Kam dispensary Ilala

Speedo

Member
Feb 15, 2011
70
19
wanaJF, jana nilipitia hapa KAM Dispensary (jirani na Amana hospital) kucheki Malaria.

Nikiwa maabara nilimsikia mhudumu wa hapo akilalamika kuwa hawana maji ya bomba wala kwenye chombo chochote ya kuwawezesha kufanya shughuli zao vizuri na wameshalalamikia uongozi wao zaidi ya juma (week) moja bila mafanikio. Upimaji unaendelea na mimi walinipima pia ila sikuzingatia majibu yao kwa kuwa tayari nilishachefuka.

Mwaka jana walifungiwa sikujua ni kwa kosa gani pakafunguliwa baada ya muda mfupi.

Je naweza kushtaki/kueleza/kulalamika wapi kuhusu hili?

Je kwa mtindo huu si unaweza kukutwa na ugonjwa kumbe ni wa mwingine sio wako? Maana swala la usafi tayari ni mgogoro.

Ni nani wakaguzi wa hizi ofisi?

Nawasilisha.
 
hospital na dispensary zenye vipimo na majibu ya ukweli chache sana!nenda wizarani watakuelekeza pa kushitaki ingawa hali hiyo ni kila mahali!bila umeme atapima kwa darubini?
 
Maji ni kitu muhimu sana maabara hata kama malaria wanapima kwa RDT, kama maji safi na salama hakuna lazima huduma zisimamishwe.
 
Kwa kweli usahihi wa majibu yanayotolewa na maabara nyingi ndogondogo ni wa mashaka. Wengi hawasimamishi upimaji wakiishiwa au kupungukiwa vitendea kazi muhimu.
 
Kwa kweli usahihi wa majibu yanayotolewa na maabara nyingi ndogondogo ni wa mashaka. Wengi hawasimamishi upimaji wakiishiwa au kupungukiwa vitendea kazi muhimu.


Nakubaliana na wewe 100%. Kulikuwa na maabara moja huko ilala jirani na amana hospital pia - shariff shamba (kwa sasa panauzwa computers) walikuwa na vipimio/darubini mbovu ipo tu mezani, unatoa damu anakuambia utoke after 5mins una results.

Niliwahi kwenda nikiwa nafahamu usanii wao nikatolewa damu, wakati anaiandaa kabla sijatoka nikaweka karatasi sehemu ya kupimia kwenye microscopy, nilipoitiwa majibu nikaikuta karatasi haijaguswa na nina malaria 2. Maana yake haikutumika.

Nashukuru pamefungwa kwa sasa sijui wamehamia wapi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom