Kama Adamu na Hawa wasingepelekwa Bustani ya Edeni kusingekuwa na KIFO

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,894
KAMA ADAMU NA HAWA WASINGEPELEKWA BUSTANI YA EDENI KUSINGEKUWA NA KIFO;

Anaandika, Robert Heriel
Mwanafalsafa

Tunasoma, Mungu alipomaliza kumuumba Mtu(Adamu) Kwa mfano wake akamchukua huyo mtu akiwa tayari Nafsi hai, akampeleka mpaka ilipo Bustani ya Edeni, Bustani ambayo Mungu mwenyewe aliiandaa Kama zawadi Kwa mwanaye Adamu.

Huenda uliwahi kuziona Bustani nzuri zenye kupendeza ambazo zimeundwa na Sisi binadamu, sasa unaweza kuchora picha kuwa Bustani iliyoundwa na Mungu mwenyewe ilikuwaje.

Katika Ile Bustani tunaoneshwa baadhi ya vitu vilivyokuwa mule kama vile Mito mizuri ya kuiogesha na kuimwagilia Bustani hiyo, Miti mizuri, Maua na miti ya matunda ya kushangaza ya kila namna, pamoja na Wanyama mbalimbali watakaokidhi mahitaji ya Adamu.

Wanyama walioripotiwa kuwapo katika Bustani hiyo ni Wanyama wawili ambao ni Nyoka na Kondoo ambao nao ni sehemu muhimu ya kisa hicho cha kusisimua.

Nilisema kuwa Wanyama waliowekwa Bustani ya Edeni Kwa kadiri ya mahitaji ya Adamu na vile Mungu alivyoona Yafaa iwe hivyo. Kuacha wanyama tunaona pia dhahabu nayo inatajwa kama moja ya vitu vilivyokuwapo Bustani ya Edeni

Kitu kingine ni Miti miwili ambayo yote ilikuwa katikati ya Bustani hiyo ya Edeni. Mmoja ukiitwa MTI WA UJUZI WA MEMA BA MABAYA, na ule wa pili ukiitwa MTI WA UZIMA. Yote ikiwa katikati ya Bustani hiyo. Kisayansi na kifalsafa kitu kuwa katikati ni kumaanisha ni msingi au kiini cha kitu au Jambo Fulani.

Unaweza kuungana na Mimi Taikon kujiuliza ni Kwa nini Miti hiyo iwekwe katikati ya Bustani na sio pembeni kabisa ya Bustani, ni Kwa nini?

Huo ni mjadala WA siku nyingine. Lakini ninachoweza kukuacha nacho kama homework ni kuchunguza vitu vilivyokatikati vinatabia na sifa zipi, unaweza angaalia hata kwenye Human anatomy and physiology Kwa kucheki viungo vya Mwili Kama jicho, masikio, Ngozi, ubongo, n.k.

Au unaweza kuangalia Geomorphology Kwa kucheki maumbile ya Dunia kama internal Earth structure na External Earth Structure kisha uangalie tabia na sifa za vitu vilivyokatikati labda unaweza kupata mantiki ya kwa nini miti hiyo miwili iwekwe katikati. Na kuchora picha ilikuwaje.

Turejee kwenye mada,

Zingatia dunia yote Mungu alipoiumba yote ilikuwa ni njema Sana. Na kila alipoumba alikiri kuwa ni chema, hapo ni kabla hajaumba hiyo Bustani.

Alipoumba Bustani hakusema wala kukiri ilikuwa ni njema ingawaje tunaamini ilikuwa ni njema kutokana na vitu vyema vya kuvutia alivyoviweka bustanini, Nani asiyejua dhahabu ilivyonjema, Nani asiyejua miti mizuri yenye kuvutia na kutamanika Kwa Kula ilivyo njema.

Lakini Mungu akiwa tayari kamuumba Adamu na keshampeleka Bustanini Edeni ili ailime na kuitunza akisema Kwa mara ya Kwanza sio vyema mtu(Adamu) awe pekeake nitamfanyia Msaidizi wa kufanana Naye.

Maandiko yanasema Adamu akapata usingizi kisha Mungu akatwaa sehemu ya nyama katika ubavu wake na kumuumba Mwanamke, Hawa.

Ubavu ni moja ya sehemu za mwili WA Mtu ambao upo katikati au karibu na katikati ya Mwili WA binadamu.

Kupitia ubavu kiungo kilichokatikati ya Mwili WA binadamu aliumbwa mwanamke, mnaweza kuona sifa na tabia za wanawake zilivyo.

Kwa harakaharaka sifa za wanawake za kimaumbile ni wazuri wenye kuvutia, lakini sifa za kitabia ni kwamba hawana msimamo yaani ni viumbe visivyotabirika kutokana na sifa za katikati kwamba havieleweki vipo juu au chini.

Ni Kama Popo hajulikani ni mnyama au ni Ndege.
Au Maeneo yaliyokatikati ambayo hubeba tabia za pande zote mbili.
Sijui Kama unapata concept Fulani hapa.

Kwa lugha nyepesi kurahisisha Uelewa wa baadhi ya watu;
i. Hapa tunazungumzia Bustani ya Edeni.
ii. Katika miti mingi kuna miti miwili iliyopowekwa katikati, mmoja ni Mtu wa Ujuzi WA Mema na mabaya, na mwingine ni Mtu WA uzima.

iii. Anaumbwa Mwanamke kutoka katikati ya Mwili WA mwanaume(ubavuni)
iv. Huyo mwanamke aliyeumbwa katikati ya Mwili WA Adamu anakuwa Mtu WA Kwanza Kula matunda ya katikati ya mtu wa Edeni.
v. Adhabu inatolewa lakini nyingi alizopewa mwanamke zinahusu Eneo la katikati ya Mwili wake.
vi. Adamu anafukuzwa Bustani Edeni ili wasijekula mti wa Kati wa Uzima.

Haya sijui kama umepata ninachojaribu kukieleza hapa.....

Maandiko yanatuambia Mungu alitoa Menu ya mtu mmoja kuliko kitu mingine. Mti huo ni moja ya Ile miti miwili iliyokatikati.

Miti mingine aliambiwa ale tuu lakini mtu mmoja akaambiwa asile Kwa maana siku atakayokula atakufa Hakika.

Kwa hiyo Matunda ya mti ule yalikuwa na sumu(Kifo/Mauti) yaani kifo patterns na codes zake zilifungwa katika Matunda ya mtu ule wa Ujuzi wa Mema na mabaya.

Lakini maandiko hayatuambii na hayatupi sababu ya Kwa nini matunda hayo mengine aliyoambiwa Adamu Ale, Kwa nini Mungu hakutoa Sababu ya Kueleza nini kawaruhusu kuyala matunda hayo. Yaani hakutoa Menu ya Kueleza faida yakula hayo matunda mengine Ila alieleza sababu ya kutokula matunda ya mtu wa Ujuzi WA Mema na mabaya kuwa ni Kifo.

Tunaona Mungu akiwafukuza Adamu na Hawa pale bustanini ili wasijekula matunda ya Uzima.
Kumbuka hawakujua pembeni ya mti wa Ujuzi WA Mema na mabaya kuna mti WA uzima Kwa sababu nilishasema hawakupewa Menu.

Hii inatuambia nini;
i. Ukiona kila tatizo au janga basi jua pembeni ya janga Hilo kuna Suluhisho. Au kila lililojema au lenye baraka basi jua karibu yake au pembeni yake lipo lililobaya na lenye laana.

ii. Inatuambia pia, hakuna Jambo zuri lisilo na kasoro au lisilo na masharti.
Adamu alipelekwa Bustani ya Edeni ilivyokuwa nzuri Sana lakini kumbe ndani yake ndimo kulikokuwa na mti wenye Sumu na Code ya kifo.
Ndio ule msemo sijui wa No free lunch ulipoanzia.

Kama Mungu angemuacha Adamu Duniani angeishi maisha ya kawaida lakini asingekutwa na Kifo.

Maswali ya kujiuliza,
i. Adamu na Hawa Walikula matunda mangapi ya ule mti wa Kifo?

ii. Mbegu za matunda hayo walizipeleka wapi?
Najaribu kuchora picha walivyomsikia Mungu akija walivyovurumuka kukimbia USO wa Mungu.
Je walificha maganda na mbegu za matunda hayo?
Au je lilikuwa ni tunda la kuliwa maganda na mbegu zake?

iii. Je nyoka/Shetani angali akijua pembeni ya mtu WA Ujuzi WA Mema na mabaya kuna mti WA uzima, je hakuchuma Yale matunda ya mti wa uzima na kuchukua mbegu zake ili kuzitumia Kwa kazi zake hasa za Ulimwengu wa rohoni?

Au je, maandiko yanaposema Yesu alishuka mpaka kuzimu kumnyang'anya Shetani funguo za mauti ambazo bila Shaka alizipata pale Edeni je ndio zile mbegu za matunda ya mtu wa uzima alizoziiba pale Bustani ya Edeni?

Tutaendelea na mjadala na kujibu baadhi ya maswali hayo na mengine mengi katika maandiko yanayofuata.

Ila Kwa sasa tuhitimishe kuwa, Pasipo Edeni mwanadamu asingekufa,
Na pasipo kanuni ya Asili ya "Katikati" mwanadamu asingeanguka wala kuasi.
Mijadala mingine inayoendana na kanuni ya Katikati "The middle Rule" nimeonelea na kuiita ndio msingi wa chanzo cha uhai na mauti Kwa mwanadamu.
Hata katika Menstruation ya mwanamke, kanuni hii ya Katikati inafanya kazi katika Ovulation ya yai la mwanamke ambalo hutoka kwenye Ovari katikati ya mwezi(siku ya 14) na kuingia katika mishipa ya Fallopian Kwa ajili ya urutubishaji.
Taikon kupitia kitabu cha "NADHARIA ZA TAIKON" nimefafanua mada hiyo ya "KANUNI YA KATIKATI"

NIPUMZIKE SASA!

SABATO NJEMA

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom