Kilichotokea Duniani Baada ya anguko

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Jun 29, 2023
286
582
Utangulizi

Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewa akala Mwanzo 2:6

Baada ya Mwanadamu kuhasi maelekezo ya Mungu pale bustani ya Edeni akala matunda ambayo Mungu alimuelekeza asile kitendo kile kilichofanyika bustani ya Edeni matokeo yake

Mosi Mbinguni

Mbinguni kulikuwa kimya kabsa wale Malaika watakatifu ambao kazi Yao ilikuwa ni kufurahi Kwa ajili ya Kazi ya Mungu kumuumba Mwanadamu walinyamaza kimya kukawa na kilio na kusaga maneno Kwa wale Malaika vinanda vikazimwa, matarumbeta yakazima , vinubi, matali na kila aina ya zana za uumbaji zilikoma mbinguni kukawa kimya

Luka 15:10 Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.

Furaha yote mbinguni ilileyuka ghafla kukawa kimya , Mungu akashikwa na mfadhaiko WA kile alichokifanya Mwanadamu akasikitika Sana Kwa kile kilichofanyika duniani.

Kutoka 32:7-8 BWANA akamwambia Musa, Haya! Shuka; kwa maana watu wako uliowatoa katika nchi ya Misri wamejiharibu nafsi zao,

[8]wamepotoka upesi kuiacha ile njia niliyowaamuru, wamejifanyizia ndama ya kuyeyusha wakaiabudu na kuitolea dhabihu, wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri.

Mungu akashuka duniani ili kwenda kuangalia ni namna gani anaweza kumsaidia , akauzunika zaidi alipotegemea Mwanadamu kuomba toba ili aweze kumsaidia mwanadamu akawa mkaida wakitupiana lawama , Mungu akapata hasira akawapa adhabu wanadamu

Kutoka 32:7-8,11
[7]BWANA akamwambia Musa, Haya! Shuka; kwa maana watu wako uliowatoa katika nchi ya Misri wamejiharibu nafsi zao,

[8]wamepotoka upesi kuiacha ile njia niliyowaamuru, wamejifanyizia ndama ya kuyeyusha wakaiabudu na kuitolea dhabihu, wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri.

[11]Musa akamsihi sana BWANA, Mungu wake, na kusema, BWANA, kwa nini hasira zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu, na kwa mkono wenye nguvu?

Mwishoe Mungu akawakasirikia wanadamu aliowaumba Akatoka adhabu Kwa wanadamu

Mwanzo 3:8,11 Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone.

Mungu akasikitika Sana Kwa habari za Mwanadamu aliyemuumba na kwa sababu Mungu ni wa haki wala asemi uongo alichokisema kina kuwa na kwake hakuna upendeleo , alichokisema Kwa wanadamu kikawa

Mwz 3:11 Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?

Mwanzo 2:16-17
[16]BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,

[17]walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.

Baada ya Mungu kujiona pale bustani na mwandamu kushindwa kutumia nafasi ya kumwomba Mungu samahani Kwa kile alichofanya kuomba toba , Mungu Akatoa adhabu.

2 Wakorintho 1:20 Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi.

Zaburi 138:2 Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu,
Nitalishukuru jina lako,
Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako, Kwa maana umeikuza ahadi yako,
Kuliko jina lako lote.

Kitu ambacho kinamtofautisha Mungu wetu katika Kristo Yesu ni uhaminifu katika ahadi zake hakuna Mungu mwaminifu kama Huyu asikwambie MTU akisema kitu hakika atakitimiza
 
Baada ya Dhambi na Adhabu kikaitwa kikao cha Dharura mbinguni kikao Kikuu ambacho walikaa viongozi watu , Mungu Baba , Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu kama kile kikao cha Kwanza cha kumuumba Mwanadamu

Mwanzo 1:26
[26]Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

Hicho kikao kilikuwa na ajenda moja Tu , nimtume Nani aweze kumwokoa Mwanadamu, kikao kilikaa kimya kidogo

Ukimya wa kikao ulikuwa ni Nani ambaye atakubali kutoka mbinguni kuja duniani kwa jinsi ya Mwanadamu Mwenye dhambi na kulipa Dhambi za Mwanadamu Kwa njia ya Mauti ili mwanadamu aweze kukombolewa kutoka utawala wa shetani, halikuwa Jambo Raisi sana wala kufikiriwa wala kuwaziwa.

Isaya 6:8 Kisha nikaisikia sauti ya Bwana, akisema, Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo niliposema, Mimi hapa, nitume mimi.

