Kama bado kuna mtu mwenye mashaka na Rais Samia, hotuba aliyoitoa leo ndio jibu lake

Ojuolegbha

Member
Sep 6, 2020
22
75
MKATAA WENGI MCHAWI

Na Dk Juma Mohammed

Zumari likipulizwa Visiwani, wahemkwao wa Maziwa Makuu.

Naam, katika viunga vya Umoja wa Mataifa katika Jiji la New York, Marekani , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amehutubia kwa mara ya kwanza Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Hii ni hotuba ya kwanza na ya kihistoria kwa Rais Samia kuhutubia katika chombo cha Kimataifa.

Huu ni uthibitisho wa kukubalika kwake katika Umoja huo wa Ulimwengu lakini pia Rais Samia amekuja na bahati ya kipekee katika uongozi wake, nchi yetu imechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Nini tafsiri ya jambo hili katika uwanja wa kimataifa?

Ni kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendeshwa kwa kufuata na kutekeleza misingi ya kidemokrasia na utawala bora.

Nchi yenye mashaka mashaka na demokrasia yake, yenye mazonge juu ya utawala bora kamwe haiwezi kuwa sehemu ya kuongoza chombo cha juu katika muundo wa Umoja wa Mataifa.

Tuna kila sababu Watanzania kutembea kifua mbele na kwamba viongozi wetu hawakukosea waliompendekeza Rais Samia kuwa Mgombea Mwenza na hatimaye leo anatuongoza katika misingi ya kiungwana, kistaarabu, mwenye kujali utu, huruma kwa raia wake, mpenda haki na mwenye kuipenda kwa dhati Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kama bado kuna mtu mwenye mashaka na Rais Samia, hotuba aliyoitoa leo ndio jibu lake.

Rais Samia hakuwa na kipapume, ametulia ameueleza Ulimwengu msimamo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika maeneo muhimu kabisa bila kuacha hata chembe ya shaka.

Ni katika mkutano huu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Viongozi hao wanapitsha kile kinachoitwa New World Order ingawaje sio lazima kupitia hadhira hiyo,lakini kawaida inatendeka hivyo.

Rais Samia kupitia hotuba yake katika mkutano wa mwaka huu wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, wengi wamefahamu Samia Doctrine ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatimiza wajibu wake katika uwanja wa kimataifa ijapokuwa sio Super power,lakini mbele ya macho ya dunia tunasauti na tunaposema tunasikilizwa.

Ule msemo wa kale kwamba Mkataa wengi mchawi, Rais Samia ameiambia Dunia umuhimu wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuishirikiana katika Nyanja mbalimbali.

Ukisoma kisa cha Nyuki utaiona mantiki ya uzito wa hoja ya Rais Samia kuhusu dhana ya kushirikiana na wenzio katika mambo.

Kitendo cha Rais Samia kushiriki vikao mbalimbali nje ya Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na hotuba yake ya leo ni wazi kuwa ameinusuru Diplomasia yetu pakubwa maana ilikuwa tunasemea katika vibuyu.

Akiwa katika Viunga vya Umoja wa Mataifa, Rais Samia amezungumza na Wakuu mbalimbali wa Mashirika ya Kimataifa.

Wamempokea vizuri na hivi ndivyo hali ya mambo inavyotakiwa katika maisha yetu wanadamu, aso hiki ana kile hakuna mtimilifu kila mmoja anamuhitajia mwenziwe.

Huko Marekani Rais Samia hakwenda peke yake kama mchawi, wafanyabiashara wetu wazalendo wametangulia kwa gharama zao na amewakutanisha na wafanyabiashara wenziwao wa huko na mengi yenye faida yatapatikana katika kukwamuka kiuchumi nasi maisha yetu yazidi kutononoka vijana wasikimbilie Ughaibuni kutafuta maisha mazuri.

Mwanafalsafa maarufu wa kale katika Taifa la China,Confucius mojawapo ya mafundisho yake kwa mwanafunzi wake, Tzu Kung, alimfunza juu ya uhusiano kati ya utajiri na umasikini.

Mwanafalsafa huyo alimwambia ukimwona mtu tajiri , basi tamani kuwa kama yeye, lakini, ukimwona aliye masikini, basi, jitafakari wewe mwenyewe .

Rais Samia anatamani nasi Watanzania tuwe matajiri na ndio maana kila uchao amekuwa akifanya kila awezalo kuhakikisha tunatoka hapa tulipo na kufika kama walivyo wenzetu walioendelea kiuchumi kwa kuwa na uchumi mkubwa na endelevu.

Moja katika jambo ambalo linakoleza ukuaji wa uchumi imara ni miradi ya uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje (Foreign Direct Investment-FDI).

Juhudi zinaochukuliwa na Rais Samia ni za kupigiwa mfano katika kukuza uchumi ili tufikie uchumi uliotononoka zaidi katika kuvutia Wawekezaji wenye tija kutoka nje kama uwekezaji wa makampuni makubwa ya nje.

Kama inavyoeleweka Uwekezaji wa makampuni ya nje ni muhimu katika uchumi wa nchi na hususan uchumi wa kileo chini ya biashara huru. Uwekezaji huo unachangia ukuaji wa uchumi wa nchi husika.

Nchi za Dunia ya tatu kama Tanzania zinatilia mkazo katika uwekezaji huo wa FDI,pamoja na biashara ya kimataifa ambazo ni chanzo muhimu cha Maendeleo.

Katika nadharia ya Uhusiano wa Kimataifa, FDI na biashara ya Kimataifa zinapewa uzito mkubwa katika ukuzaji wa uchumi wa nchi zinazoendelea,mchango katika maendeleo ya rasilimali watu, kubadilishana teknolojia ndio msingi wa uchumi wa kileo.

Tanzania hivi sasa ipo pazuri kwenye biashara ya Kimataifa.

Huko Marekani Tumemuona Rais Samia namna anavyochaakazi kwa kufanya vikao na Makampuni makubwa, hii yote ni sehemu ya kuitangaza Tanzania kuvutia Wawekezaji , huwezi kupata Wawekezaji wa maana kwa kufanya ziara za Sikonge au Tandahimba, lazima utoke kimataifa.

FDI ina aina mbili za uwekezaji ambao ni ile ya Fixed asset na Portfolia investment ambazo zote hizo zinachangia ukuzaji uchumi wa nchi inayowekezwa, tembelea katika mradi wa Symbion Power Plant na miradi mengine hapa nchini utathibitisha hili.

Ni jambo lisiloweze kubishaniwa kwamba Tanzania kwa hivi sasa inategemea misingi ya mfumo thabiti na imara wa shughuli za uwekezaji mkubwa kutoka nje na hatua za kuwa na uchumi huru, hali ambayo itastawisha biashara huru ya bidhaa na huduma ikiwemo huduma za bandari.

Faida nyengine ya FDI ni kubadilishana teknolojia, utaalam na pia kuongezeka kwa fedha za kigeni katika nchi.

Mfano bora wa nchi zilizopata mafanikio kwa FDI ni Singapore, Korea Kusini,Hong Kong naTaiwan kwa kuwa na sera nzuri za Uwekezaji-FDI leo nchi hizo zinaitwa Asia Tigers au four dragons.

Kwa mfano, Bandari ya Hong Kong ni miongoni mwa bandari zenye kusafirisha bidhaa nyingi zaidi duniani ikifuatiwa na Singapore.

Tunatagemea pia bandari ya Dar es Salaam nayo iwe kama bandari ya Hong Kong.

Hong Kong pia ni ya mwanzo duniani iliyosheheni Uwekezaji wa moja kwa moja (FDI) huku Taiwan ikiongoza katika dunia kuwa learder in micro-electronic research and development hakuna sababu ya kwanini Jamhuri ya Muungano wa Tanzania isiwe leader in micro-electronic research and development ya Afrika.

Wakati ndio huu, lazima tufunge mkanda na kujituma katika kutekeleza yale tuliyoyapanga.

Tunawajibu wa kuwajibika kwa mwende wa haraka maana hivi sasa mwendokasi wa uchumi wa dunia na ukuaji wa teknolojia haitusubiri na wala hawana nafasi ya kutungoja

MWISHO

IMG-20210923-WA0081.jpg
 
Poppy Hatonn

JF-Expert Member
Apr 9, 2021
338
500
Threshold inaitwa thrash hold . We can see why there was a clamp down on the internet ternet before this spéech.
 
barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
31,666
2,000
MKATAA WENGI MCHAWI

Na Dk Juma Mohammed

Zumari likipulizwa Visiwani, wahemkwao wa Maziwa Makuu.

Naam, katika viunga vya Umoja wa Mataifa katika Jiji la New York, Marekani , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amehutubia kwa mara ya kwanza Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Hii ni hotuba ya kwanza na ya kihistoria kwa Rais Samia kuhutubia katika chombo cha Kimataifa.

Huu ni uthibitisho wa kukubalika kwake katika Umoja huo wa Ulimwengu lakini pia Rais Samia amekuja na bahati ya kipekee katika uongozi wake, nchi yetu imechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Nini tafsiri ya jambo hili katika uwanja wa kimataifa?

View attachment 1950269
Suala la kutoa hotuba ktk baraza la un sio kwamba unakubalika...
Gaddafi katoa hotuba pale akiwa hapatani na mataifa ya ulaya na marekani, ahmadinajan wa iran nae katoa hotuba na kuwatusi wamarekani na eu pale pale, mugabe nae kawatusi pale pale...
Ni utaratibu tu wa wanachama wa un kutoa hotuba sio ukitoa hotuba unakubalika..
 
inchaji

JF-Expert Member
Jul 5, 2019
2,169
2,000
hotuba ya kawaida sana na wala aliyokuwa anayasema siyo akili yake ametumika tu kama kipaza sauti.

imagine alikuwa anashindwa kutamka multilateralism 🤣 yaaani akilifikia hilo neno lazima akwame 🤣 ni ushahidi alichokuwa akikisema pale hajakiandaa wala kukifikiria yeye.
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,593
2,000
Naunga mkono hoja
Hata mimi nimeipongeza
P
 
barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
31,666
2,000
hotuba ya kawaida sana na wala aliyokuwa anayasema siyo akili yake ametumika tu kama kipaza sauti.

imagine alikuwa anashindwa kutamka multilateralism 🤣 yaaani akilifikia hilo neno lazima akwame 🤣 ni ushahidi alichokuwa akikisema pale hajakiandaa wala kukifikiria yeye.
Ila kafanyia sana rehersal na akina waziribwa mambo ya nje...kasoma kama yalivyoandikwa.
 
Earthmover

JF-Expert Member
Sep 28, 2012
18,305
2,000
Naunga mkono hoja
Hata mimi nimeipongeza
P
 
KANYAMA

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
1,080
2,000
Suala la kutoa hotuba ktk baraza la un sio kwamba unakubalika...
Gaddafi katoa hotuba pale akiwa hapatani na mataifa ya ulaya na marekani, ahmadinajan wa iran nae katoa hotuba na kuwatusi wamarekani na eu pale pale, mugabe nae kawatusi pale pale...
Ni utaratibu tu wa wanachama wa un kutoa hotuba sio ukitoa hotuba unakubalika..
Muda pia ni dakika 10. Utatiririkaje sijui bila kusoma
 
MGOGOHALISI

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
852
1,000
Suala la kutoa hotuba ktk baraza la un sio kwamba unakubalika...
Gaddafi katoa hotuba pale akiwa hapatani na mataifa ya ulaya na marekani, ahmadinajan wa iran nae katoa hotuba na kuwatusi wamarekani na eu pale pale, mugabe nae kawatusi pale pale...
Ni utaratibu tu wa wanachama wa un kutoa hotuba sio ukitoa hotuba unakubalika..
Bora mewaambia mapopoma wa Lumumba. Nakumbuka mwendazake alivyopewa uenyekiti wa sadc ikawa kana vile kaupambania kha. Hawa watu ni mbukula kabisa
 
Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
2,279
2,000
MKATAA WENGI MCHAWI

Na Dk Juma Mohammed

Zumari likipulizwa Visiwani, wahemkwao wa Maziwa Makuu.

Naam, katika viunga vya Umoja wa Mataifa katika Jiji la New York, Marekani , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amehutubia kwa mara ya kwanza Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Hii ni hotuba ya kwanza na ya kihistoria kwa Rais Samia kuhutubia katika chombo cha Kimataifa.

Huu ni uthibitisho wa kukubalika kwake katika Umoja huo wa Ulimwengu lakini pia Rais Samia amekuja na bahati ya kipekee katika uongozi wake, nchi yetu imechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Nini tafsiri ya jambo hili katika uwanja wa kimataifa?

Ni kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendeshwa kwa kufuata na kutekeleza misingi ya kidemokrasia na utawala bora.

Nchi yenye mashaka mashaka na demokrasia yake, yenye mazonge juu ya utawala bora kamwe haiwezi kuwa sehemu ya kuongoza chombo cha juu katika muundo wa Umoja wa Mataifa.

Tuna kila sababu Watanzania kutembea kifua mbele na kwamba viongozi wetu hawakukosea waliompendekeza Rais Samia kuwa Mgombea Mwenza na hatimaye leo anatuongoza katika misingi ya kiungwana, kistaarabu, mwenye kujali utu, huruma kwa raia wake, mpenda haki na mwenye kuipenda kwa dhati Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kama bado kuna mtu mwenye mashaka na Rais Samia, hotuba aliyoitoa leo ndio jibu lake.

Rais Samia hakuwa na kipapume, ametulia ameueleza Ulimwengu msimamo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika maeneo muhimu kabisa bila kuacha hata chembe ya shaka.

Ni katika mkutano huu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Viongozi hao wanapitsha kile kinachoitwa New World Order ingawaje sio lazima kupitia hadhira hiyo,lakini kawaida inatendeka hivyo.

Rais Samia kupitia hotuba yake katika mkutano wa mwaka huu wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, wengi wamefahamu Samia Doctrine ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatimiza wajibu wake katika uwanja wa kimataifa ijapokuwa sio Super power,lakini mbele ya macho ya dunia tunasauti na tunaposema tunasikilizwa.

Ule msemo wa kale kwamba Mkataa wengi mchawi, Rais Samia ameiambia Dunia umuhimu wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuishirikiana katika Nyanja mbalimbali.

Ukisoma kisa cha Nyuki utaiona mantiki ya uzito wa hoja ya Rais Samia kuhusu dhana ya kushirikiana na wenzio katika mambo.

Kitendo cha Rais Samia kushiriki vikao mbalimbali nje ya Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na hotuba yake ya leo ni wazi kuwa ameinusuru Diplomasia yetu pakubwa maana ilikuwa tunasemea katika vibuyu.

Akiwa katika Viunga vya Umoja wa Mataifa, Rais Samia amezungumza na Wakuu mbalimbali wa Mashirika ya Kimataifa.

Wamempokea vizuri na hivi ndivyo hali ya mambo inavyotakiwa katika maisha yetu wanadamu, aso hiki ana kile hakuna mtimilifu kila mmoja anamuhitajia mwenziwe.

Huko Marekani Rais Samia hakwenda peke yake kama mchawi, wafanyabiashara wetu wazalendo wametangulia kwa gharama zao na amewakutanisha na wafanyabiashara wenziwao wa huko na mengi yenye faida yatapatikana katika kukwamuka kiuchumi nasi maisha yetu yazidi kutononoka vijana wasikimbilie Ughaibuni kutafuta maisha mazuri.

Mwanafalsafa maarufu wa kale katika Taifa la China,Confucius mojawapo ya mafundisho yake kwa mwanafunzi wake, Tzu Kung, alimfunza juu ya uhusiano kati ya utajiri na umasikini.

Mwanafalsafa huyo alimwambia ukimwona mtu tajiri , basi tamani kuwa kama yeye, lakini, ukimwona aliye masikini, basi, jitafakari wewe mwenyewe .

Rais Samia anatamani nasi Watanzania tuwe matajiri na ndio maana kila uchao amekuwa akifanya kila awezalo kuhakikisha tunatoka hapa tulipo na kufika kama walivyo wenzetu walioendelea kiuchumi kwa kuwa na uchumi mkubwa na endelevu.

Moja katika jambo ambalo linakoleza ukuaji wa uchumi imara ni miradi ya uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje (Foreign Direct Investment-FDI).

Juhudi zinaochukuliwa na Rais Samia ni za kupigiwa mfano katika kukuza uchumi ili tufikie uchumi uliotononoka zaidi katika kuvutia Wawekezaji wenye tija kutoka nje kama uwekezaji wa makampuni makubwa ya nje.

Kama inavyoeleweka Uwekezaji wa makampuni ya nje ni muhimu katika uchumi wa nchi na hususan uchumi wa kileo chini ya biashara huru. Uwekezaji huo unachangia ukuaji wa uchumi wa nchi husika.

Nchi za Dunia ya tatu kama Tanzania zinatilia mkazo katika uwekezaji huo wa FDI,pamoja na biashara ya kimataifa ambazo ni chanzo muhimu cha Maendeleo.

Katika nadharia ya Uhusiano wa Kimataifa, FDI na biashara ya Kimataifa zinapewa uzito mkubwa katika ukuzaji wa uchumi wa nchi zinazoendelea,mchango katika maendeleo ya rasilimali watu, kubadilishana teknolojia ndio msingi wa uchumi wa kileo.

Tanzania hivi sasa ipo pazuri kwenye biashara ya Kimataifa.

Huko Marekani Tumemuona Rais Samia namna anavyochaakazi kwa kufanya vikao na Makampuni makubwa, hii yote ni sehemu ya kuitangaza Tanzania kuvutia Wawekezaji , huwezi kupata Wawekezaji wa maana kwa kufanya ziara za Sikonge au Tandahimba, lazima utoke kimataifa.

FDI ina aina mbili za uwekezaji ambao ni ile ya Fixed asset na Portfolia investment ambazo zote hizo zinachangia ukuzaji uchumi wa nchi inayowekezwa, tembelea katika mradi wa Symbion Power Plant na miradi mengine hapa nchini utathibitisha hili.

Ni jambo lisiloweze kubishaniwa kwamba Tanzania kwa hivi sasa inategemea misingi ya mfumo thabiti na imara wa shughuli za uwekezaji mkubwa kutoka nje na hatua za kuwa na uchumi huru, hali ambayo itastawisha biashara huru ya bidhaa na huduma ikiwemo huduma za bandari.

Faida nyengine ya FDI ni kubadilishana teknolojia, utaalam na pia kuongezeka kwa fedha za kigeni katika nchi.

Mfano bora wa nchi zilizopata mafanikio kwa FDI ni Singapore, Korea Kusini,Hong Kong naTaiwan kwa kuwa na sera nzuri za Uwekezaji-FDI leo nchi hizo zinaitwa Asia Tigers au four dragons.

Kwa mfano, Bandari ya Hong Kong ni miongoni mwa bandari zenye kusafirisha bidhaa nyingi zaidi duniani ikifuatiwa na Singapore.

Tunatagemea pia bandari ya Dar es Salaam nayo iwe kama bandari ya Hong Kong.

Hong Kong pia ni ya mwanzo duniani iliyosheheni Uwekezaji wa moja kwa moja (FDI) huku Taiwan ikiongoza katika dunia kuwa learder in micro-electronic research and development hakuna sababu ya kwanini Jamhuri ya Muungano wa Tanzania isiwe leader in micro-electronic research and development ya Afrika.

Wakati ndio huu, lazima tufunge mkanda na kujituma katika kutekeleza yale tuliyoyapanga.

Tunawajibu wa kuwajibika kwa mwende wa haraka maana hivi sasa mwendokasi wa uchumi wa dunia na ukuaji wa teknolojia haitusubiri na wala hawana nafasi ya kutungoja

MWISHO
View attachment 1950269
Risala ndefu isiyokuwa na cha maana. Hizo nafasi za uongozi kwenye UN ni za mzunguko, hakuna upekee wowote unaotazamwa.

Kuna wakati, katikati ya kulaaniwa sana juu ya uminywaji wa Demokrasia nchini Libya, Libya hiyo hiyo ikawa mjumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Nafasi hizo za uongozi za kzunguko inapewa nchi, siyo Rais.

Unaweza kumpongeza mama kwa kuzaa lakini siyo tukio la ajabu au tuseme umefanya kitu cha pekee wakati ni kawaida kwa kila mwanamke kuzaa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom