Kalamu ya Askofu Bagonza: Sio pigo kwa Tundu Lissu, Tumepigwa Wote

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
50,136
Reaction score
96,161
Kalamu ya Baba Askofu Mch. Dr. Kalikawe Lwakalinda Bagonza

SIYO PIGO KWA Tundu A. M. Lissu Tumepigwa Wote.

Nimesikia baadhi ya watu wanasema Tundu Lisu amepata pigo mahakamani baada ya mahakama kuamua kwamba mashahidi watakaotoa ushahidi katika kesi ya uhaini, watakuwa wa siri. Yeye hatawajua na umma hautawajua, hautawaona, na hata familia zao hazitajulikana. Hili Si pigo kwa Lisu. Ni pigo kwa mahakama na pigo kwa haki. Zingatia.

1. Tunazo mahakama tatu: Mhimili wa dola, mahakama ya umma na ya Mwenyezi Mungu. Hii ya mwisho haina rufaa na ndiyo pekee yenye mashahidi wa siri. Jaji ni Mwenyezi Mungu. Uamuzi wa leo unaigeuza mahakama ya dola kuwa ya Mungu. Haikubaliki.

2. Serikali iliyotaka kupinduliwa ni yetu wananchi. Si ya Rais wala chama. Umma una haki kuwajua na kuwahoji mashahidi waliotusaidia kuzuia serikali yetu isipinduliwe na huyu mhaini. Kuwaficha mashahidi ni kuwanyima haki ya kutambuliwa uzalendo wao.

3. Uhaini ni kosa kubwa (high crime). Mahakama huendesha kesi hizi kwa wazi na kuwaadhibu wakosaji kwa wazi ili kutoa fundisho kwa wengine. Leo tunaficha mashahidi, kuna siku tutaficha wahaini na kuwanyonga mafichoni. Haiwezekani kuipindua serikali sirini. Aliyeshauri mashahidi wa kesi hii wawe siri afutiwe matokeo ya elimu yake. Sina tatizo na Jaji aliyekubaliana na ushauri huu. Kuna kupigwa upofu feki unaoitwa “maelekezo toka kinyume cha chini”.

4. Mtuhumiwa wa uhaini ana haki zake. Moja ni kuwajua wanaomshtaki (ambao ni sisi Jamhuri), na kuwajua wanaoshuhudia uhaini wake. Kwa kuwa ni mtuhumiwa na kwa msingi wa uamuzi wa kulinda mashahidi, hata yeye angefichwa tusimjue ili ikitokea akashinda kesi, tusiendelee kumwona na kumnyanyapaa kuwa ni mhaini. Tungemwona tu baada ya kuhukukiwa. Kwa kuwa tunamjua mtuhumiwa, tuwajue mashahidi.

5. Kuingiza au kuonekana unaingiza mizengwe mahakamani ni kuifanyia uhaini mahakama yetu. Mtu mmoja aitwaye Tundu Lisu asifanywe kuwa ana nguvu na umuhimu wa kulazimisha mahakama yetu inajisiwe. Mahakama ina wajibu wa kuitetea heshima yake. Umma una haki ya kutetea uhuru wa mahakama.

6. Kutumia siasa kutatua masuala ya kisheria au kutumia sheria kutatua masuala ya kisiasa ni kufanya uchochezi na kuchonganisha siasa na sheria. Katika mwaka wa uchaguzi, ni kuwachagulia wananchi viongozi kinyume na matakwa yao. Tunaandaa uongozi wa kutawala miili badala ya mioyo. Kuna watu wengi saaana wako tayari kumchagua Rais Samia akiwa na mpinzani kuliko akiwa peke yake.

7. Yanayoonekana kupitia chaguzi ndani ya vyama ni kielelezo halisi cha hali ya nchi yetu. Huu si uchaguzi, si uchafuzi, ni urasmishaji wa rushwa katika taifa letu. Baada ya kupata viongozi kupitia mtindo huu, hatuwezi kupata kiongozi wa kupambana na rushwa. Wapi hapajafikiwa na rushwa katika taifa letu?!

