Kama bado hajapimwa, kwanini asipimwe?

Inawezekana walipambanua wakaona wasiojulikana wanawezakuwa wameandaa mazingira kwenye hizo hospitali kubwa wammalizie kwa sindano ya sumu
 
Hivi hii animus dhidi ya Mbowe inatokana na nini?

Sina animus yoyote ile dhidi ya Mbowe. Simjui kivile naye hanijui.

Hivi tumefika mahali ambapo mtu yeyote anayetaka haki itendeke kuhusiana na kuumia kwa Mbowe anahesabika kuwa ni mfuasi wake?

Hilo umelianza mwenyewe kwa kutumia neno ‘wenzako’. Rudi usome vizuri ulichokiandika na ambacho nimekinukuu.


Hata mimi nataka uchunguzi kamili ufanyike. Kama kweli alikuwa amelewa, basi hilo nalo liingizwe katika mlinganyo ili ukweli wa kilichotokea ujulikane.
 
Chadema wamesema kavunjwa mguu, bungeni imesemwa kateguka mguu baada ya kuteleza kwenye ngazi kwa sababu ya ulevi. Kama kateguka maana Yake kaumia ila hajavunjika hata daktari aliyemtibu kasema hajavunjika.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kinachotafutwa hapa ni nani kusababisha kuteguka au kuvunja mguu wake. Wanaosema kuwa aliteguka kutoka na ulevi wake watoe ushahidi au bora zaidi wawasilishe kwa mamlaka husika inayofanya uchunguzi wa tukio. Lakini Daktari bingwa aliyemtibu amesema wazi kuwa alikuwa na mvunjiko kwenye mfupa unaoitwa fibla.

Amandla...
 
Humu jukwaani tunapingana kwa sababu za kisiasa. Hata wabunge wanaosema alikuwa kalewa ni wapinzani wa Mbowe na chadema, wanaopinga kuwa hakuwa kalewa ni chadema ambao ni wapinzani wa CCM.
Sasa ili ukweli ujulikane acha polisi wachunguze tupate ukweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je, kulewa kubazuia vibaka wasikuvamie?? Ikiwa ndivyo, basi tutakubali kuassume kuwa pombe inaweza kuwa ilisababisha kuteleza na kuumia lkn kama sivyo, basi ipo haja ya vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina jambo ambalo naamini linaendelea
 
Apimwe blood alcohol level kwani kuna jinai amefanya? Mtu anapimwa blood alcohol level kama kuna jinai amefanya au kuna dalili za kufanya kosa ambalo litasababisha madhara kwake au kwa wengine.
 

Nadhani ungejizungumzia mwenyewe ingekuwa vizuri. Sio watu wote wanaosema kuwa ulevi usiwe kigezo cha kwanza ni Chadema. ingawa ni vigumu kuamini lakini kuna wakati katika jukwaa hili watu walikuwa wanapingana kwa hoja bila kujali vyama. Wengine bado tuna msimamo huo huo.

Amandla....
 
Kwani hata kama alikuwa amekunywa, pombe inazuiaje hoja ya kuwa kapigwa na watu wasiojulikana??
 
Mbna umekuja na majibu yako ww poyoyo?
 
Binafsi natamani kujua Mbowe alipovamiwa ilikuwa na muda gani, na alikuwa anatoka wapi. Na huko alikokuwa, alikuwa anafanya nini.

Kama kuna ukweli kuwa Mbowe alikuwa amelewa basi itatia doa heshima yake kwenye Jamii japo ulevi ni jambo Personal. Itampasa kujitathmini kama anastahili kuendelea kuongoza Chama baada ya kukumbwa na kashfa ya Ulevi.

Japokuwa yeye kulewa haiwapi uhalali watu kumfanyia kitendo cha kinyama kama kumpiga ama hata kumtweza kwa namna yeyote.
 
Hoja zako za Kisengerema sana, hivi na wewe ni msengerema kama Daudi Albert Bashite na Jiwe???
 
Chadema waache huu mjadala ufe wenyewe kama taarifa hizi ni kweli. Mbowe anastahili faragha na kuheshimiwa kwa mchango wake.
 

Nyani ni nyani tu hawezi kubadilika akawa Mtu kama "evolution science" inavodanganya watu....!
We nyani ni lini au sheria ipi inayosema mtu akilewa chakari na ikatokea akavamiwa na kushambuliwa na wasiojulikana ni HALALI?
Tuondolee akili za kinyani hapa!
 
Halafu, kama kapigwa kweli, ina maana kapigwa kimyakimya?

Hakupiga hata mayowe? Majirani zake hawakusikia purukushani? Au hana majirani yeye?
Majirani wenyewe wa maccm roho mbaya sha hata Kama yamesikia utafikiri yatasema ukweli Tena mbele ya bunge unataka majina yasirudi nini,shambulio la lisu tu majirani zake Tena wakubwa serikalini walikimbilia kungoa cctv camera,ccm ni mashetani
 
Chadema waache huu mjadala ufe wenyewe kama taarifa hizi ni kweli. Mbowe anastahili faragha na kuheshimiwa kwa mchango wake.

CHADEMA siyo CCM comrade!
CHADEMA Ina watu makini wanaojua wanafanya nini.
Wala Mbowe siyo Kitwanga aliyeingia Bungeni amelewa na kushindwa kujibu maswali ya Wizara yake alipokuwa Waziri!
Hoja ya kwamba alilewa na alikuwa na kimada IS NOT AN ISSUE HERE!
The issue is: NANI WALIMSHAMBULIA MHE. MBOWE HUKU WAKIDAI AACHE KUMTUKANA/KUMSUMBUA RAIS MAGUFULI HIVO WANAVUNJA MGUU HALAFU WAONE ATAFANYAJE KAMPENI!!
Akili ya kawaida kabisa haikubaliani na huu ushenx unaodaiwa na Wabunge Mafisccm na Policcm yao. Swali ni: KUNA WALEVI WANGAPI TANZANIA WANAOLEWA NA KUANGUKA BAADA YA KULEWA CHAKARI KIASI CHA KUUMIA SEHEMU ZA MIILI NA KULAZWA WAKIWA MAHUTUTI?
Kama kweli Kuna hiyo CCTV Video footage recorded tunaomba iwekwe hadharani! Itakuwa ni ushahidi tosha lakini pia hapohapo CHADEMA waombe na CCTV footage ya MHE. TUNDU LISSU alipopigwa risasi zaidi ya 30 tarehe 7 Sept, 2017 ili tuwajue hao wasojulikana!
 
Kwani hata kama alikuwa amekunywa, pombe inazuiaje hoja ya kuwa kapigwa na watu wasiojulikana??
Pombe haizuii chochote kutokea. Lakini pia yaweza kuwa ndo chanzo cha yote kutokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…