Kama hali ndio hii Simiyu, kazi ni ngumu kwa Magufuli

ngurasu aba

Senior Member
Jul 12, 2015
105
29
Nipo Bariadi wilaya kubwa ya mkoa huu wa Simiyu, nilitegemea kuona watu wa huku wakimuunga mkono Magufuli kutokana na kwamba ni wa kanda yao lakini isivyo tegemewa ni kwamba huku vijana weng wanaonekana kuunga mkono M4C na hawataki kusikia CCM, labda kwa kiasi kidogo wazee weng bado wameikumbatia CCM wakidai imewakuza, hii hali itampa mtihan mzito sana mgombea urais kupitia CCM mh. Magufuli kuubadili upepo wa kisiasa katika kanda yake kwani huku Lowassa na dr. Slaa wanaonekana kukubalika sana na vijana wengi katika wilaya hii ya Bariadi.
 
Magufuli hana mvuto! Hata kiingereza hajui. Sijui huko UN atatumia lugha gani kutuwakilisha maana huko hakuna Kiswahili.
 
Ccm walishajifia hakuna wanapokubalika hata hapa nyumbani kwangu hakuna inzi wa kijani wote nimewaua tangu mwaka 2010
 
lowasaa mwambab wa kaskazini na slaa jabali la kaskazini Tz imara slaa ingineer na lowassa master planer
 
Magufuli hana mvuto! Hata kiingereza hajui. Sijui huko UN atatumia lugha gani kutuwakilisha maana huko hakuna Kiswahili.
Mkuu huko hata kimasai unaweza kuongea. Kwanza nani kakuambia kwamba John Joseph Pombe Magufuli (PhD) hajui kiingereza?
 
Nipo bariadi wilaya kubwa ya mkoa huu wa simiyu, nilitegemea kuona watu wa huku wakimuunga mkono magufuli kutokana na kwamba ni wa kanda yao lakini isivyo tegemewa ni kwamba huku vijana weng wanaonekana kuunga mkono M4C na hawataki kusikia ccm, labda kwa kiasi kidogo wazee weng bado wameikumbatia ccm wakidai imewakuza, hii hali itampa mtihan mzito sana mgombea urais kupitia ccm ndg. mh. Magufuli kuubadiri upepo wa kisiasa katika kanda yake kwani huku lowasa na dr. Slaa wanaonekana kukubalika sana na vijana wengi katika wilaya hii ya bariadi.
Mkuu umejikita kwenye siasa za ukanda?
 
Magufuli hana mvuto! Hata kiingereza hajui. Sijui huko UN atatumia lugha gani kutuwakilisha maana huko hakuna Kiswahili.

Bora hata magufuri anajua kuongea lowasa anaongea kama mtoto anaejifunza kuongea! Hata mbowe arikili kwamba lowasa bubu
 
Nipo bariadi wilaya kubwa ya mkoa huu wa simiyu, nilitegemea kuona watu wa huku wakimuunga mkono magufuli kutokana na kwamba ni wa kanda yao lakini isivyo tegemewa ni kwamba huku vijana weng wanaonekana kuunga mkono M4C na hawataki kusikia ccm, labda kwa kiasi kidogo wazee weng bado wameikumbatia ccm wakidai imewakuza, hii hali itampa mtihan mzito sana mgombea urais kupitia ccm ndg. mh. Magufuli kuubadiri upepo wa kisiasa katika kanda yake kwani huku lowasa na dr. Slaa wanaonekana kukubalika sana na vijana wengi katika wilaya hii ya bariadi.

Kwanza m4c ifute saivi ni safari ya matumaini maana chama saivi kipo chini ya lowasa
 
Unajua nini kuhusu Ikungu wewe?

Mi ndo meya wa mji.

Hakuna Ikungu bila mimi.

hivi pale mji wa ikungu uko wapi?zamani nikipita naona nyumba moja kuleeee,nyingine kuleeee,hapakuwa hata viduka.au kulikuja pakajengeka pale?
 
Acheni kujipa moyo Wa kipuuzi,subirin mwenyewe mtaona jinsi huyo fisadi wenu aliye mroho Wa madaraka atakavyopigwa gap
 
Magufuli hana mvuto! Hata kiingereza hajui. Sijui huko UN atatumia lugha gani kutuwakilisha maana huko hakuna Kiswahili.
Hoja ya kitoto kabisa. Unafikiri Putin, Shinzo Abe, Angela Merkel, Xi Jinping, Hollande na wengineo wakienda UN wanatumia Kiingereza?

Kung'ang'ania kutumia Lugha za mabwana ni tabia ya watwana ambao bado hawajajitawala kisaikolojia. Magufuli/Lowassa/Slaa ataweka historia na atakuwa shujaa wa Afrika kama akienda UN na kutumia Kiswahili. Na vijana wetu watapata ajira nzuri sana za kuwa watafsiri katika kiwango cha kimataifa!
 
Back
Top Bottom