Katika ukimya ule Mungu Mwana akasema nitume Mimi nitakwenda Kwa ajili ya Mwanadamu, kukawa na uzuni nyingi mbinguni , wale watatu walikuwa kitu kimoja kama vile mwili wa mwanadamu ambavyo Una nafsi, roho na mwili

Kwahiyo kitendo cha Mungu Mwana kukubali kuja duniani kwa ajili ya dhambi zetu, kungepelekea utengano katika ya wale watatu , na ndio maana ili bidi Mungu Mwana kuchukua mwili WA mwandamu aweze kuja kulipa mshahara wa dhambi ambao ni mauti

Warumi 6:23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele

Mungu Mwana alipokubaki Tu kuchukua dhambi za Mwanadamu akapewa Jina la Mungu Baba Jina la Yesu ili atakapokuwa duniani asiwe pekee yake awe pamoja na Baba

1 Samweli 25:25 .......kwa maana kama lilivyo jina lake ndivyo alivyo yeye..

Baada ya Mungu Mwana kukubali kuja duniani , kukawa furaha mbinguni malaika wote wakafurahi juu ya Wokovu wa Mwanadamu

Mungu Baba akakwa na kikao na Mungu Mwana juu ya maamuzi yake Kwa Mwanadamu , juu ya Upendo alionao Kwa wanadamu aliwapenda upeo kiasi cha kwamba akakubali kufa kwa ajili Yao , hakukuwa na upendo Mkubwa kiasi kile

Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Baada ya Yesu kukubali kufa kwa ajili ya dhambi za Wanadamu msalabani kulikuwa na kilio duniani shetani na malaika zake walilia kilio cha kusaga meno hawakujua kwamba Mungu anaweza kulipa gharama ya kufa kwa ajili ya Mwanadamu wakajua dili lao la kumfanya Mwanadamu kuwa mateka na mtumwa WA shetani limefeli

Shetani alikuwa anajua kabsa kitendo cha kumshinda mwanadamu hakukuwa na namna yoyote duniani ya Mwanadamu kusaidiwa kwa sababu hakukuwa na mwanadamu Mwenye haki mbele za Mungu kulipa deni la dhambi ndio maana walikuwa wanafurahia Kwa kucheza na kuimba

Kitendo cha Yesu kuja duniani kilikuwa ni kilio Kwa shetani kwani Shetani alitapanga Mungu akose hata mmoja ambaye atamwabudu yeye Kwa hiyo kitendo cha Yesu kukubali kufa kwa ajili ya Mwanadamu ilikuwa ni ngumu ya pua Kwa shetani hakika Mungu aliupiga mwingi vijana wa Leo wanasema

Ambacho hakujua shetani kwamba Mungu alikusudia hata mwanadamu anatenda dhambi alikuwa ameweka mpango tayari wa kumwokoa hendapo mwanadamu atatenda dhambi.

Mathayo 8:28-29 Naye alipofika ng’ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile.
.
[29]Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?

Shetani akafanya kila vigisu kuhakikisha kwamba Yesu Haji duniani kwa sababu alitakiwa kuja Kwa njia ya mwili WA mwanadamu , akaweka kila aina magonjwa , vifo kwa wakina mama ili Tu Yesu asizaliwa lakini Mungu ni Mungu Tu Yesu akazaliwa

Yesu akakua akawa akafanya kazi yake aliyotumwa alikuja kuleta ukombozi na ndio maana pale msalabani alisema imekwisha

Wakolosai 2:13-14 Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote;

[14]akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo;

Siku zote nacho muomba Mungu daima siku ile ambayo atakuja kuwachukua watu wake namimi nisikose, kitendo alichokifanya Yesu pale Msalabani Kwa kweli alituheshimisha shetani mwenyewe anatetemeka Kwa kile kitendo hakutegemea, hakufikiria , hakuwai kuwaza ndio maana kila siku anatupiga vita ili Tu tusimwamini Yesu ili aendele kututesa

Kitendo cha kuokolewa katika dhambi hakuna kitendo kikubwa kama hicho usiku na mchana ni maombi yangu kwa Mungu siku ile niwepo sio Mimi Tu na ndugu zangu na watanzania wenzangu

Shetani siku zote anaweka figusi Kwa wanadamu wasijue kile kilichoko kwenye msalaba Kwa kuleta udini na vitu kama hivyo Ila msalaba ni zaidi ya dini ilikuwepo Kabala hata dini kuwepo Ila tumepigwa chenga na shetani kwenye udini

Msalaba ndio haisili ya ukombozi na Damu ndio asili ya msamaha ukiona MTU anamwaga Damu Kwa ajili ya ibada anajua anatafuta nini Kwa hiyo Damu lakini mwambie kuna Damu ya Yesu aachane na Damu za wanayama , Yesu tayari kamwaga Damu yake


Unaweza kuiita Damu ya Yesu ikakukomboa kutoka katika dhambi , kiukweli msalabani Yesu aliupiga mwingi , Mwanakondo ameshinda na Tumfuate
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom