Family business: Mke wa kamshika masikio kaka, anazidi kuingiza ndugu zake, ndio mwanzo wa hostile takeover ??

gearbox

JF-Expert Member
Apr 20, 2024
564
1,650
kuna family business ya close relatives naona inakoelekea sio kuzuri and i am so concerned, Binafsi nimepewa huu mkasa na moja wanafamilia ila nikaona mawazo yangu pekee yanaweza yasitoshe.

OK ipo hivi....

Inatokea mna family business mliachiwa na wazazi muisimamie.

Kaka mwenye nafasi kubwa kwenye maamuzi ana mke ambae kamshika sana masikio.

Mwanzoni aliingiza ndugu yake dereva mtoto wa mjomba wake, akaja kumuingiza muhasibu mtoto wa baba mdogo, kuna nafasi mbili nyingine anataka aingize ndugu zake wawili wa ziada kwenye ofisi ya tawi la mkoa mwengine, kuna mdogo wake na mtoto wa shangazi yake -nafasi hizo ni meneja wa tawi na muhasibu.

Naanza kuona kwanini ni ngumu kufanya family business kwetu waafrika
 
hapana usikubali huo ujinga, mtapigwa sijui mlie na nani, maana wakifanya chochote cha hasara kesi itapotezwa kifamilia na huo ndo mwisho wa biashara. hutakuwa na nguvu hata ya kuwakemea na lazima wataiba tuu.
 
Aliyewafundisha kwamba umshirikishe Mke wako mambo yako (biashara, mshahara, kile unachofikiria,n.k) aliwaharibu sana. Sisi Wazee wenu hatukuwa na huo ujinga.

Wanawake wengi ni ma-Delilah. Muda wote wanaweza kumuangusha Samson kwa mbinu tata sana. Kaka yenu ameshaangushwa tayari. Endeleeni na tabia ya kuwashirikisha wake zetu mambo yenu yote mpoteze kila kitu.
 
wewe ni ndugu wa mbali sana na hiyo familia pamoja na biashara yao?...kama ni ndugu wa karibu then you should act direct mana kuandika huku sio solution sana.
 
hapana usikubali huo ujinga, mtapigwa sijui mlie na nani, maana wakifanya chochote cha hasara kesi itapotezwa kifamilia na huo ndo mwisho wa biashara. hutakuwa na nguvu hata ya kuwakemea na lazima wataiba tuu.
Na si ajabu mpaka ipo siku ndugu wa huyo shemeji yako pamoja na yeye mwenyewe wata declare kwamba biashara ni yao.
 
Au pengine nyie ndugu wa huyo kaka enu wengi wenu ni mabogus katika swala zima la uendeshaji wa biashara ndo mana kaona bora aweke mashemeji zake?
 
Hii scenario ipoje wakuu ? kuna family business ya close relatives naona inakoelekea inaweza kuwa dissolved, Lakini najua humu JF kuna mawazo tele.

Inatokea mna family business mliachiwa na wazazi muisimamie.

Kaka mwenye nafasi kubwa kwenye maamuzi ana mke ambae kamshika sana masikio.

Mwanzoni aliingiza ndugu yake dereva mtoto wa mjomba wake, akaja kumuingiza muhasibu mtoto wa baba mdogo, kuna nafasi mbili nyingine anataka aingize ndugu zake wawili wa ziada kwenye ofisi ya tawi la mkoa mwengine, kuna mdogo wake na mtoto wa shangazi yake -nafasi hizo ni meneja wa tawi na muhasibu.

Naanza kuona kwanini ni ngumu kufanya family business kwetu waafrika
Cha msingi kaka yako hatakiwi kumu involve mke wake kwenye mambo ya familia yenu, kaka yenu anawazamisha mazima ombeni nae kikao muwekeane misingi ya biashara na miiko ,hapo amewakosea sana
 
Mkuu c km kaka mtu Hana mtu ktk familia yake ambaye anaelimu yakukidhi vigezo vinavyotakiwa ktk ofisi wanazomilikii ss watawekwa wakafanye nn,unakuta kaka mtu ndio tu ana akili madogo n pasua kichwa ,hvyo shemeji Yao kashaliona hlo anawaweka ndugu zake wenye elimu🤪🤪🤪
 
Hivi mmewahi kuyafatilia maisha ya yule Mlowezi wa Kiingereza Lord Delamere niliyejiitia jina lake? Alikuwa na misimamo ambayo ambayo imefanya mali zake zidumu kizazi na kizazi. Misimamo ambayo Waafrika wengi hatuna.

Kuna familia kubwa tajiri duniani za Rockefellers na Rothschilds . Hizi familia zina utajiri wa toka karne nyingi sana. Moja ya siri yao ni; wana family unity ya kiwango cha juu sana, halafu mgeni anayeingia ndani ya familia kwa kuolewa au kuoa hahusishwi moja kwa moja kwenye family business.

Sasa nyinyi endeleeni kushirikisha kila kitu wageni wanaoingia kwenye familia yenu.
 
Hivi kuna mmewahi kuyafatilia maisha ya yule Mlowezi wa Kiingereza Lord Delamere niliyejiitia jina lake? Alikuwa na misimamo ambayo ambayo imefanya mali zake zidumu kizazi na kizazi. Misimamo ambayo Waafrika wengi hatuna.

Kuna familia kubwa tajiri duniani za Rockefellers na Rothschilds . Hizi familia zina utajiri wa toka karne nyingi sana. Moja ya siri yao ni; wana family unity ya kiwango cha juu sana, halafu mgeni anayeingia ndani ya familia kwa kuolewa au kuoa hahusishwi moja kwa moja kwenye family business.

Sasa nyinyi endeleeni kushirikisha kila kitu wageni wanaoingia kwenye familia yenu.
Nimeipenda hii

Vile vile nilijifunza kwamba hawa matajiri huwa hawawaingizi watoto wao katika biashara bila kujifunza kutoka hatua ya mwanzo,,,mpaka wanakuja kushika nafasi za juu basi ujue wanajua system nzima ya kampuni jinsi inavyofanya kazi

Huwezi kuwadanganya kitu,,badala yake sisi wafrika tunapeana tu nafasi kwakuwa ni ndugu bila ujuzi wala uzoefu wowote ule,,ndio maana huwa tunafeli sana
 
kuna family business ya close relatives naona inakoelekea sio kuzuri and i am so concerned, Binafsi nimepewa huu mkasa na moja wanafamilia ila nikaona mawazo yangu pekee yanaweza yasitoshe.

OK ipo hivi....

Inatokea mna family business mliachiwa na wazazi muisimamie.

Kaka mwenye nafasi kubwa kwenye maamuzi ana mke ambae kamshika sana masikio.

Mwanzoni aliingiza ndugu yake dereva mtoto wa mjomba wake, akaja kumuingiza muhasibu mtoto wa baba mdogo, kuna nafasi mbili nyingine anataka aingize ndugu zake wawili wa ziada kwenye ofisi ya tawi la mkoa mwengine, kuna mdogo wake na mtoto wa shangazi yake -nafasi hizo ni meneja wa tawi na muhasibu.

Naanza kuona kwanini ni ngumu kufanya family business kwetu waafrika
Duuu huyo brother ibidi apigwe chini kwenye vikao vya familia au ni Bora wavunje biashara Kila mtu afe na chake kuliko kushuhudia anguko kwa sababu ya boya mmoja katika familia
 
Family Matters

images (1) (7).jpeg
 
Back
Top Bottom