Kakobe amfananisha babu wa Loliondo na DECI

Askofu Laizer kashasema,Askofu Kweka na Shoo as well,kwamba huyu mzee wanamjua...ana karama! Kwanini Kakobe na hawa waliopona wanataka kumislead watu? Cha kufanya ni kumtengenezea mazingira mazuri ya kutoa huduma basi!
 
Kwa nini mwingira na kakobe hawajengi shule au hospitali?fedha za fungu la 10 watakuambia wanaenda kueneza injili
 
Inawezekana ni wivu manake anawish sana yeye ndio angekuwa ameoteshwa na Mungu hili bingo.

Ninavyomjua KATORTOISE asingechaji 500 tu.

KATORTOISE hajui ni kwa nini Mungu kamchagua babu wa loliondo na sio yeye KATORTOISE.
 
Hapa kuna mgongano wa kimaslahi. Kakobe anaonyesha anahofia kupoteza rasilimali watu wakati babu yeye ile huduma ni sawa na anaitoa bure na hapokei zawadi yoyote ya mtu, jambo linalopelekea Kakobe kuhukumika nafsini mwake maana amekuwa akipokea dhamani kubwa kutoka kwa watu kama zawadi ya utumishi wake.
Inashangaza sana kuona mtumishi wa kipentekoste kama kakobe kutegemea siasa imuokoe kwenye vita vyake, serikali ile ile ya ccm aliyoipinga na kudai haina haki ya kuondosha mabango mbele ya kanisa lake, ndiyo sasa anayoipongeza na kuishauri itumie nguvu zaidi kumzuia babu asitoe dawa.
Mwisho kakobe anapaswa kutambua kuwa sii babu aliyevifuata vyombo vya habari bali ni vyombo vya habari vilivyomfuaya baada ya ushuhuda wa watu walioponywa kuamsha umati mkubwa wa watu kumfuata babu.
Babu aachwe afanye kazi ya kile alichofunuliwa na Mungu na uzuri mmoja anakifanya katika mazingira ya kirahisi sana. Bwana Yesu alizaliwa kwenye hori la ngombe na kwa familia masikini sana tofauti na mawazo ya walimwengu kwamba angezaliwa kwa mkuu fulani hivi mwenye jina kubwa.
.
 
kWANINI hawa watu wa Jamii ya Kakobe hawawezi hata kumuiga Mwalimu Mwakasege?(nadhani shule ni ishu hapa)!!

Mwakasege alikuwa na mkutano mkubwa wa injili na mahubiri hapa Arusha wiki iliyoishia jumapili 06/03/2011, wakati Misafara ya kwenda kwa Babu ndio imechachamaa sana, lakini hakuwahi kugusia kabisa huduma ya mwenzake, achilia mbali kuikandia!..

Je Kakobe angekuwa Arusha siku hizo ingekuwaje, si angevua shati kupigana?...Hekima ni lulu!
Je watu waliopona kama watarudi kanisani kwake ataweka wapi sura?
Huyu amewekeza kwenye matatizo ya binadamu, na hapendi aone wanakombolewa!
Aibu kubwa!
 
Huo ni wivu na sio kitu kingine.

Kwanza Babu anatoa dawa kwa bei ambayo ni sawa na kupewa zawadi kuashiria kwamba kweli amepewa karama hiyo na mwenyezi mungu. Pili kila anayeenda ni lazima anywee dawa hiyo pale tu anapopewa ili watu wasije wakaanza biashara ya kuchukua dawa na kwenda kuwalangua wengine.

Yeye Kakobe amewafilisi watu hususani wanawake kwa kuwadanganya wazi kabisa kwamba wapeleke pete, hereni na mikufu ya dhahabu kwake watabarikiwa, je yeye alipeleka wapi dhahabu zile? sio chanzo cha utajiri wake?

Kakobe amekuwa akiwaombea watu na kuwabariki kutokana na wingi au ukubwa wa michango yao, je kweli huyo atajiita mtumishi wa Mungu?

Amwache babu afanye kazi yake kama alivyoelekezwa. Kikubwa kwamba sisi binadamu tunaamini zaidi kwa kuona ushuhuda, so if watu wanapona babu hawezi kufananishwa na DESI. Kakobe ashindwe na alegee kabisa.
 
Huo ni wivu wa kakobe, wauminiwake wanakufa kwa njaa na magonjwa na watoto wao hawaendi shule kwa kukosa ada, yeye anatembelea nissan patrol na watoto wake wanasoma ulaya na kutibiwa hospitali kubwa, Babu saaafi, waache watu wakapate uponyaji kwa babu, kile kikombe kweli ni cha damu ya Yesu.Apuuzwe Kakobe hata jipya tena tapeli.
 
Yaani kwangu mimi Kakobe hana tofauti na yule (Kibwetere) Mganda aliyewadanganya waamini wake kuwa mwaka 2000 ni mwisho wa dunia na mwisho akawafungia ndani na kuwachoma moto kisha akatoweka. Huyo si mwingine ni Kibwetere.
 
