Mokaze
JF-Expert Member
- Aug 3, 2018
- 14,370
- 14,913
Ha ha ha ha ha! Swali zuri lakini lazima nikiri linachekesha. Kwa mtazamo ulio nao, ingekuwa wakati mtu akiruka akianguka chini anakuta pale aliporukia pameshapita saa nyingi! Ingekuwa nikitaka kwenda Kigoma toka Dar, basi naruka juu umbali fulani, nikianguka chini najikuta nimeangukia Kigoma Dar ilishapita saa nyingi!
Zile story za ukiruka ndani ya lori utaangukia chini si kweli, japo nasikia watu wakisema kuna Mmasai aliruka ndani ya lori linalokimbia akaachwa! Huwezi kuachwa kwa kuwa unaporuka unakuwa uko kwenye spidi ya lori tayari. Ingekuwa unaachwa basi ingekuwa ukiwa kwenye ndege ukarusha shilingi ingeangukia nyuma kabisa ya ndege!
Lakini kitu cha kukumbuka ni kwamba dunia inazunguka jua katika obiti yake ile ile, ya mduara na wakati na yenyewe inazunguka katika mhimili wake. Na kinachosababisha usiku na mchana sio kitendo cha dunia kuzunguka jua, bali ni dunia kuzunguka kwenye mhimili wake yenyewe wakati inalizunguka jua. Kuizunguka jua kunasababisha mabadiliko ya majira, masika, kiangazi nk.
Sasa dunia haiziachi satelite kwa kuwa satelite na zenyewe zinakimbia, haziko stationery. Ukiona unaiona satelite kila siku iko pale pale ni kwamba inazunguka kwa spidi ile ile ya dunia. Ni sawa na gari mbili zilizo sambamba zikiwa spidi moja utaona kama gari ya pili haiendi iko pale pale kwa kuwa zinaenda spidi sawa. Ili satelite isihame na kwenda mbali na dunia izunguke dunia kuna hesabu zinapigwa ili kujua ikimbie kwa spidi gani ili kubaki kwenye mvutano kati yake na dunia. Spidi hiyo hutegemea uzito wa satelite na umbali kutoka uso wa dunia.
Ili kujua satelite ikimbie kwa spidi gani ili kuendelea kuzunguka dunia tunatumia hii forula
v = (GM/R)1/2
ambapo G = nguvu ya gravity (9.8m/s2)
R = umbali toka katikati ya dunia na satelite
M = uzito wa satelite
Labda tofauti moja ni kwamba kuna satelite ambazo kutokana na sehemu zilipo, kadiri dunia inavyozunguka jua na kuzunguka katika mhimili wake inafanya wakati fulani direct line ya satelite toka duniani iwe sehemu mbalimbali za dunia kulingana na dunia inavyozunguka, hasa zile zilicho chini chini karibu na dunia, kwenye kinachoitwa Low Earth Orbit. Ndio maana kwa mfano, unaweza kuwa na satelite ambayo ni saa sita hadi saa saba mchana tu inakuwa katika direct line na Dar es Salaam, na hivyo inaweza kukupigia picha za Dar wakati huo.
Nadhani umeelewa. Tupo Mzee, hata kama Magufuli hatutambui!
Mkuu umefafanua vizuri, shukrani, lakini samahani jaribu kucheki katika hiyo formular (kikokoto).
G=universal gravitational constant 6.67×10^-11 m^3kg^-1s^-2, na wala siyo g=9.81m/s^2.
Ukitaka kutumia g hiyo formular itakuwa:-
V=√[g/(1+h/re)]
Ambapo h ni umbali kutoka uso wa dunia hadi kwenye satellite na re ni nusu kipenyo cha dunia.
Juu ya yote formular yako ni safi mkuu.