ruaharuaha
JF-Expert Member
- Feb 14, 2018
- 4,453
- 5,711
Serikali ni pana sana na kazi ya serikali ni kuhudumia wanachi wake, kuna vitu ambavyo huwa matokeo yake yanaonekana moja kwa moja na mengine sio.,kwa maana hiyo usipende sana kuitupia lawama SERIKALI ambayo kiongozi wake ni mh rais SSH.Hebu jiulize ww moyoni mwako unaitendea nini TANZANIA YETU.
Kwahiyo mgao wa umeme, wa maji, mfumuko wa bei, kuondoa ruzuku kwa wakulima wote, kufukuza wachapakazi, kuwaweka washikaji, ndugu.
Kuchoma masoko, kufukuza machinga mjini bila kuwapa alternative ya maana, Masai next, umeme, tozo, kodi lukuki, kutokemea udini, ukabila, ukanda, ubinafsi.
Kuhimiza viongozi wale kwa urefu wa kamba zao,ila wasivimbie,kutokuwa na sera, maono, serious hata kwa kitu kimoja.
Kukopa hovyo hovyo na kupeleka pesa zaidi ya 20% siku zote Zanzibar, idadi ya watu chini ya 3% ya Watz.
Kuzuzura ili kupiga picha na Wapuuzi Flani hii ndio mipango ya serikali hii, yenu kuwahudumia Watanzania.
Siitupii lawama yoyote, kila kitu kipo kwenye vyombo vya habari.
Unaniuliza nimeitendea nini Tanzania, ninalipa kodi, tozo, madeni mnayochukua, tozo,mikopo, maamuzi ya hovyo,tutayalipia sisi.
Swali zuri ni mmeitendea nini Tanzania wewe na Serikali yenu?
Mmefanya nini cha maana kwa kodi zetu, au ni posho, kusafiri, kuteuana, kupiga dili, kufanya maisha ya Watz wengi yawe magumu zaidi?