Juma Wage
Senior Member
- Sep 8, 2023
- 132
- 279
Katika dunia ya hoja na mantiki, ni kweli kwamba ujumbe ni muhimu kuliko mjumbe. Lakini je, kila mjumbe anastahili jukwaa? Mbona si kila njiwa huleta barua njema; wapo wanaoruka wakiwa wamebeba hadaa na uzushi.
Gwajima ni baba wa ahadi zilizoharibika kabla ya kuzaliwa. Aliwahadaa wananchi wa Kawe kwa ndoto za Birmingham, akawakatia tiketi za meli kutoka Japan ambazo hazikuwahi kutia nanga.
Leo hii anajivika joho la mtetezi wa haki za binadamu? Ni sawa na fisi kujitambulisha kama mchungaji wa kondoo.
Huyu ni yuleyule aliyewahi kudai anaweza kuwafufua Chifupa na Sokoine, kauli iliyovuka mpaka wa hekima na kuingia kwenye ukumbi wa miujiza ya kisiasa isiyo na staha.
Anapotamka sasa kuhusu utekaji na mauaji, haionekani kama sauti ya ujasiri, bali ni sauti ya mtu aliyekata tamaa ya kisiasa akililia jukwaa kwa maneno makali na maigizo.
Hoja yake inaweza kuwa na uzito, lakini ikitolewa na mtu aliyebobea katika uongo, maigizo na usanii wa mimbari, inageuka kuwa mzaha mchafu.
Kwa mtazamo wa wengi, si haki anayoitafuta bali ni umaarufu anaoutafuta kwa hila.