Kama hamkubali mtoto wako Acha tu haitabadilisha kitu.

miss chagga

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
57,821
48,976
Habari zenu

Leo nimekutana na jambo hospital ikanibidi tukumbushane wakuu.. mama alikuwa anambadili diaper mtoto wake me nipo karibu mtoto kanangozi kama ya mamba huku akianimbia kwa madaha yani mwanangu kila diaper inamkataa. Nikamwangalia nikapata hasira nikamwambia si lazima kuvaa hizo disposable diaper... nikaona na huku niwakumbushe tu...

Kwanza tukubaliane tunatesa watoto kisa ubussy wa kutafuta pesa na pia vipesa vyetu tukivipata ndiyo hatari zaidi...

Adhabu ambayo tayari na naona inatosha Kumwacha mtoto na dada wa kazI na kutuona wazazi weekend tu. Huku hatujui wanaishi vipi ila tunamwachia Mungu hili..

Kingine kumvalisha mtoto diaper hasa hizi za kutupa 24/7 mtoto kafungwasha mzigo huko hasa maeneo ya joto ni mateso sana kwa watoto embu imagine tukiwa mp tu kero yake .. lakini sijui tunahisi mtoto anakuwa tofauti? May be.

Haya madaiper yanaletea watoto UTI, michubuko vipele lakini tumekomaa tu na kubadilisha brand... tuache kufanyia watoto majaribio.

Kama mtoto yupo nyumbani mnunulie vikaptula vya pamba vya kutosha abadilishwe kila anapojisaidia na asubuhi kabla ya kwenda kazini fua anika ondoka akiwa analala avalishwe nepi au hiyo diaper sasa..
Kama ni lazima mtoto avae diaper basi usiwe mkali dada anapombadili mtoto mara kwa mara unakuta una mbajetia dada atumie tatu may be kwa siku na akitumia zaid unamind as if kavaa yeye. Mwisho wa siku tunaumiza mtoto kwa kuachwa na uchafu muda mrefu ili boss aridhishwe jamani embu tubadilike.

Wenzetu wanaangalia ubora kuliko wingi .. ila sisi tunaangalia wingi kuliko ubora .. nyingi zinazokuja kwetu hazipo katika ubora huo tunaofikiria...

SI LAZIMA KUMVALISHA MTOTO HIZO DISPOSABLE DIAPER HATA KAMA UNAINGIZA MILIONI ISHIRINI KWA SIKU KAMA HAI MKUBALI MWANAO ACHA MAVALISHE NEPI FUA HUTABADILIKA NA KUWA MASKINI.. .

Siku njema msalimie mwanao..
 
Kusema ukweli haya ma disposable mimi ninayatumia nikiwa safarini tu lakini home ninapenda nappy za taulo zile za kufunga na pini. Tena ninakinga maji ya mvua kufulia hata jua lisipotoka ukiweka baraza ya nyuma upepo unakausha
 
Sorry miss chagga unamtoto au umeolewa.....??? kama bado naomba tutafutane kwamaana nimesoma nyuzi zako nyingi sana JF unaoneka uko vzr kuwa mke ila kama una mtu kwenye mahusiano usinitafute kwani uwa sitaki kivunja au kuharibu mahusiano ya watu.
 
Umesema ukweli kabisa Miss, uvivu wetu unawaumiza watoto muda mwingine si kwamba tuna kazi nyingi ila unakuta mzazi anaogopa kinyesi cha mwanae na kukionea kinyaa hivyo huisi pampasi ni mkombozi wao! Wanawake wa kileo acheni ubishoo tutimize wajibu kama tulivyotimiziwa na wazazi wetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sorry miss chagga unamtoto au umeolewa.....??? kama bado naomba tutafutane kwamaana nimesoma nyuzi zako nyingi sana JF unaoneka uko vzr kuwa mke ila kama una mtu kwenye mahusiano usinitafute kwani uwa sitaki kivunja au kuharibu mahusiano ya watu.
Mkuu nimekuelewa
 
Umesema ukweli kabisa Miss, uvivu wetu unawaumiza watoto muda mwingine si kwamba tuna kazi nyingi ila unakuta mzazi anaogopa kinyesi cha mwanae na kukionea kimyaa hivyo huisi pampasi ni mkombozi wao! Wanawake wa kileo acheni ubishoo tutimize wajibu kama tulivyotimiziwa na wazazi wetu

Sent using Jamii Forums mobile app
Inasikitisha watoto hawashi kuumwa umwa tutaadhibiwa kwa hili kwa kweli
 
zipo chupi za mkojo fulani hivi wengi wanapenda kuziita pumpers za kufua nzuri sana mimi nilimnunulia zile ishirini mtoto alivaa diaper usiku tu alafu hata kufua nepi sio kazi kama kweli ulijiandaa kuwa mzazi kwanza hakuna raha kama kulea mwanao,mimi mpaka leo na ubaba wangu nafua nguo za watoto nikiwa na time kipindi cha uchanga wao nimefua sana nepi kiroho safi tu..Nacho zungumza hapa niukweli wala simajivuno au story za furahisha genge
 
Back
Top Bottom