Unajua gharama ya kumuona tu,au kununua dawa ya ulcers au sukari kwa Isaack Ndodi? Huyu mzee anataka 500. DECI nani sasa?kakobe,ndodi au babu? Kakobe chunga ulimi wako!
 
Kakobe anatamani angeoteshwa yeye na nnavyo mjua kama aliweza kuwavua dhahabu watu kanisani, angekua yeye ndo babu angepiga bingo ya kufa mtu, nadhani kila kichwa kupata kikombe ingekua si chini ya laki...kudadadeki!!
 
Yote katika yote, Simsikilizi Kakobe wala nani,
Natamani mtu aniambie ni nini kinatufanya tuamini asilimia mia moja kama ule ni ufunuo wa Kimungu??

Sina shida na uponyaji, kama mtu anakunywa na anapona na apone sana!!
Kwa sababu ulkiwa mgonjwa hata ukiambua kinyesi cha kuku ni dawa ya ugonjwa wako utakunywa tu,
kwa sababu ya shauku ya kupona.

Lakini bado sijajua vizuri, ni kitu gani hasa kinachopelekea sisi kuamini asilimia mia moja kwamba huu ni ufunuo wa Mungu aliye hai,
anayeabudiwa katika Roho na Kweli??
 
Yote katika yote, Simsikilizi Kakobe wala nani,
Natamani mtu aniambie ni nini kinatufanya tuamini asilimia mia moja kama ule ni ufunuo wa Kimungu??

Sina shida na uponyaji, kama mtu anakunywa na anapona na apone sana!!
Kwa sababu ulkiwa mgonjwa hata ukiambua kinyesi cha kuku ni dawa ya ugonjwa wako utakunywa tu,
kwa sababu ya shauku ya kupona.

Lakini bado sijajua vizuri, ni kitu gani hasa kinachopelekea sisi kuamini asilimia mia moja kwamba huu ni ufunuo wa Mungu aliye hai,
anayeabudiwa katika Roho na Kweli??
Mshiki na wewe ni kitu gani kinakupelekea wewe usiamini kua huu ufunua wa babu sio wa kutoka kwa Mungu alie hai?
 
Mshiki na wewe ni kitu gani kinakupelekea wewe usiamini kua huu ufunua wa babu sio wa kutoka kwa Mungu alie hai?

Kwa kweli kaka, mi siwezi kusema sio ufunuo wa Mungu wala siwezi kusema ni ufunuo wa Mungu kwa sababu mpaka sasa sijapata cha kunifanya nithibitishe kauli yangu kuhuso hilo.

Ila kwa sababu kuna kitu kinachoonekana kwa macho ya nyama haya, kwamba mti umechemshwa ukatumika kama dawa,
basi mi nitabaki na hili la mti uliogundulika na babu kwamba ukitumiwa unaponya basi.

Lakini kumhusisha Mungu tena kwa Jina la Yesu asilimia mia moja bado haijaniingia vizuri akilini.
Nahisi nahitaji msaada zaidi hapo.
 
Kwa kweli kaka, mi siwezi kusema sio ufunuo wa Mungu wala siwezi kusema ni ufunuo wa Mungu kwa sababu mpaka sasa sijapata cha kunifanya nithibitishe kauli yangu kuhuso hilo.

Ila kwa sababu kuna kitu kinachoonekana kwa macho ya nyama haya, kwamba mti umechemshwa ukatumika kama dawa,
basi mi nitabaki na hili la mti uliogundulika na babu kwamba ukitumiwa unaponya basi.

Lakini kumhusisha Mungu tena kwa Jina la Yesu asilimia mia moja bado haijaniingia vizuri akilini.
Nahisi nahitaji msaada zaidi hapo.
Twende pole pole mshiki, katika imani yako hiyo....kuna kitu chochote uliashaamini asilimia mia kua hii ni sababu ya Mungu baba alie hai? na kama ndio ni nini kilikufanya udhibitishe kua ama kweli huu ni muujiza kutoka kwa Mungu ninae muamini. Maana nielewavyo mimi Ku prove imani sijui kama inawezekana...!!
 
alpha na omega. anaona omega yake imefika ya babu imeanza alpha ndiyo maana anatapatapa tu kama mfa maji.. kila jambo na wakati wake zama za kaa kobe zimepita.
 
Kwa nini kuhofu kuhusu Mungu aliyemfunulia?
Kama babu angekuwa anatafuta wafuasi na kumtaka kila anayepata kikombe ashikamane nae katika imani yake kwa Mungu hapo ndio case ya kuchunguza aliyemfunulia babu ni mungu yupi. Maadamu babu hachagui dini wala rangi wala kabila la mgonjwa, bali yeye hushughulika na kumfungua mgonjwa aliyesetwa na magonjwa kwa kumweka huru na maradhi yake. Hivyo hatuna budu kujiridhia kwamba huyu ni Mungu wa yaliyo mema kwa watu wake.
.
 
Back
Top Bottom