Kakobe amfananisha babu wa Loliondo na DECI

Askofu Kakobe ameifananisha tiba ya Loliondo kwa babu na iliyokuwa taasisi feki ya DECI huku akidai imesababisha watu kuacha tiba za kuaminika za hospitali na kukimbila huko.

Maswali yangu ni haya:
1. Si kweli kwamba hata yeye aliwaombea watu waliokata tamaa na tiba za hospitali au amekuwa akijitangaza kuwa na uwezo wa kuombea na kutibu magonjwa sugu ?

2. Amefanya uchunguzi ili kujiridhisha kwamba huo ni utapeli?

3. Swali la mwisho ni kwamba: inawezekana ana wasiwasi wa idadi ya waumini wake kupungua wakikimbilia Loliondo kutesti zali?

Naombeni mawazo yen Great Thinkers
Nawashukuru kwa utulivu wenu>

Hapa U-great thinking imedhihirika kuwa huwa UNACHAKACHUKA na personal interests! Halafu hata mleta thread kama akiileta kwa namna ya kuwin mawazo au michango anayotaka yeye, hatutakuwa na uwezo wa kuboresha lolote katika jamii yetu! Weka thread isiyo bias, watu wanoe bongo wachangie kitu kiuhalisia.. Ziko thread nyingi tu za aina hii.. Nashauri kabla ya kupost mtu awe analytical,na si kuongozwa na ushabiki,au maslahi binafsi.
 
ana wivu tu yeye ameponyesha wangapi? hata mawaziri wetu humkwepa, yeye alimnasa kigeu geu Mrema tu.
 
[h=1]LOLIONDO KUNATISHA[/h]
  • Posted by GLOBAL on March 10, 2011 at 9:00am


Na Mwandishi Wetu, Loliondo
Maelfu ya watu wanaomiminika kwenda kupata tiba kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapile anayedaiwa kutibu magonjwa sugu ikiwa ni pamoja na Ukimwi, wanakabiliwa na vifo kutokana na eneo la Loliondo, Arusha kuelemewa hivyo kutishia usalama wa wahitaji.

Habari kutoka eneo husika zinadai kuwa, maisha ya watu wanaofika kwa mchungaji huyo yanazidi kuwa magumu kila iitwapo leo kutokana na gharama za bidhaa kupanda huku miundombinu nayo ikiwa haitoshelezi.

"Hali inazidi kutisha hapa Loliondo kutokana na maelfu ya watu wanaomimika kila siku kuja kupata tiba kwa mchungaji huyu, bei ya bidhaa imepanda na kuwafanya wengine washindwe kupata mahitaji muhimu," alisema Thomas Katobolwa, mkazi wa eneo hilo.
BEI YA VYAKULA
Hali ya chakula imekuwa mbaya kijijini hapa kutokana na wingi wa watu na kinachopatikana kinauzwa kwa bei ya juu tofauti na siku za nyuma.

Sahani moja ya chakula inauzwa kati ya shilingi 5,000 na 10,000 huku baadhi ya watu wakishindwa kuimudu bei hiyo na kuwafanya waishi maisha ya shida wakati wakisubiri matibabu.

Kutokana na kukaa muda mrefu bila kukutana na mchungaji huyo, baadhi ya watu wameishiwa fedha hivyo kuwa katika wakati mgumu kimaisha.

HOFU YA MAGONJWA YA MILIPUKO
Licha ya watu kumiminika kupata tiba ya magonjwa sugu yanayowasumbua, kuna uwezekano wa kuibuka kwa ugonjwa wa kipindupindu kutokana na kukosa sehemu maalum ya kujisaidia.

Aidha, wingi wa watu wanaozidi kwenda kwa mchungaji huyo wakati hakuna miundombinu kama vile maji safi na salama, vyoo na huduma nyingine za kiafya wanaweza kukumbwa na maradhi ya milipuko kama vile Kipindupindi.

Tayari watu watano wameripotiwa kufariki dunia eneo hilo kutokana na maradhi mbalimbali lakini wachunguzi wa mambo ya kijamii wanasema vifo hivyo vinaweza kuongezeka kutokana na mateso wanayopata wagonjwa njiani.

Inadaiwa kuwa, baadhi ya wahalifu wanatumia vibaya ‘chansi' hiyo kufanya vitendo viovu na kuwaliza watu.
Huku hayo yakiendelea huko Loliondo, Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zachary Kakobe ameangusha maombi mazito ya kupambana na kazi alizoziita za kishetani.

Alisema kuwa, mtu pekee anayeweza kumponya mwanadamu ni Mungu pekee kupitia jina la Yesu.

Inaelezwa kuwa, zaidi ya watu 300,000 wamekwenda kwa mchungaji huyo kwa siku, hali ambayo imesababisha bei ya nauli kupanda maradufu
 
Sumaye atinga Loliondo
Send to a friend
Thursday, 17 March 2011 22:52
Waandishi Wetu
sumaye1.jpg




















WAKATI mamia ya watu wakiendelea kumiminika kupata tiba ya dawa ya magonjwa sugu kwa mchungaji wa KKKT katika Kijiji cha Samunge, Wilayani Loliondo, jana ilikuwa zamu ya Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye kupata kikombe cha babu huyo.

Hatua ya Sumaye ni mwendelezo wa uwazi kwa viongozi wanaokwenda Samunge siku za karibuni tofauti na awali ambao baadhi ya vigogo walidaiwa kwenda kupata tiba hiyo kwa kificho.Lakini, kama ilivyokuwa kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa ambaye alifika Samunge, Loliondo siku tatu zilizopita na kunywa kikombe cha Babu, jana Sumaye naye alifika kijijini hapo kunywa kikombe hicho.

Akiongozana na watu kumi wa familia yake, Sumaye alifika kijijini Samunge saa 7 mchana ambapo alipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Loliondo, Elias Wawalali ambaye kwa kutumia njia maalumu ya viongozi alipelekwa moja kwa moja kwa Mchungaji Mwasapile na kunywa dawa hiyo.

Kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wanaofika kijijini Samunge kunywa dawa hiyo ya maajabu kwa mchungaji Mwasapile ambaye alisema kuwa anatoa tiba hiyo baada ya kuoteshwa na Mungu.

Mchungaji Loliondo awajibu Kakobe, MwingiraKatika hatua nyingine, Mchungaji huyo jana alivunja ukimya na kuwajibu baadhi ya viongozi wa dini waliomtuhumu kuwa tiba anayotoa ni ya nguvu za giza akisema kuwa waliotoa tuhuma hizo wana mtazamo wa kifedha zaidi na siyo imani.

Miongoni mwa viongozi ambao walitoa matamshi makali dhidi ya Mchungaji Mwasapile, ni Askofu Zakary Kakobe wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) na Nabii Josephat Mwingira wa Kanisa la Efata ambao walikaririwa na vyombo vya habari wakituhumu tiba hiyo kwamba ni ya nguvu za giza.

Lakini, jana Mchungaji Mwasapile alisema,"..Hao (Kakobe na Mwingira) hawapo kiimani, wana mtazamo wa kifedha zaidi.

Ninachowaomba, wasiwazuie wengine kuja kupata tiba na wao wakitaka waje kupata tiba hii."Alisema viongozi hao na watu wengine wasifikirie kuwa yeye anatoa tiba hiyo ili kutafuta sifa binafsi, kwa madhehebu, dini au kikundi fulani cha watu bali kwa ajili ya utukufu wa Mungu.

Mchungaji huyo pia alitoa tahadhari akiwataka watu kutowatorosha wagonjwa hospitalini kwa ajili ya kuwapeleka kwake wakiwa mahututi.Aliwataka wananchi wajihadhari na utapeli ulioibuka kwa baadhi ya watu kuwa wana dawa hiyo akisisitiza kuwa tiba yake ameoteshwa na Mungu na hakuna yeyote anayetoa bali yeye.

Wakati huo huo, Chama cha Waganga na Wakunga wa Tiba Asilia Tanzania (Chawatiata), kimedai kushangazwa na viongozi wa Serikali kupanga foleni mchana kweupe kupata huduma ya dawa kwa Mchungaji Ambikilile Mwasapile wakati wanapoenda kwa waganga wengine wa kienyeji, huenda kwa kujificha.

Kauli hiyo imekuja, siku chache baada ya vigogo wengi serikalini kwenda kwa mchungaji huyo maarufu kwa jina la 'Babu' wakiwamo Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustino Mrema na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa. Dawa ya mchungaji huyo imejizolea umaarufu wa kutibu magonjwa sugu kiasi cha kuwafanya hata wagonjwa kutoka nje ya nchi kuja nchini kutibiwa.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi Katibu Mkuu wa Chawatiata, Mittam Magombeka alisema waganga wa tiba asilia wamekuwa wakidharauliwa na hata kuonekana kuwa ni aibu kupata tiba kwao.Jambo hilo alisema limekuwa likiwafanya baadhi ya wale wanaoamini tiba hizo kwenda kwao kwa siri ili wasionekane na watu.Habari hii imeandaliwa na Musa Juma, Elizabethy Suleyman, Exuper Kachenje


 
[h=2]Friday, March 18, 2011[/h] [h=3]Babu Loliondo awajibu akina Kakobe na Mwingira [/h]
images



Mchungaji huyo jana alivunja ukimya na kuwajibu baadhi ya viongozi wa dini waliomtuhumu kuwa tiba anayotoa ni ya nguvu za giza akisema kuwa waliotoa tuhuma hizo wana mtazamo wa kifedha zaidi na siyo imani. Miongoni mwa viongozi ambao walitoa matamshi makali dhidi ya Mchungaji Mwasapile, ni Askofu Zakary Kakobe wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) na Nabii Josephat Mwingira wa Kanisa la Efata ambao walikaririwa na vyombo vya habari wakituhumu tiba hiyo kwamba ni ya nguvu za giza. Lakini, jana Mchungaji Mwasapile alisema,"..Hao (Kakobe na Mwingira) hawapo kiimani, wana mtazamo wa kifedha zaidi. Ninachowaomba, wasiwazuie wengine kuja kupata tiba na wao wakitaka waje kupata tiba hii."Alisema viongozi hao na watu wengine wasifikirie kuwa yeye anatoa tiba hiyo ili kutafuta sifa binafsi, kwa madhehebu, dini au kikundi fulani cha watu bali kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
 
Mbona mnaumia sana wakuu! Kakobe kawambia facts! BABU NAYE NI TAPELI! mpende msipende huo ndio ukweli! hakuna uthibitisho wowote kwa mtu aliyepata tiba ya BABU na kupona. Mambo na story nyingine ni fixation tu! watanzania wengi ni wajinga na wanapoambiwa ukweli huwa hawakubali kwa kuwa wana imani za kijinga!
 
[h=2]Babu Wa Loliondo Alikuwa Mgonjwa Wa Akili[/h]
Mobhare Matinyi: " Huenda Babu Wa Loliondo Alikuwa Mgonjwa Wa Akili"

Submitted by Mjengwa on 1.1.12


Maggid,

Uko sahihi kabisa.

Huyu Babu alikuwa janga kwa taifa letu na anapaswa kulaaniwa vikali na watu wote wenye akili timamu. Uwezekano mkubwa ni kwa Babu wa Loliondo kuwa na tatizo la akili ambalo halikujitokeza kwa namna tuliyozoea - ile kupiga kelele na kuvua nguo. Huyu babu labda ni mgonjwa akili aliyejikita katika imani za kimiungu.

Watanzania, kutokana na ujinga wetu, umaskini wetu, na maradhi yetu, tulimpa fursa ambayo hakustahili. Taifa lenye watu zaidi ya 60% wanaoamini ushirikina, asilimia 40% wasiojua kusoma na kuandika, 35% wanaoishi katika umaskini uliokithiri, na viongozi wengi wanaoshinda kwa waganga, watu wanaofikiri kuwa unene tipwatipwa na ulevi ni afya, ni lazima mtu kama Babu angeonekana shujaa kwetu.

