Elections 2015 Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali Yetu ni Serikali Dhalimu?, Haramu?. Hukumu ya Karma ii Juu Yake!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,464
2,000
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali kuhusu figisu figisu za kwenye uchaguzi mkuu ambapo kila anayeshindwa, hakubali kushindwa kihalali kwenye sanduku la kura katika uchaguzi huru na wa haki, na badala yake huja na tuhuma za kuibiwa kura, kupokwa ushindi halali, na kususia matokeo, hivyo bandiko hili ni swali, Kama Tuhuma Hii ni Kweli, Then, Serikali Yetu ni Serikali Dhalimu?, Haramu? iliyoingia madarakani kwa hila, udhalimu na ulaghai?. Kama ni kweli, then Hukumu ya Karma ii Juu Serikali Yetu!. Na kama sii kweli, then tutashuhudia rais Magufuli na serikali yake, wakibarikiwa, nchi yetu ikibarikiwa na kupata neema na ustawi.


Naomba kuanza na angalizo. Hli ni bandiko swali la dhana tuu ya kufikirika, hypothetical situation kuwa if A is true, then B is true, if it is not true, then its not!. Hivyo kwa euelewa wa mashaka wa wengi wetu humu, msije kushangaa wakashindwa kuiona hicho kitangulizi cha "kama ni kweli", na kupelekea kudhania nimesema serikali yetu ni serikali dhalimu!, ninachosema hapa ni kama hii tuhuma iliyotolewa leo na Edward Lowassa ni kweli, then..

Tuhuma yenyewe imetolewa hapa
Tamko la Edward Lowassa Baada ya NEC Kumtangaza Dr Magufuli Kuwa Mshindi wa Kiti cha Urais - JamiiForumsWatanzania wenzangu!
Leo tarehe 29 October 2015, kwa kupitia Mgombea Mwenza wangu, Mh. Juma Duni Haji nimewasilisha rasmi malalamiko yetu kuhusu mwenendo mzima wa uchaguzi mkuu wa 2015 kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Tumeainisha kwenye malalamiko yetu, kutokuridhishwa kwetu na mwenendo na matukio mbalimbali, hususani, utangazaji wa matokeo batili, yasiyo akisi matokeo halisi yaliyopatikana kwenye vituo vya kupiga kura, kama ifuatavyo.

? Upunguzwaji wa kura zangu
? Kuongeza kura kwa mgombea wa CCM
?Tunaendelea kukataa dhuluma hii dhidi ya matakwa ya wananchi, na jaribio la kutaka kubakwa kwa Demokrasia kunakooneka wazi kutokana na mwenendo wa Tume kuendelea kutangaza matokeo ya kura yasiyo ya kweli kwa kupoka ushindi wetu.

Aidha, kumekuwepo pia na uporaji wa ushindi kwa wagombea wa vyama vya UKAWA kwenye ngazi ya Ubunge na Udiwani

Kama tulivyoeleza jana takwimu zetu sisi zilionesha kwamba nilikua naongoza kwa zaidi ya 67%,na sasa tumejiridhisha kwamba nimepata kura 10,268,795 sawa na asilimia 62% baada ya kukamilisha kazi ya kukusanya fomu za matokeo nchi nzima.

Kwa hali hii, ninaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi initangaze mara moja mimi EDWARD NGOYAI LOWASSA kuwa mshindi wa nafasi ya Urais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania.

Naendelea kuwashukuru wananchi kwa imani yenu kwangu na kunichagua, MImi, pamoja na viongozi wenzangu tunaamini kuwa kuchezea Demokrasia ni kuvunja Amani, lakini sote tunatambua ni nyie watanzania ndio mnaoporwa haki yenu ya kupata mabadiliko, na viongozi mnao wahitaji, hivyo nitaendelea kuwa pamoja na watanzania wote kudai haki yenu kwa nguvu zote.

Tanzania kwa miaka mingi imefahamika kama kisiwa cha amani katika Afrika, tunashangaa leo kuona vyombo vya ulinzi na usalama vikitanda kila mahali wakiwa na silaha za kivita mitaani kana kwamba uchagzui ni vita, hii ni kuwatisha wananchi ili wakubali kunyang?anywa haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanao wataka, nina amini watanzania hatutakubali hali hiyo.

Lowassa, Edward Ngoyai.
29.10.2015

Tamko la Edward Lowassa Baada ya NEC Kumtangaza Dr Magufuli Kuwa Mshindi wa Kiti cha Urais - MPEKUZI
View attachment 303426
Kama tuhuma hii ni kweli, then serikali ya rais Magufuli itakuwa ni serikali haramu na serikali iliyopatikana kwa njia za udhalimu na udanganyifu wa kwenye sanduku la kura, kitu ambacho sio kizuri kwa mustakabali mwema wa taifa letu kwa mujibu wa sheria ya karma.

Kwa mujibu wa katiba yetu, Tume ya Uchaguzi, ikiisha kumtangaza fulani ndie mshindi, kwa tangazo hilo ndio limehitimisha rasmi mchakato wote wa uchaguzi wa urais.

Mgombea urais akiishatangazwa kuwa ni mshindi, regardless amepatikanaje, kihalali au kiharamu, by means of hooks or crooks, kwa bao la kisigino, faulo au bao la mkono, as long as yeye ndie ametangazwa mshindi, this is the end that justifies the means!, there is nothing more anyone can do, ukubali usikubali matokeo, uwe ulimchagua, au hukumchagua, umtambue, au usimtambue, its never gonna change a thing!, huyu sasa ndie rais wetu and this is a fact!.

Kitu kizuri kuhusu haki, haki kamwe huwa haipotei, hata kama sio kwa dunia hii, bali kwa dunia ijayo, na ubaya siku zote huwa haulipi na malipo yote ni hapa hapa duniani, hata kama sio kwako, then kwa kizazi chako!.

Then namshauri Edward Lowassa, kuwa umetimiza wajibu wako, kutaka kuwatumikia Watanzania!. Umefanya kazi yako, imekamilika!. Sasa nakuomba statement yako hii iwe ndio ya mwisho, usiendelee kulalamika popote, bali sasa nenda zako kajipumzikie kwa amani kwa kuchunga ng'ombe wako kama ulivyoahidi, tena usipeleke malalamiko yako mahali pengine popote zaidi ya kwa aliye JUU, hivyo haya meingine yote muachie Mungu!, YEYE ndiye atakulipia!. kuna mahakama ya haki kuliko mahakama zote za dunia hii, au za ulimwengu huu!, hii ni mahakama ya karma, ndio mahakama pekee ya haki bin haki!.

Kwa wale wote waliomchagua Lowassa lakini haki zenu zikadhulumiwa, poleni sana!, Mungu atawalipia.

Na wale wengine wote wanaoshangilia ushindi haramu, ushindi dhalimu, hawa wanashangilia ujinga!, hawa nao pia watakuwa na sehemu ya malipo yao kwenye karma.


Na kama ni kweli Magufuli ameupata urais wa Tanzania kwa hila, na udhalimu, then tutashuhudia utawala wa mkono wa chuma, the reign of terror and iron hand. Mtashuhudia udikiteta na udhalimu wa ajabu, kuna watu kwa sasa wanashangilia, lakini mwisho wa siku, watakuja kulia na kusaga meno!.

Kama uchaguzi mkubwa hivi wa rais na wabunge kumeweza kufanyika hila, hii inamaanisha kule ambako wapinzani wameshinda ni maeneo ambako hila zimeshindikana, hivyo kwa uchaguzi wa 2020, wapinzani jiandaeni kuyarejesha majimbo karibu yote na nchi kurejea kwenye mfumo wa chama kimoja.

Kipimo cha hili kitapimwa kwa chaguzi ndogo zozote zitakazotokea hapa katikati, kwanza upinzani hautaweza tena kushinda uchaguzi wowote, na kama kiti cha ubunge au udiwani kilichokuwa kinashikiliwa na upinzani kitakuwa wazi, uchaguzi wa marudio utakirudisha CCM kwa mbinu zile zile dhalimu by hooks and crooks!.

Kama tuhuma hizi za Edward Lowassa ni kweli kuwa ushindi wa Magufuli umetokana na hila na dhulma katika uchaguzi mkuu, then hasira ya Mungu itatuwakia juu ya Tanzania yetu, tutapata mabalaa na majanga ya ajabu ajabu kwa sababu ya hasira ya Mungu, na sisi wote kama taifa, we will all suffer!, tutasuffer sana na kuna watu hadi wataangamia!.
Ila pia, endapo tuhuma hizi ni za uongo, ni za kupika na ni uzushi, then rais John Pombe Joseph Magufuli, ndiye rais chaguo la Mungu kwa Tanzania aliyetangazwa mshindi siku yake ya kuzaliwa!, katika uchaguzi huru na wa haki, hivyo atasimama test in time, of which time will tell!.

Kupitia kwa Magufuli, Tanzania itapata neema, mafanikio na maendeleo makubwa ya ajabu kwa sababu ya baraka za Mungu zitakuwa juu yake, nchi yetu inakwenda kageuka kuwa ni ile nchi ya ahadi ya maziwa na asali.


