Kama haki itatendeka ndani ya CC ya CCM, Dkt Salim A Salim ndie Rais bora ajaye

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Wasalaam wanajukwaa!

Nadhani kila mtu anamjua huyu mwanamapinduzi,mwanadiplomasia aliyebobea wa siasa za kitaifa na kimataifa,Waziri mkuu mstaafu, katibu mkuu mstaafu wa Umoja wa Africa(AU),Mtumishi wa umma wa miaka mingi asiyekua na doa katika uongozi wake!

Huyu ni kiongozi aliyewahi kutia nia kugombea urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania miaka ya nyuma ndani ya CCM lakini rafu za kimakundi zikamchezea!

Ni mtu mwenye maono na anayekubalika kila kona ya dunia, Hakika hii ndio dhahabu ambayo CCM hakitakiwi kucheza nayo, Kama kweli inavyosemekana kua atachukua form ya kuwania urais naye wiki ijayo basi ndiye atakayemaliza kazi maana mpaka hapa kwa waliotia nia wote hakuna wa kufanana naye!

Ni mtu ambaye kwakweli kama atapitishwa ndiye atakayewapa wakati mgumu sana upinzani nchini.

Huyu mzee ni Turufu ya Taifa.
 
Akichukuwa fomu ya kuwania urais nina uhakika atatusumbuwa sana UKAWA.lakini nasikia alishasema hataki tena urais.labda ccm wamfate wakamuombe msamaha si unakumbuka matusi na kashfa walizompa huyu jamaa mwaka 2005 mkuu?
 
Kwa mazingira ya siasa za sasa ambapo waislam wamekuwa wakiandamwa na maadui wa taifs hili hasa wale wanaoona kuwa wenye dini yao tu ndo wanastahili kuongoza, sioni nafasi ya Salim kwenye mfumo huu dhalimu. Pia kuna kautamaduni ka kubalilishana baina ya Waislam na Wakristo katika nafasi ya Urais. Ni utamaduni mzuri japo una kasoro zake
 
Akichukuwa fomu ya kuwania urais nina uhakika atatusumbuwa sana UKAWA.lakini nasikia alishasema hataki tena urais.labda ccm wamfate wakamuombe msamaha si unakumbuka matusi na kashfa walizompa huyu jamaa mwaka 2015 mkuu?
CCM hata wakisimamisha bata anaweza kushinda tu mbele ya mgombea wa UKAWA. Hawana lolote.
 
Sidhani kama CCM watampitisha.

SAS ni muumini wa serikali 3 kumbuka pia timu Kikwete ndiyo iliyomchafua kuwa yeye ni mwarabu.
 
huyu mzee yuko vizuri tatizo amenyamazia maovu yakitendeka..... ccm imechakachua maoni ya wananchi lakini yeye yuko kimya tu...
 
Mbona tuliambiwa ni herz bollah 2005 sasa huo uraia wa Tz kaupata lini tena?
 
CCM hata wakisimamisha bata anaweza kushinda tu mbele ya mgombea wa UKAWA. Hawana lolote.

inawezekana uko sahihi maana mtaji wa ccm ni ujinga. maana nasikia kule maeneo ya kibakwe,kongwa na maeneo mengine ya dodoma bado wanaamini nyerere ndo rais wa tanzania...
 
Naunga mkono hoja, mtoa mada amefikiria sana japo hakuna mkamilifu ila mwenyezi mungu pekee lakini kwa viongozi wetu wa taifa hili kuanzia upinzani hadi ccm Salim anafaa.
 
MAHANJU

Sorry, He would have been in 2005. He would have done a better job. He is not what he was in 2005 and furthermore, I doubt his resolve to root out mega corruption and deal with the whales and sharks. Tunahitaji mfumo mzima uwe overhauled ili kujenga institutions. Sioni kwenye CCM atakayeanza kwa kuifuta katiba pendekezwa ambayo ndiyo chanzo cha matatizo.
 
Last edited by a moderator:
Haki gani unaongelea? Mgombea si atapatikana kwa kura au kuna mengineyo?
 
Ulivyo mjinga unawafananisha wagombea wa CCM na bata!
Ni ujinga wako tu ndio unaokufanya usione hoja yangu. Hoja ni kwamba Upinzani wa Tanzania hauna nafasi yamkushinda nafasi ya urais hata kama CCM wasiposimamisha mtu. Kwa waliokuwa wanachagua enzi za chama kimoja wamenielewa nini nimemaanisha
 
Kwa mazingira ya siasa za sasa ambapo waislam wamekuwa wakiandamwa na maadui wa taifs hili hasa wale wanaoona kuwa wenye dini yao tu ndo wanastahili kuongoza, sioni nafasi ya Salim kwenye mfumo huu dhalimu. Pia kuna kautamaduni ka kubalilishana baina ya Waislam na Wakristo katika nafasi ya Urais. Ni utamaduni mzuri japo una kasoro zake

Hii ni zamu yetu make msitake
 
Kama ni mie nabaki na heshima yangu kama Mzee Augustino tu, haiwezekani watu wale wale wakukatae 1995 na 2005 kwa mbwembwe na vijembe kibao alafu eti leo waonekane wanakupenda. Uho ni unafikina uzandiki mkubwa, namshauri huyu Mzee aendelee na mambo yake kwasababu kukataa hatakuwa wa kwanza ukizingatia akina Warioba nao wamechomoa.
 
Hatutaki rais wa kimataifa...tunataka rais atakayetoa kipaumbele kushugulikia matatizo ya ndani kikamilifu....na hapo sioni mtu mwingine anayeweza kupigana na fraud, money laundering, corruption & racketeering nje ya JP Magufuli
 
Back
Top Bottom