8. Tuliwahi kuwa na gaidi feki. Ikiwa tumeruhusu mashahidi wawe siri
na ushahidi uwe siri, basi tutakuwa na mhaini feki. Pia tunaye kijiweni msaliti feki anayedaiwa ni mchanga katika chama chetu “kinachochukia” rushwa. Ufeki
huu utatufanya tuone kila kitu ni feki. Nimeishaitwa Askofu feki.

Hukumu hii inasisitiza TURUDI MEZANI.
Mahakamani hakuna msaada.
 
Ubongo ,mkono na karamu ya Askofu Bagonza huandika hekima, busara, fikra na maono yenye utukufu na hofu ya Mungu.

Viongozi wetu wamechagua kututawala kadri wapendavyo wao na sio kutuongoza kadri tutakavyo sisi.

Viongozi wamechagua kuunda genge lao na wapendwa wao kusudi lake likiwa kunyanyasa, kukandamiza na zaidi kuhararisha uhuni, udhalimu na unyanyasaji dhidi ya watu wenye mawazo mbadara na tofauti na wao.

Ni wazi kuwa uongozi huu wa awamu ya 6 ulikuwapo ndani ya awamu 5 kama chui waliojivika ngozi ya kondoo.

Nazani tutakubaliana sasa kuwa awamu hii imefanya unyang'anyi mchana kweupe, umepiku na kuharibu maana harisi ya utawala wa Sheria, uhuru wa raia na mhimili wa maakama umebaki kuwa chombo kipokeacho maelekezo na maamuzi.

Nchi hii siyo mali ya mtu na kinachoendelea Mungu atakijibu. Machozi ya wengi humfikia Mungu na majibu yake Huwa hayana huruma.
 
Huyu makengeza wa kiroho naye..
Ameshindwa kutatua migogoro inafukuta kanisani kwake..

Hv aliyaandka haya wakati lisu anasema atakinukisha?
 
2. Serikali iliyotaka kupinduliwa ni yetu wananchi. Si ya Rais wala chama. Umma una haki kuwajua na kuwahoji mashahidi waliotusaidia kuzuia serikali yetu isipinduliwe na huyu mhaini. Kuwaficha mashahidi ni kuwanyima haki ya kutambuliwa uzalendo wao.
Askofu kasema vyema hapa.
 
Kwa hukumu hii, Mahakama imeingia rasmi katika Orodha ya Maadui Wakubwa zaidi na wa Hatari zaidi kwa Usalama wa Umma nchini Tanzania.
Wananchi kwa Sasa wanazo Haki zote kabisa za kujichukulia Sheria Mkononi ili kujilinda na Kujihami. Mahakama siyo ya kutegemewa tena katika Upatikanaji wa HAKI zilizodhulumiwa na Wadhalimu.
 
Askofu naye kila mwezi lazima aende Burundi kumsalimia baba na mama yake
Kosa liko wapi hasa kwa yeye kwenda kusalimia Wazazi wake huko Burundi, endapo kama mdai yako haya ni ya kweli??
Amevunja Sheria gani???
Kwani kuwa Raia wa Tanzania ni lazima wazazi wako wote wawili nao wawe Raia wa Tanzania??
Unaielewa vizuri kweli Sheria ya Uraia ya Tanzania? Je, unakijua kitu kinachoitwa Uraia Tajnisi????

Usifikiri kwamba Watu wote kabisa wa kwenye Mtandao huu ni Mazumbukuku kama ulivyo wewe..Ondoa huu upuuzi wako hapa na wapelekee Wajinga wenzako huko uliko.
 
Kalamu ya Baba Askofu Mch. Dr. Kalikawe Lwakalinda Bagonza

SIYO PIGO KWA Tundu A. M. Lissu Tumepigwa Wote.

Nimesikia baadhi ya watu wanasema Tundu Lisu amepata pigo mahakamani baada ya mahakama kuamua kwamba mashahidi watakaotoa ushahidi katika kesi ya uhaini, watakuwa wa siri. Yeye hatawajua na umma hautawajua, hautawaona, na hata familia zao hazitajulikana. Hili Si pigo kwa Lisu. Ni pigo kwa mahakama na pigo kwa haki. Zingatia.