Neno litasimama, mambo mengine yote yatapita, lakini neno litasimama!.

Mungu ibariki Tanzania.

Paskali

Kwa rejea mambo ya karma, karibu mitaa hii
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili
"Bora Katiba", Tuikubali!, Tusiichukie CCM!, Kwa Sababu
When Karma comes calling, she stings like a bitch
Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanaz
"Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu ya Miujiza Ya Uponyaji kwa
 

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
3,079
2,000
So sad wametutukana malofa, kura wametuibia wazi wazi, mabomu wametupiga, sehemu nyingine ubunge wamechukua kwa nguvu, zanzibar wamedhulumu kwa nguvu na ushindi wamechukua kibabe. Waliofanya haya hukumu yao ni ya kifo.

Ee baba Mungu uwalipe ujira wao bila kuwapunja. Amen
 

Kiboko.

JF-Expert Member
Jul 31, 2013
2,833
2,000
wewe hukuwah mpenda Magufuli, ulivuka mipaka na kujiita Nabii kuwa Rais ajaye n Eddo, wananch tumemkata na amekaaaa, swal rahis hiv Eddo apate kura zote hzo toka wapi?mikoa ipi labdba? mbona hana wabunge kabsaa? angekubalika kwa kiasi hko tungewaona wabunge 100+ toka Ukawa.......


wachaw wa Edo

Chadema kwa kumchafua miaka 7 iliyopta
Gwajima a.k.a mshenga kuwa msemaj wake kampotezea kura nying za waslam
safu yake ya kampein Mbatia, Sumaye< mbowe na Mrema hawa n watu wa jamii moja, pale wanaposimamia issue ya kitaifa na kuonekana n sura zile zile hutilia shaka hata jamii nyingne kujilinda, na hiki ndicho wana lake zone na mikoa mingne walchokifanya.... Eddo kapigwa na wanzania wote kasoro wapemba
 

jebibay

JF-Expert Member
Nov 3, 2012
1,413
1,225
Amen !

So sad wametutukana malofa, kura wametuibia wazi wazi, mabomu wametupiga, sehemu nyingine ubunge wamechukua kwa nguvu, zanzibar wamedhulumu kwa nguvu na ushindi wamechukua kibabe. Waliofanya haya hukumu yao ni ya kifo.

Ee baba Mungu uwalipe ujira wao bila kuwapunja. Amen
 

Kiboko.

JF-Expert Member
Jul 31, 2013
2,833
2,000
anatangazwa mshind siku hyo hyo anaadhimisha siku yake ya Kuzaliwa hajaona tu kuw huyu ndiye chaguo la Mungu
 

Kansigo

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
2,664
2,000
Pasco hivi mwenzako Ocampor four na Mussa Allan vp wanaendeleaje! nasikia wame commit criminal offense! ndo maana Mzee Ruksa aliwashauri msipende kuvuka mipaka haya ndo madhara yake! eti mahaba nyambafff
 

PRINCE CROWN

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
4,902
2,000
Mkuu Inauma Sana, Amwachietu MUNGU Atamlipia Kwa Wote Walio Usika Kuipotoa Haki Ya Walio Wengi, Malipo Ni Hapa Hapa, Haki Ya Mtu Haipotei. Ikiwa MUNGU Amemridhia Kuwa RAIS Itakuwatu.
 

Jay One

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
13,967
2,000
Mm nimeshaanza KUFUNGA KWA MAOMBI....!!! Kama ni ushindi wa haki, MUNGU hatatoa ADHABU...!!!

Kama ni USHINDI wa DHULUMA, MUNGU ataangamiza watu, hadi wakome...!!! Narudia, Mungu ataangamiza wahusika hadi wakome...!!!

In Jesus name...!!!
 

PRINCE CROWN

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
4,902
2,000
Wewe kijana ni mpumbavu na lofa kabisa. Yaani ni loofaaa. Rais wako ni Dr Magufuli!
Binti, Tumia Basi Maneno Yenye Utu Kwa Ndugu Zako, Sote Ni Watanzania Hatuna Budi Kueshimiana Ndiyo Utamaduni Ulio Wakitanzania Mkuu Wangu, Kila Mtu Anao UHURU Wa Kutoa Maoni Yake Bila Kuvunja Sharia Na Kueshimu Utu Wa Wengine Uo Ndio Ustaarabu Ndugu.
 

shafii83

Member
Sep 21, 2015
29
0
angekubalika na wananchi si tungeona majimboni angepata kura za kutosha ivi jaman kwa lile gape alilopigwa loaswa kwa mtu mwenye akili as great thinker unaweza kuisini kweli CCM imechota au tunafosi ushindani?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom