Kaka yangu na mkewe wananikwaza.

Wameoana kwa ndoa ya Kikristo na kubahatika kupata watoto wawili, wote wa kike.
Tatizo ni kwamba mtoto mmoja yuko upande wa kiumeni na mwingine upande wa kikeni.
Pia baba na mama licha ya kuwa wana nyumba ya familia, kila mmoja ameikimbia na kwenda kupanga jirani na nyumba yao.
Na kibaya zaidi ukiwauliza habari za utengano wao wanakuwa wakali kuliko mwiba wa mbasa, sijui sisi kama ndugu tufanye nini ili kuinusuru ndoa hii.?

Kwa nini wewe uwauliza-ulize kuhusu maisha yao? Lazima wawe wakali, unamfuata kaka yako mpaka chumbani kwake?!!
 
Wameoana kwa ndoa ya Kikristo na kubahatika kupata watoto wawili, wote wa kike.
Tatizo ni kwamba mtoto mmoja yuko upande wa kiumeni na mwingine upande wa kikeni.
Pia baba na mama licha ya kuwa wana nyumba ya familia, kila mmoja ameikimbia na kwenda kupanga jirani na nyumba yao.
Na kibaya zaidi ukiwauliza habari za utengano wao wanakuwa wakali kuliko mwiba wa mbasa, sijui sisi kama ndugu tufanye nini ili kuinusuru ndoa hii.?

Hao achana nao, walikofika ni mbali sana!, ujue mpaka hapo na watoto wamegawana!, imebaki kuuza nyumba kila mtu achukue chake. Ila kama kweli ni kaka yako, lazima unajua zaidi ya hayo uliyosema!, chanzo utakua unakijua tu, na kama ni kweli hujui lolote, basi huna sifa ya kuwa mshauri wao, kaa kimya!

Wazazi wao wapo?, wajomba na mashangazi wapo?, hawayaoni?, bila shaka walishashindwa!,

walikubaliana kuowana na inavyoonekana wamekubaliana kuachana!, achana naooo!.
 
wanahitaji maombi makali ya kufunga kabisa. Kuna li roho li chafu linawafanya watengane.
Washauri waende kwenye maombi mapema kabla hawajachelewa. Shetani mbaya sana.
 
Ufuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu! kujua undani wa hilo itahitajika kazi kubwa mkuu. Kadiri muda unavyoenda utajua tu, kwani mmojawapo ataamua kufunguka. Kwa sasa waache wapoe kwanza kaka
 
Back
Top Bottom