Kakobe amfananisha babu wa Loliondo na DECI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kakobe amfananisha babu wa Loliondo na DECI

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lukansola, Mar 11, 2011.

 1. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Askofu Kakobe ameifananisha tiba ya Loliondo kwa babu na iliyokuwa taasisi feki ya DECI huku akidai imesababisha watu kuacha tiba za kuaminika za hospitali na kukimbila huko.

  Maswali yangu ni haya:
  1. Si kweli kwamba hata yeye aliwaombea watu waliokata tamaa na tiba za hospitali au amekuwa akijitangaza kuwa na uwezo wa kuombea na kutibu magonjwa sugu ?

  2. Amefanya uchunguzi ili kujiridhisha kwamba huo ni utapeli?

  3. Swali la mwisho ni kwamba: inawezekana ana wasiwasi wa idadi ya waumini wake kupungua wakikimbilia Loliondo kutesti zali?

  Naombeni mawazo yen Great Thinkers
  Nawashukuru kwa utulivu wenu>
   
 2. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Askofu Kakobe ameifananisha tiba ya Loliondo kwa babu na iliyokuwa taasisi feki ya DECI huku akidai imesababisha watu kuacha tiba za kuaminika za hospitali na kukimbila huko.

  Maswali yangu ni haya:
  1. Si kweli kwamba hata yeye aliwaombea watu waliokata tamaa na tiba za hospitali au amekuwa akijitangaza kuwa na uwezo wa kuombea na kutibu magonjwa sugu ?

  2. Amefanya uchunguzi ili kujiridhisha kwamba huo ni utapeli?

  3. Swali la mwisho ni kwamba: inawezekana ana wasiwasi wa idadi ya waumini wake kupungua wakikimbilia Loliondo kutesti zali? maana hapa kuna conflict of interest.

  SOURCE: Power Breakfast Kuperuzi na kudadis

  Naombeni mawazo yen Great Thinkers
  Nawashukuru kwa utulivu wenu>
   
 3. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  amenishangaza sana pilipili iliyopo shambani yeye inamuwashia nini......na yeye ni nani mpaka apinge hivyo......mchawi utamjua tu......watu wengine bana
   
 4. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  chuki binafsi..je anataka karama apewe yeye tu?
   
 5. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2011
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Hajiamini!
   
 6. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,257
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Ni tatizo la kufanya kanisa biashara. Unahubiri watu kuwa na imani japo yeye haamini. Ana mifano mingi kwenye biblia yake (kama ndicho kitabu anachokiamni).
  Ni yeye alietuambia kuwa umeme hautawaka kisa nyaya kupitishwa kanisani kwake.
  Ajitizame kwanza!
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Tapeli mnoooo huyu Kakobe anaona umaarufu wake unaporomoka sa ana tapatapa sasa. kwa babu ni kikombe cha uzima, kwa wale wakatoliki huwa tunaimba wimbo flani hivi unaanza TUKALE MKATE WA UZIMA NA DAMU YA UZIMAAAAA!!!! SO KWA BABU KULE KUNA KIKOMBE CHA UZIMA ILE NI DAMU YA YESU ALIYE HAI
   
 8. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ameshazoea kutapeli watu kwa mazingaombwe yake aliyosomea Nigeria, anahisi soko lake litakufa.
   
 9. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kakobe ni mmoja kati ya watu matapeli hapa nchini,yaani yupo kibishara na si kidini + mzee wa upako,wote ni wale wale tu.
   
 10. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #10
  Mar 11, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Ameona waumini wamepungua ndio maana amekasirika!
   
 11. M

  Mary Chuwa Senior Member

  #11
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli Kakobe hatambui anachokifanya yeye pekee ndiyo anajiona anamhubiri Yesu wa kweli na wengine ni manabii wa uongo ila ajue katika shamba la Bwana watenda kazi ni wachache sana na mavuno ni mengi sana,Mungu anapomuinua mtu kwa ajili ya huduma fulani siyo ajifanye wa kwanza kumtupia jiwe,
  Na katika Biblia kuna ahadi nyingi sana za Mungu juu yetu,vinywa vyetu vifanyike baraka na si laana kwa wengine alitambue hilo,na hukumu si ya mwanadamu bali Mungu,aache kupotosha watu.
  Hata mwanamke aliyevuja damu miaka kumi na miwili aliamini akishika vazi la Yesu basi damu itakoma kutoka na kweli kwa Imani alipona.
  na tunachohitaji ni watu kumjua Yesu na si kuwagombea kama bidhaa kama anavyotaka yeye.
  Amani ya Mungu Iwe na Yeye ili mwisho wa siku ajitambue
   
 12. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #12
  Mar 11, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  issue ni watu wapone....kama watu wanapona yeye chamsumbua nini?
  ni bora babu ambae hajaenda nigeria
   
 13. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #13
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jamani nilishesema watu wampuuze huyu jamaa hana lolote anaibia maskini kwa kutumia neno la mungu,akili yake ni ndogo sana,kama mtu anaweza kusema umeme hautawaka na ukawaka ana akili kweli huyo?
   