Dawa za Babu zilielezwa na wazee wa Kisonjo kwamba ni za kawaida, na zinatibu magonjwa kadhaa likiwemo kisukari, lakini kwa ujinga wetu watu wakawa wanakunywa kikombe kimoja kwa kudhani imani za kimiujiza zitawasaidia. Wale mababu hawakunywa vikombe vya Babu na bado wanaendelea kuzitumia bila shida kila wakiumwa. Mababu wasiojua kusoma na kuandika wanatushinda akili watu tuliokwenda shule. Dawa zile zimefanyiwa utafiti duniani na zikaonekana kuwa na uwezo wa kufanya kazi fulani, hivyo, ukinywa kikombe kimoja unaweza kupata nafuu lakini hutapona kwa sababu hukunywa kitaalam. Unafuu huu ndio uliowapa wajinga imani kwa Babu anaponya.

Babu hakuwa na utumishi wa uungu wowote wala utabibu wowote. Huenda ni mgonjwa wa akili na ni kweli amekuwa janga la kitaifa. Aibu na fedheha kwa taifa letu.

Mobhare Matinyi.

 
Tiba ya Loliondo yamtisha Kakobe Send to a friend
Monday, 07 March 2011 12:00


kakobe.jpg













Mussa Juma, Loliondo na Nora Damian
WAKATI idadi kubwa ya wagonjwa wakionekana kumzidi nguvu mchungaji mstaafu, Ambilikile Mwasapile, Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe ameingia hofu ya kupoteza waamini kufuatia taarifa kwamba mchungaji huyo anatibu Ukimwi.

Jana akihubiri katika kanisa lake lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam, Askofu Kakobe alisema uwepo wa mchungaji Mwasapile unatishia vituo vya maombezi vinavyofurika mijini kubaki vitupu kutokana na watu kukimbilia Loliondo.
Habari kutoka Loliondo zinasema wakati watu wakiendelea kufurika nyumbani kwa mchungaji huyo ili kupata matibabu, mamia ya watu wengine wamekwama jijini Arusha na katika eneo la Mto wa Mbu kutokana na kukosa usafiri wa kuweza kuwafikisha nyumbani kwa mchungaji Mwasapile.
Mwasapile(76) ni mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) na Inadaiwa kuwa anatibu magonjwa sugu ukiwemo Ukimwi.
Mwananchi lilishuhudia mamia ya watu katika maeneo kadhaa ya jiji la Arusha na mji wa Mto wa Mbu kwenye barabara inayoelekea Samunge kupitia Engaruka na Ngaresero umbali wa takriban kilometa 400 toka Arusha mjini.
Taarifa zinasema kuzidi kuongezeka kwa idadi hiyo kumechangiwa na baadhi ya ndugu za wagonjwa wa HIV, Saratani, Kisukari na pumu waliokuwa wamelazwa katika hospitali mbali mbali nchini, kuwaondoa wagonjwa hao na kuwapeleka kwa mchungaji huyo.
Hali za baadhi ya wagonjwa zimeelezwa kuwa ni mbaya na wengine bado wamekwama njiani ambapo hadi jana vilikuwa vimeripotiwa vifo vya watu wawiliambao walifikishwa Loliondo kwa lengo la kupatiwa tiba.
Mwandishi wa Mwananchi alishuhudia idadi kubwa ya magari yakifika kwa mchungaji huyo, huku wagonjwa wakiwa kwenye magodoro na wengine wakiwa hawajitambui kutokana na maradhi.
Hali hiyo pia inachangiwa na masharti ya dawa hiyo, ambapo mchungaji Mwasapile anasema, hairuhusiwi kusafirishwa na ni yeye pekee kwa mkono wake akikupa ndipo utapona.

Uhaba wa Magari
Mbali na uhaba wa magari, pia gharama za magari ya kukodi na mabasi zimepanda.
Magari ya kukodi kwenda na kurudi kijiji cha Samunge wilayani Ngorongoro, alipo mchungaji huyo imefikia kati ya Sh100,000 na Sh150,000 kwa mtu mmoja huku nauli za mabasi zikiwa ni kati ya Sh50,000 na Sh80,000.
Bei ya magari ya kukodi siku tatu ziliyopita ilikuwa ni kati ya Sh50,000 hadi 80,000 ambapo mabasi ya kawaida nauli ilikuwa ni kati ya Sh14,000 hadi 20,000.

