Mwlmgomaji
Member
- Aug 3, 2012
- 93
- 6
Kuna mtanzania mmoja ananiambia Chama Tawala kiliahidi maisha bora kwa kila mtanzania. Gharama za maisha zimepanda, Gharama za usafiri juu. Hata mayai ya kienyeji na yenyewe juu yani yai moja mia saba mitaa fulani ya iringa huku. Nusu kilo ya nyama 3000/=. Vocha ya 450/= inauzwa 500/=. Anasema akili hamchezi. Mie namwambia wewe ni mwananchi tena mkulima. Mie mfanyakazi napokea mshahara laki tatu na themanini richa ya serikali kutuongezea asilimia 14 lakini makato yako juu sana kama 80elfu nzma inarudi kwao. Nae anashangaa. Ko jamani. "Maisha magumu kwa kila mtanzania"