 14. TheChoji

  TheChoji JF-Expert Member

  #14
  Mar 11, 2011
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 672
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Kitu kimoja ambacho hawa wahubiri wanasahau ni kwamba, mtu kama anaumwa huwezi kamwe kumzuia kwenda kutafuta tiba! Na siku hizi watu wanataka results, na hawataacha kumiminika huko kwene results hata uwaambie nini.
   
 15. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #15
  Mar 11, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Kakobe,Ndodi wote wezi tu! Wanatumia jina la Mungu kutapeli watu! Kati ya kakobe na babu DECI nani? Akwende zake huko zama zake zinafikia mwisho!
   
 16. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #16
  Mar 11, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Huyu mzee wa Nigeria wa hajabu! DECI walikuwa wanapanda mbegu sh.500? Hata kama mchungaji angekuwa na njaa akaomba kila mtu amchangie 500 asingepata? Uyu babu hajaita chombo chochote cha habari ila watu wanaenda wenyewe. Kakobe ananunua airtime ch.10 lakini wapi!sadaka kibao,sasa analalama nini? Babu hakodi watu ili wakatoe ushuhuda,yeye anatibu tu. Abarikiwe!
   
 17. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #17
  Mar 11, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  huyu bwana ni mjinga kweli...
   
 18. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #18
  Mar 11, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Haya ndio matatizo ya kuingiza biashara makanisani.
   
 19. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #19
  Mar 11, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Hilo ndilo tatizo, ...

  1- pia lazima watu waelewe kuwa viongozi wengi wa makanisa yenye mrengo wa kipentekoste hudhani ya kuwa wao tu ndiyo wenye hati miliki ya kuzungumza na Mungu kwa kisingizio cha kuwa wao ndiyo waliookoka kwa sababu tu ya ubatizo wa maji mengi, kunena kwa lugha etc. Na inapotokea mtu wa madhehebu mengine akaonyeshwa/akafunuliwa jambo si wepesi wa kulikubali kuwa linatoka kwa Mungu. Wapentekoste wanapopaka watu mafuta, kugawa chumvi, vitambaa vya upako hakuna mprotestant anayewalalamikia, inakuwa shida pale mprotestant anapofunuliwa jambo.

  3 - Ni jambo la ajabu analinganisha jambo hili na deci (ya wapentekoste) ilhali huyu Babu hachukui pesa ya mtu bali wenye pesa wote wanaotaka kumpa kama shukrani anawaambiwa wazipeleke makanisani au misikitini kwao.

  4- Mwelezeni kakobe pia ikiwa jambo hili ni ufunuo (rhema-neno/jambo linalotolewa kwa wakati maalum), basi tiba hii itakoma kwani itakuwa imetolewa kwa situation fulani. na situation hiyo ikipita ukomo wake hufika.

  5- Na kama kakobe na watu wa design yake WANAKWAZIKA KWA SABABU TU NI MIZIZI INACHEMSHWA, WANAPASWA KUJUA KUWA MUNGU HUZUNGUMZA KUPITIA UTAMADUNI WA KILA MTU, NA KILA JAMII INA UTAMADUNI WAKE ULIO NA SURA MBILI, GIZA NA NURU-MUNGU HUZUNGUMZIA KUPITIA UTAMADUNI WA NURU. HATA YESU KRISTO ALIZUNGUMZA NA KUISHI KATIKA UTAMADUNI NURU WA KIYAHUDI. TATIZO WATU WENGI TUMEKUBALI UONGO WA WAMISHENI WAFANYABIASHARA WALIOTUKATAZA KUTUMIA MIZIZI ILI TUNUNE ASPIRINI ZAO. AMBAZO NI DAWA ZINAZOTOKANA NA MITI PIA.

  CHUKI YA KAKOBE NI KWA SABABU TU ALIYEFUNULIWA JAMBO HILI NI MLUTHERI NA SI MPENTEKOSTE KAMA YEYE AU YEYE MWENYEWE.

  JIULIZE ANGEKUWA YEYE NDIYE KAFUNULIWA HALI INGEKUWAJE PALE SAM NUJOMA ROAD. NINA UHAKIKA ANGEITISHA MKUTANO WA WAUMINI WA KANISA LAKE NCHI NZIMA WAJE DAR KWA MKUTANO MAALUM WA TIBA.
   
 20. Mkare_wenu

  Mkare_wenu JF-Expert Member

  #20
  Mar 11, 2011
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Sikutegemea mtu kama yeye anaweza kutoa tamko la kumkashifu babu ni jealo├║s isiyokuwa na maana,ana uhakika gani kwamba babu anadanganya?ni wa2 wangapi walioenda kule,inamaana wote wale ni wadanganyika?hana lolote ni maneno ya mkosaji hayo
   
Loading...