Watu kuongezeka
Mchungaji Mwasapile alisema juzi kuwa idadi ya watu watakaofika kupata tiba inatarjiwa kuongezeka na kwamba ameoteshwa kuwa watu watatoka mabara mbalimbali na kwamba itamchukuwa mwezi mmoja mtu mmoja kupata tiba.
Dalili za hali hiyo, zimeanza kujidhihirisha kwani tofauti na awali ambapo kwenda kupata dawa na kurudi ilikuwa ni safari ya siku moja, hivi sasa maelfu ya watu kutoka mikoa mbali mbali nchini, wapo kwa mchungaji huyo kwa zaidi ya siku tano na hawajafanikiwa kupata tiba.
Mchungaji Mwasapile anadai kuwa alioteshwa na Mungu kuhusu dawa hiyo inayotokana na mti aina ya Mugariga ambao ni chakula maarufu cha Twiga, tangu mwaka 1991 lakini alisubiri hadi mwaka jana alipoanza rasmi kutoa tiba.
Alitahadharisha watu wenye virusi HIV ambao watakaokunywa dawa hiyo na kupona kujikinga na maambukizi mapya, kwa kuwa mgonjwa haruhusiwi kunywa dawa hiyo mara mbili.
"Wanaopona HIV waache kujiingiza katika matendo ya kupata maambuki kwani hawatapona tena...; Hii dawa sio kinga ni tiba na hairuhusiwi kunywa zaidi ya kikombe kimoja,"alisema Mchungaji Mwasapile.
Msaidizi wa mchungaji huyo, Marko Nedula alisema kuwa watu wengi wanaofika kupata huduma kwa mchungaji huyo wanatoka nje ya wilaya ya Ngorongoro hasa kutokana na wenyeji kudharau awali.
"Hawa wanaoleta vurugu leo hapa, mchungaji aliwambia siku nyingi njooni mpate tiba lakini walidharau,"alisema Nedula.

FFU waongezwa
Kutokana na maelfu ya watu kufika katika kijiji hicho kupata tiba jeshi la polisi mkoani Arusha, limelazimika kuongeza askari wa kutuliza ghasia(FFU) katika eneo la mchungaji huyo.
Askari hao, wamekuwa wakisimamia na kupanga watu ili kupata tiba na kuimarisha ulinzi katika kijiji hicho, ambacho hakina huduma za kulala, vyoo, hoteli wala umeme.
Akizungumzia hali ya sasa Loliondo, Mkurugenzi wa kampuni ya kukodi magari ya Sanufa , Said Kakiva aliomba serikali kuingia kati suala hilo kwa kupeleka mahema eneo la tiba na kukarabati barabara.
"Mimi magari yangu yote yamekodishwa kupeleka wagonjwa, kwa huyo babu, lakini, barabara ni mbaya sana na kule hakuna huduma zozote muhimu kama mahala pa kulala na chakula,"alisema Kakiva.
Alisema suala la matibabu ya magonjwa sugu Lilondo serikali inaweza kulifanya ni sehemu ya kutangaza utalii kwani, watu wa mataifa mengi wanafika kupata tiba ambayo inatokana na miti ya asili ya Tanzania.
"Serikali itengeneze sasa barabara, kwani barabara hii ndiyo iliahidiwa lami na rais na inakwenda hadi mkoani Mara,"alisema Kakiva.

Hofu ya Askofu Kakobe
Askofu Kakobe alisema Watanzania wengi wanapenda uwongo kuliko ukweli na kutahadharisha kuwa kutokana na kuwepo mtu huyo watu hawatasubiri tena maombezi bali watapukutika kwenda Loliondo."Hofu yangu iko katika vituo vya maombezi vilivyofurika mjini, wakati huu vitabaki tupu, watu wataenda Loliondo na hawatasubiri tena maombezi,"alisema Kakobe na kuongeza :

"Tukisema tusubiri serikali ama TFDA ituthibitishie itakuwa ngumu maana kila mmoja anatia bidii kama polisi na wengine".Alisema kanisa lake litaendelea kuwepo na kamwe haliwezi kutikiswa na Loliondo na kujigamba kuwa wanaweza kumsambaratisha mchungaji huyo.
Kakobe alieleza kuwa kwake yuko muhubiri wa Injili iliyo hai na ambayo iko ndani ya Biblia huku akikumbusha mtu aliyemwita 'Babu wa Tegeta' ambaye alijitokeza miaka ya nyuma na kudai kuwa anatibu Ukimwi ambaye alisema walimsambaratisha.Kakobe ambaye alitumia muda mwingi kunukuu vifungu mbalimbali vya Biblia, alisema mfumo wa uponyaji wa Mungu umeshafunuliwa na kwamba kwa sasa hawahitaji Mungu yeyote atoe ndoto.
"Hizi ni nyakati za mwisho, unatakiwa kuchagua kanisa ambalo utaongozwa katika haki na si kupeperushwa kama karatasi,"alisema Kakobe huku akishangiliwa na waumini wake.Aliwatahadharisha waumini wake akiwataka kuwa makini na mchungaji huyo huku akimtuhumu kwa kudai kuwa anatumia nguvu za giza.
"Kama umesikia mtu fulani anafanya maombezi la kwanza la kujiuliza je ameokoka kwa sababu Mungu hatendi kazi na watu ambao hawajaokoka, lazima awe anahubiri Injili,"alisema.Askofu huyo alitumia ibada hiyo kuwahamasisha waumini wake kumpinga mchungaji huyo kwa maombi huku akitamka:
"Kanyaga Babu wa Loliondo, sambaratisha babu wa Loliondo, kazi za babu saga."Kakobe alikwenda mbali zaidi na kumfananisha mchungaji huyo na mganga wa kienyeji huku akijigamba kuwa hata kanisani kwake watu waliokuwa na Ukimwi walipona."Tusibabaishwe na Ukimwi, hapa tumeombea watu wamepona Ukimwi na vithibitisho vya vyeti vipo,"alisema Kakobe na kushangiliwa na waumini wake ambao baadhi yao walisikika wakisema, "tupo."
Kakobe alisema hata kama mtu huyo angekuwa anatibu kwa Sh1 kwenye Neno la Mungu haikubaliki na kueleza kuwa maandiko yanasema, 'mmepewa bure toeni bure.'Katika hatua nyingine, askofu Kakobe alisema matatizo ya umeme nchini hayataisha hadi waziri wa Nishati na Madini aende akatubu kanisani kwake.Alisema mambo yanayojitokeza sasa ni matokeo ya yale waliyoyafanya Tanesco kanisani kwake na kutaka Ngeleja akatubu ili matatizo yaishe.

 
Askofu Kakobe ameifananisha tiba ya Loliondo kwa babu na iliyokuwa taasisi feki ya DECI huku akidai imesababisha watu kuacha tiba za kuaminika za hospitali na kukimbila huko.

Maswali yangu ni haya:
1. Si kweli kwamba hata yeye aliwaombea watu waliokata tamaa na tiba za hospitali au amekuwa akijitangaza kuwa na uwezo wa kuombea na kutibu magonjwa sugu ?

2. Amefanya uchunguzi ili kujiridhisha kwamba huo ni utapeli?

3. Swali la mwisho ni kwamba: inawezekana ana wasiwasi wa idadi ya waumini wake kupungua wakikimbilia Loliondo kutesti zali? maana hapa kuna conflict of interest.

