchezo wa mpira wa miguu kwa wachezaji wawili au mipira miwili kwa wachezaji wanne yaani wawili kwa kila goli*


Ngoja niishie hapa maana sheria ni nyingi na uzuri hazikuwa (na idadi) maalum nyingine zilikuwa zinajitokeza humohumo mnacheza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kibonge kuliko wote anakaa golikipa.
😂😂😂😂 kuna jamaa alikuwa ananitesa sana kumfunga, alikuwa kibonge kweli. Issa sijui sasa hivi unadaka nini uko uliko mana sio kwa sifa zile za udakaji wako na ubabe juu.
 
Ukipigwa tobo linawekwa tuta!Mpaka leo sijawahi kuelewa kwanini mtu akishika tulikuwa tunasema "Enzi"!
 
Faulo au penati mpaka mtu ashike labda upgwe buti hdi ushndwe kunyanyuka ndo tutakuonea huruma..
Faulo ya kwanza haikingwi
Faulo inakingwa mpira ulpo hapo hapo hamna kusogea hata hatua moja
Mwenye mpira ndo anapiga penati
 
Kama mechi inaendelea! Alafu akaja mchezaji anaejua na kila mtu anafahamu kwamba huyu mchizi anajua .Mechi lazima isimame ili tujue hatima yake


Noma sana
 
Back
Top Bottom