Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali ya Magufuli ni Serikali Haramu. Hukumu ya Karma ii Juu Yake!. | Page 8 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali ya Magufuli ni Serikali Haramu. Hukumu ya Karma ii Juu Yake!.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Oct 29, 2015.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,640
  Likes Received: 23,836
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Kuna hii tuhuma iliyotolewa leo na Edward Lowassa.

  Kama tuhuma hii ni kweli, then serikali ya Magufuli ni serikali haramu na serikali iliyopatikana kwa njia za udhalimu kitu ambacho sio kizuri kwa mustakabali mwema wa taifa letu.

  Kwa mujibu wa katiba yetu, Tume ya Uchaguzi, ikiisha kumtangaza fulani ndie mshindi, kwa tangazo hilo ndio limehitimisha rasmi mchakato wote wa urais.

  Mgombea urais akiishatangazwa kuwa ni mshindi, regardless amepatikanaje, kihalali au kiharamu, by means of hooks or crooks, kwa bao la kisigino, faulo au bao la mkono, as long as yeye ndie ametangazwa mshindi, this is the end that justifies the means!, there is nothing more anyone can do, ukubali usikubali matokeo, uwe ulimchagua, au hukumchagua, umtambue, au usimtambue, its never gonna change a thing!, huyu sasa ndie rais wetu and this is a fact!.

  Kitu kizuri kuhusu haki, haki kamwe huwa haipotei, hata kama sio kwa dunia hii, bali kwa dunia ijayo, na ubaya siku zote huwa haulipi na malipo yote ni hapa hapa duniani, hata kama sio kwako, then kwa kizazi chako!.

  Then namshauri Edward Lowassa, kuwa umetimiza wajibu wako, kutaka kuwatumikia Watanzania!. Umefanya kazi yako, imekamilika!. Sasa nakuomba statement yako hii iwe ndio ya mwisho, usiendelee kulalamika popote, bali sasa nenda zako kajipumzikie kwa amani kwa kuchunga ng'ombe wako kama ulivyoahidi, tena usipeleke malalamiko yako mahali pengine popote zaidi ya kwa aliye JUU, hivyo haya meingine yote muachie Mungu!, YEYE ndiye atakulipia!. kuna mahakama ya haki kuliko mahakama zote za dunia hii, au za ulimwengu huu!, hii ni mahakama ya karma, ndio mahakama pekee ya haki bin haki!.

  Kwa wale wote waliomchagua Lowassa lakini haki zenu zikadhulumiwa, poleni sana!, Mungu atawalipia.

  Na wale wengine wote wanaoshangilia ushindi haramu, ushindi dhalimu, hawa wanashangilia ujinga!, hawa nao pia watakuwa na sehemu ya malipo yao kwenye karma.

  Na kama ni kweli Magufuli ameupata urais wa Tanzania kwa hila, na udhalimu, then tutashuhudia utawala wa mkono wa chuma, the reign of iron hand. Mtashuhudia udikiteta na udhalimu wa ajabu, kuna watu kwa sasa wanashangilia, lakini mwisho wa siku, watakuja kulia na kusaga meno!.

  Kama uchaguzi mkubwa hivi wa rais na wabunge kumeweza kufanyika hila, hii inamaanisha kule ambako wapinzani wameshinda ni maeneo ambako hila zimeshindikana, hivyo kwa uchaguzi wa 2020, wapinzani jiandaeni kuyarejesha majimbo karibu yote na nchi kurejea kwenye mfumo wa chama kimoja.

  Kipimo cha hili kitapimwa kwa chaguzi ndogo zozote zitakazotokea hapa katikati, kwanza upinzani hautaweza tena kushinda uchaguzi wowote, na kama kiti cha ubunge au udiwani kilichokuwa kinashikiliwa na upinzani kitakuwa wazi, uchaguzi wa marudio utakirudisha CCM kwa mbinu zile zile dhalimu by hooks and crooks!.

  Kwa hili hasiri ya Mungu itawaka juu ya Tanzania yetu, tutapata mabalaa na majanga ya ajabu kwa sababu ya hasira ya Mungu, na as taifa tutasuffer ba kuna watu wataangamia!.

  Ila pia, endapo tuhuma hizi ni za uongo, ni za kupika na ni uzushi, then John Pombe Magufuli, ndiye rais chaguo la Mungu kwa Tanzania aliyetangazwa mshindi siku yake ya kuzaliwa!, katika uchaguzi huru na wa haki, hivyo atasimama test in time, of which time will tell!.

  Tanzania itapata neema, mafanikio na maendeleo ya ajabu kwa sababu ya baraka za Mungu zitakuwa juu yake, nchi yetu inakwenda kageuka kuwa ni ile nchi ya ahadi ya maziwa na asali.


  Neno litasimama, mambo mengine yote yatapita, lakini neno litasimama!.

  Mungu ibariki Tanzania.

  Paskali

  Kwa rejea mambo ya karma, karibu mitaa hii
  "The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili
  "Bora Katiba", Tuikubali!, Tusiichukie CCM!, Kwa Sababu
  When Karma comes calling, she stings like a bitch
  Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanaz
  "Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu ya Miujiza Ya Uponyaji kwa
   
 2. n

  nkese JF-Expert Member

  #141
  Feb 23, 2018
  Joined: Mar 8, 2017
  Messages: 1,276
  Likes Received: 987
  Trophy Points: 280
  The reign of terror has downed on Tz!
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #142
  Feb 27, 2018
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,640
  Likes Received: 23,836
  Trophy Points: 280
  Kama hii ni kweli, then serikali yetu ni ...

  P
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...