SOURCE: Power Breakfast Kuperuzi na kudadis

Naombeni mawazo yen Great Thinkers
Nawashukuru kwa utulivu wenu>


Kuna usemi unasema "NYANI HAONI KUNDULE". Anachofanya yeye cha kuwaaminisha watu kwamba yeye anauwezo wa kimungu wakati sio kweli hakioni isipokuwa anaona ya wenzake. Ana wivu na hofu ya kukosa waumini na hivyo kukosa fedha anazozikusanya kitapeli
 
Kuna usemi unasema "NYANI HAONI KUNDULE". Anachofanya yeye cha kuwaaminisha watu kwamba yeye anauwezo wa kimungu wakati sio kweli hakioni isipokuwa anaona ya wenzake. Ana wivu na hofu ya kukosa waumini na hivyo kukosa fedha anazozikusanya kitapeli
Bw Majid Mjengwa anachuki gani na Babu au wewe una chuki binafsi na Kakobe???.Hoja hapa ni Kwamba kabla ya Babu kuwa Janga la Kitaifa Kakobe alionya , lakini wewe na wenzako hukusikia, leo Babu ni janga la Kitaifa lakini wewe bado huoni hivyo , nilitegemea ujibu , hali ya Babu ya sasa , je si tapeli??

Pia kama una ushahidi Kuwa Askofu Kakobe ni tapeli weka Ushahidi hapa tuona kama kama watu walivoweka ushahidi wa Babu Loliondo !!! Vinginevyo wewe si great thika bali ni mshabiki wa Waganga wa kienyeji!!

Tueleze Babu hajaleta maafa ??. Au wewe ni kuwadi wa Babu???
Pia tueleze Askofu kakobe kakutapeli nini kabla ya kuweka humu ili tuchangie!!!
Kama anakusanya pesa kwa utapeli kwa nini serikali haijachukua hatua ???
 
Askofu Kakobe ameifananisha tiba ya Loliondo kwa babu na iliyokuwa taasisi feki ya DECI huku akidai imesababisha watu kuacha tiba za kuaminika za hospitali na kukimbila huko.

Maswali yangu ni haya:
1. Si kweli kwamba hata yeye aliwaombea watu waliokata tamaa na tiba za hospitali au amekuwa akijitangaza kuwa na uwezo wa kuombea na kutibu magonjwa sugu ?

2. Amefanya uchunguzi ili kujiridhisha kwamba huo ni utapeli?

3. Swali la mwisho ni kwamba: inawezekana ana wasiwasi wa idadi ya waumini wake kupungua wakikimbilia Loliondo kutesti zali?

Naombeni mawazo yen Great Thinkers
Nawashukuru kwa utulivu wenu>

Wewe Lukansola bilashaka unamaswali ya ajabu,
kwanza hujui mambo ya Mungu kwa ufasaha ndo maana unalopola kuwa waliombewa waliokata tamaa na hospital, afu unadakia mambo kwa juu, "amekuwa akijitangaza kuwa na uwezo wa kuombea na kutibu magonjwa sugu" wewe tangu lini ulisikia akitangaza kuwa anatibu na kuponya? mwenzio huwa anamtangaza Bwana Yesu na sio yeye kuwa anatibu na kuponya. sasa acha upuuzi wa kupotosha uma wa watanzania kama hunachakuzungumza si ukaekimya, kwani lazima uandike?

kweli inaonekana ufatiliji wako wa habari ni mfinyu, Lostam Azizi alitamkaga azarani kuwa alimpeleka ndugu yake kukandamiza kikombe lakini amna kitu, na sio huyo tu fatilia walioenda wakwambie. nakama unatumia akili vizuri embu jiulize nani alierudi na kufanya vipimo na kuonesha hadharani kuwa kipimo cha mwanzo kilikuwa hivi na sasa ni amepona subutu!

Kuhusu idada ya waumini, Kakobe ni askofu na mchungaji wa tofauti sana, kama ulishafanya uchunguzi ukaingia kanisani kwake ndio utajua kuwa habembelezi waumini bali anawafundisha masomo magumu kiasi cha wale wafuasi wa mkumbo wanaondoka wenyewe, kipindi fulani alirushaga mafundisho ya mawigi, na mengine mbona wa TZ walihenya.

sasa kwataarifa yako huyu jamaa huwa anafundisha neno la Mungu ktk biblia bila kupindisha kushoto au kulia na huwa nasema kabisa kama uwezi milango iko wazi; waulize waliobaatika kuingia ndio watakwambia bana, achakuropoka.

Nakushauri achana kabisa na kumzungumza mtumishi wa Mungu kama huyu ambae haangalii sura ya mtu; unadhani ukisema hivyo ndio atajikomba komba? kwajinsi navyomfaham unachemsha tu, fanya biashara nyingine bana hata ya kuuza karanga inalipa, kama hunamtaji tafuta ajira wapo watu wanaweza kabisa kukuajiri kuuza karagara.
 
Kwani watu wana amini Ushirikina kuliko Mungu?.Hata waislam utakuta wanatoka Msikitini kuswali halafu nje ya Msikiti mizizi
 
Badala ya serikali kulipa posho za Madaktari Mhimbili wanakwenda Kuimalisha Tiba ya Kishirikina Loliondo!
 
Askofu Kakobe ameifananisha tiba ya Loliondo kwa babu na iliyokuwa taasisi feki ya DECI huku akidai imesababisha watu kuacha tiba za kuaminika za hospitali na kukimbila huko.

Maswali yangu ni haya:
1. Si kweli kwamba hata yeye aliwaombea watu waliokata tamaa na tiba za hospitali au amekuwa akijitangaza kuwa na uwezo wa kuombea na kutibu magonjwa sugu ?

2. Amefanya uchunguzi ili kujiridhisha kwamba huo ni utapeli?

3. Swali la mwisho ni kwamba: inawezekana ana wasiwasi wa idadi ya waumini wake kupungua wakikimbilia Loliondo kutesti zali?

Naombeni mawazo yen Great Thinkers
Nawashukuru kwa utulivu wenu>
Mkuu hivi haya maswali ni wewe kweli uliuliza??
 
Wewe Lukansola bilashaka unamaswali ya ajabu,
kwanza hujui mambo ya Mungu kwa ufasaha ndo maana unalopola kuwa waliombewa waliokata tamaa na hospital, afu unadakia mambo kwa juu, "amekuwa akijitangaza kuwa na uwezo wa kuombea na kutibu magonjwa sugu" wewe tangu lini ulisikia akitangaza kuwa anatibu na kuponya? mwenzio huwa anamtangaza Bwana Yesu na sio yeye kuwa anatibu na kuponya. sasa acha upuuzi wa kupotosha uma wa watanzania kama hunachakuzungumza si ukaekimya, kwani lazima uandike?

kweli inaonekana ufatiliji wako wa habari ni mfinyu, Lostam Azizi alitamkaga azarani kuwa alimpeleka ndugu yake kukandamiza kikombe lakini amna kitu, na sio huyo tu fatilia walioenda wakwambie. nakama unatumia akili vizuri embu jiulize nani alierudi na kufanya vipimo na kuonesha hadharani kuwa kipimo cha mwanzo kilikuwa hivi na sasa ni amepona subutu!

Kuhusu idada ya waumini, Kakobe ni askofu na mchungaji wa tofauti sana, kama ulishafanya uchunguzi ukaingia kanisani kwake ndio utajua kuwa habembelezi waumini bali anawafundisha masomo magumu kiasi cha wale wafuasi wa mkumbo wanaondoka wenyewe, kipindi fulani alirushaga mafundisho ya mawigi, na mengine mbona wa TZ walihenya.

sasa kwataarifa yako huyu jamaa huwa anafundisha neno la Mungu ktk biblia bila kupindisha kushoto au kulia na huwa nasema kabisa kama uwezi milango iko wazi; waulize waliobaatika kuingia ndio watakwambia bana, achakuropoka.

Nakushauri achana kabisa na kumzungumza mtumishi wa Mungu kama huyu ambae haangalii sura ya mtu; unadhani ukisema hivyo ndio atajikomba komba? kwajinsi navyomfaham unachemsha tu, fanya biashara nyingine bana hata ya kuuza karanga inalipa, kama hunamtaji tafuta ajira wapo watu wanaweza kabisa kukuajiri kuuza karagara.



Mkuu nashukuru kwa ushauri wako, lakini punguza ukali kidogo bwana daah.
 
Back
Top Bottom