1. Tunazo mahakama tatu: Mhimili wa dola, mahakama ya umma na ya Mwenyezi Mungu. Hii ya mwisho haina rufaa na ndiyo pekee yenye mashahidi wa siri. Jaji ni Mwenyezi Mungu. Uamuzi wa leo unaigeuza mahakama ya dola kuwa ya Mungu. Haikubaliki.

2. Serikali iliyotaka kupinduliwa ni yetu wananchi. Si ya Rais wala chama. Umma una haki kuwajua na kuwahoji mashahidi waliotusaidia kuzuia serikali yetu isipinduliwe na huyu mhaini. Kuwaficha mashahidi ni kuwanyima haki ya kutambuliwa uzalendo wao.

3. Uhaini ni kosa kubwa (high crime). Mahakama huendesha kesi hizi kwa wazi na kuwaadhibu wakosaji kwa wazi ili kutoa fundisho kwa wengine. Leo tunaficha mashahidi, kuna siku tutaficha wahaini na kuwanyonga mafichoni. Haiwezekani kuipindua serikali sirini. Aliyeshauri mashahidi wa kesi hii wawe siri afutiwe matokeo ya elimu yake. Sina tatizo na Jaji aliyekubaliana na ushauri huu. Kuna kupigwa upofu feki unaoitwa “maelekezo toka kinyume cha chini”.

4. Mtuhumiwa wa uhaini ana haki zake. Moja ni kuwajua wanaomshtaki (ambao ni sisi Jamhuri), na kuwajua wanaoshuhudia uhaini wake. Kwa kuwa ni mtuhumiwa na kwa msingi wa uamuzi wa kulinda mashahidi, hata yeye angefichwa tusimjue ili ikitokea akashinda kesi, tusiendelee kumwona na kumnyanyapaa kuwa ni mhaini. Tungemwona tu baada ya kuhukukiwa. Kwa kuwa tunamjua mtuhumiwa, tuwajue mashahidi.

5. Kuingiza au kuonekana unaingiza mizengwe mahakamani ni kuifanyia uhaini mahakama yetu. Mtu mmoja aitwaye Tundu Lisu asifanywe kuwa ana nguvu na umuhimu wa kulazimisha mahakama yetu inajisiwe. Mahakama ina wajibu wa kuitetea heshima yake. Umma una haki ya kutetea uhuru wa mahakama.

6. Kutumia siasa kutatua masuala ya kisheria au kutumia sheria kutatua masuala ya kisiasa ni kufanya uchochezi na kuchonganisha siasa na sheria. Katika mwaka wa uchaguzi, ni kuwachagulia wananchi viongozi kinyume na matakwa yao. Tunaandaa uongozi wa kutawala miili badala ya mioyo. Kuna watu wengi saaana wako tayari kumchagua Rais Samia akiwa na mpinzani kuliko akiwa peke yake.

7. Yanayoonekana kupitia chaguzi ndani ya vyama ni kielelezo halisi cha hali ya nchi yetu. Huu si uchaguzi, si uchafuzi, ni urasmishaji wa rushwa katika taifa letu. Baada ya kupata viongozi kupitia mtindo huu, hatuwezi kupata kiongozi wa kupambana na rushwa. Wapi hapajafikiwa na rushwa katika taifa letu?!

8. Tuliwahi kuwa na gaidi feki. Ikiwa tumeruhusu mashahidi wawe siri
na ushahidi uwe siri, basi tutakuwa na mhaini feki. Pia tunaye kijiweni msaliti feki anayedaiwa ni mchanga katika chama chetu “kinachochukia” rushwa. Ufeki.
huu utatufanya tuone kila kitu ni feki. Nimeishaitwa Askofu feki.

Hukumu hii inasisitiza TURUDI MEZANI.
Mahakamani hakuna msaada.
Mhaini feki, hii imekaa sawa
 
Back
Top Bottom