Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 738
- 478
MKATAA WENGI MCHAWI
Na Dk Juma Mohammed
Zumari likipulizwa Visiwani, wahemkwao wa Maziwa Makuu.
Naam, katika viunga vya Umoja wa Mataifa katika Jiji la New York, Marekani , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amehutubia kwa mara ya kwanza Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Hii ni hotuba ya kwanza na ya kihistoria kwa Rais Samia kuhutubia katika chombo cha Kimataifa.
Huu ni uthibitisho wa kukubalika kwake katika Umoja huo wa Ulimwengu lakini pia Rais Samia amekuja na bahati ya kipekee katika uongozi wake, nchi yetu imechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Nini tafsiri ya jambo hili katika uwanja wa kimataifa?
Ni kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendeshwa kwa kufuata na kutekeleza misingi ya kidemokrasia na utawala bora.
Nchi yenye mashaka mashaka na demokrasia yake, yenye mazonge juu ya utawala bora kamwe haiwezi kuwa sehemu ya kuongoza chombo cha juu katika muundo wa Umoja wa Mataifa.
Tuna kila sababu Watanzania kutembea kifua mbele na kwamba viongozi wetu hawakukosea waliompendekeza Rais Samia kuwa Mgombea Mwenza na hatimaye leo anatuongoza katika misingi ya kiungwana, kistaarabu, mwenye kujali utu, huruma kwa raia wake, mpenda haki na mwenye kuipenda kwa dhati Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kama bado kuna mtu mwenye mashaka na Rais Samia, hotuba aliyoitoa leo ndio jibu lake.
Rais Samia hakuwa na kipapume, ametulia ameueleza Ulimwengu msimamo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika maeneo muhimu kabisa bila kuacha hata chembe ya shaka.
Ni katika mkutano huu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Viongozi hao wanapitsha kile kinachoitwa New World Order ingawaje sio lazima kupitia hadhira hiyo,lakini kawaida inatendeka hivyo.
Rais Samia kupitia hotuba yake katika mkutano wa mwaka huu wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, wengi wamefahamu Samia Doctrine ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatimiza wajibu wake katika uwanja wa kimataifa ijapokuwa sio Super power,lakini mbele ya macho ya dunia tunasauti na tunaposema tunasikilizwa.
Ule msemo wa kale kwamba Mkataa wengi mchawi, Rais Samia ameiambia Dunia umuhimu wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuishirikiana katika Nyanja mbalimbali.
Ukisoma kisa cha Nyuki utaiona mantiki ya uzito wa hoja ya Rais Samia kuhusu dhana ya kushirikiana na wenzio katika mambo.
Kitendo cha Rais Samia kushiriki vikao mbalimbali nje ya Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na hotuba yake ya leo ni wazi kuwa ameinusuru Diplomasia yetu pakubwa maana ilikuwa tunasemea katika vibuyu.
Akiwa katika Viunga vya Umoja wa Mataifa, Rais Samia amezungumza na Wakuu mbalimbali wa Mashirika ya Kimataifa.
Wamempokea vizuri na hivi ndivyo hali ya mambo inavyotakiwa katika maisha yetu wanadamu, aso hiki ana kile hakuna mtimilifu kila mmoja anamuhitajia mwenziwe.
Huko Marekani Rais Samia hakwenda peke yake kama mchawi, wafanyabiashara wetu wazalendo wametangulia kwa gharama zao na amewakutanisha na wafanyabiashara wenziwao wa huko na mengi yenye faida yatapatikana katika kukwamuka kiuchumi nasi maisha yetu yazidi kutononoka vijana wasikimbilie Ughaibuni kutafuta maisha mazuri.
Mwanafalsafa maarufu wa kale katika Taifa la China,Confucius mojawapo ya mafundisho yake kwa mwanafunzi wake, Tzu Kung, alimfunza juu ya uhusiano kati ya utajiri na umasikini.
Mwanafalsafa huyo alimwambia ukimwona mtu tajiri , basi tamani kuwa kama yeye, lakini, ukimwona aliye masikini, basi, jitafakari wewe mwenyewe .
Rais Samia anatamani nasi Watanzania tuwe matajiri na ndio maana kila uchao amekuwa akifanya kila awezalo kuhakikisha tunatoka hapa tulipo na kufika kama walivyo wenzetu walioendelea kiuchumi kwa kuwa na uchumi mkubwa na endelevu.
Moja katika jambo ambalo linakoleza ukuaji wa uchumi imara ni miradi ya uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje (Foreign Direct Investment-FDI).
Juhudi zinaochukuliwa na Rais Samia ni za kupigiwa mfano katika kukuza uchumi ili tufikie uchumi uliotononoka zaidi katika kuvutia Wawekezaji wenye tija kutoka nje kama uwekezaji wa makampuni makubwa ya nje.
Kama inavyoeleweka Uwekezaji wa makampuni ya nje ni muhimu katika uchumi wa nchi na hususan uchumi wa kileo chini ya biashara huru. Uwekezaji huo unachangia ukuaji wa uchumi wa nchi husika.
Nchi za Dunia ya tatu kama Tanzania zinatilia mkazo katika uwekezaji huo wa FDI,pamoja na biashara ya kimataifa ambazo ni chanzo muhimu cha Maendeleo.
Katika nadharia ya Uhusiano wa Kimataifa, FDI na biashara ya Kimataifa zinapewa uzito mkubwa katika ukuzaji wa uchumi wa nchi zinazoendelea,mchango katika maendeleo ya rasilimali watu, kubadilishana teknolojia ndio msingi wa uchumi wa kileo.
Tanzania hivi sasa ipo pazuri kwenye biashara ya Kimataifa.
Huko Marekani Tumemuona Rais Samia namna anavyochaakazi kwa kufanya vikao na Makampuni makubwa, hii yote ni sehemu ya kuitangaza Tanzania kuvutia Wawekezaji , huwezi kupata Wawekezaji wa maana kwa kufanya ziara za Sikonge au Tandahimba, lazima utoke kimataifa.
FDI ina aina mbili za uwekezaji ambao ni ile ya Fixed asset na Portfolia investment ambazo zote hizo zinachangia ukuzaji uchumi wa nchi inayowekezwa, tembelea katika mradi wa Symbion Power Plant na miradi mengine hapa nchini utathibitisha hili.
Ni jambo lisiloweze kubishaniwa kwamba Tanzania kwa hivi sasa inategemea misingi ya mfumo thabiti na imara wa shughuli za uwekezaji mkubwa kutoka nje na hatua za kuwa na uchumi huru, hali ambayo itastawisha biashara huru ya bidhaa na huduma ikiwemo huduma za bandari.
Faida nyengine ya FDI ni kubadilishana teknolojia, utaalam na pia kuongezeka kwa fedha za kigeni katika nchi.
Mfano bora wa nchi zilizopata mafanikio kwa FDI ni Singapore, Korea Kusini,Hong Kong naTaiwan kwa kuwa na sera nzuri za Uwekezaji-FDI leo nchi hizo zinaitwa Asia Tigers au four dragons.
Kwa mfano, Bandari ya Hong Kong ni miongoni mwa bandari zenye kusafirisha bidhaa nyingi zaidi duniani ikifuatiwa na Singapore.
Tunatagemea pia bandari ya Dar es Salaam nayo iwe kama bandari ya Hong Kong.
Hong Kong pia ni ya mwanzo duniani iliyosheheni Uwekezaji wa moja kwa moja (FDI) huku Taiwan ikiongoza katika dunia kuwa learder in micro-electronic research and development hakuna sababu ya kwanini Jamhuri ya Muungano wa Tanzania isiwe leader in micro-electronic research and development ya Afrika.
Wakati ndio huu, lazima tufunge mkanda na kujituma katika kutekeleza yale tuliyoyapanga.
Tunawajibu wa kuwajibika kwa mwende wa haraka maana hivi sasa mwendokasi wa uchumi wa dunia na ukuaji wa teknolojia haitusubiri na wala hawana nafasi ya kutungoja
MWISHO