Kama hukusoma/husomi chuo cha serikali, pole sana!!!

Kama hukusoma/husomi chuo cha serikali, pole sana!!!

Najua mnaosoma vyuo vya st, mmenielewa.
1. Hawa ndio wanaoongoza kwau uoga
2. Hawa ndio wanaoongoza kwa kuishi maisha kama ya primary au secondary ( sheria za vyuo)
Ongezea na mengine
Sioni unawapa pole ya nini, kama walichagua hivyo vyuo na wako smart watakua wamesoma student by-laws na sheria nyingine za vyuo hivyo. Issue ya uoga tujiulize ni uoga wa nini? Unauthibitisho gani kuwa ni waoga? Naishi karibu na chuo cha St. na pia nina ndugu anasoma chuo kingine cha St. sijaona wala kuthibitishiwa hayo unayosema. Nakumbuka ndugu yangu yule alianza kulalamika kuhusu mavazi-nikamuuliza umesoma hizo sheria akawa hajasoma, nikamuelekeza tafuta mtu anaesoma huko uulize alipouliza akakuta mambo tofauti. Amekwenda huko anafurahia maisha hapo. Kama kuna unalojua weka vitu vyenye uhakika.
 
Man usijaribu kuvipandisha vyuo vya serikali. Mm nimepata bahati ya kusoma vyote. Both private na goverment... na nikwambia tu at the end ni juhudi zako mwenyewe...
Usipo jishughulisha utatoka empty
Hapo nyekundu uko sawa 95%. F6 wanaanza mitihani hivi karibuni. Taarifa kama za mleta uzi zisizo na ukweli kwa ujumla wake zinawachanganya vijana wasio makini wakati wa kuchagua vyuo na matokeo yake wengi wanafanya uchaguzi usio sahihi. Na kama CAS itafutwa kama JPM anavyotaka ni vijana wengi tu watakutana na kiama kwa kufikiria vyuo vya serikali ndo vyuo. Kila chuo kina mazuri na mabaya yake hivyo mtu aeleze kitu chenye uhakika sio kitu ambacho hakina chembe za ukweli. Vyuo vikuu havina nafasi za kutosha (vyumba) hivyo itakuwa jambo la ajabu kulazimisha vijana wakae madarasani hata kama hawana darasa. Pili huyo anaechukua roll call anatoka wapi wakati anatakiwa awe anafundisha au kwenye majukumu mengine.
 
Back
Top Bottom