geraldkowero1
JF-Expert Member
- Jul 5, 2014
- 1,838
- 644
Sio kwamba haya yote alikua hayaoni mkuu! Tatizo hapa lilikua ni mfumo mbovu wa uongozi! Walimbana sana na kumwita nwarabu, ndio maana hata kwenye ujumbe wa kamati kuu hakupewa nafasi ndio juzi tu hapa wakaona aibu wakamwingiza, Anayajua madhaifu yote ya kimfumo ndio maana anaitaka nafasi ya urais anyooshe mambo.
Nakubaliana na wewe ila hawezi kuyanyoosha akiwa ccm, hata yeye mwenyewe hilo analielewa. Ninavyoamini ingawa sina ushahidi wa kuthibisha imani yangu ni kuwa hawawezi kumpitisha huku wakielewa anaweza kuwarudi wote waliomchafua. Hilo lipo pia kwa lowasa ingawa wanaweza wakasema kuwa nae ana kashfa ya richmond. Hata hivyo yeye alishasema hakuna alichokifanya ambacho hakikueleweka kwa mkuu wake.Tatizo hajajitetea kwa wananchi wakalielewa vizuri tofauti na kutamka tu na kudai mbele ya waandishi ataeleze. Lini? Naamini pia hao wakubwa ili wakukabidhi kijiti lazima muwe na makubaliano nao kuwa sio wao na familia zao tu bali hata marafiki zao hutawagusa. Pia lazima wawe na sauti kwenye serikali utakayoiunda na si ajabu wakakupa na orodha ya watwule wao. Ukikaidi wanaangalia kwenye orodha na kumpa dhaifu yeyote. Hata hivyo kwa yaliyomkuta mteule wako 2005 na kwenye bunge la katiba sidhani kama atawaamini tena labda kama una taarifa kuwa alishaombwa radhi.Kwa nini usiunganishe nguvu kwa pendekezo langu?