Kaka yangu ananichukia

LDA COMPANY

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
303
570
Za leo ndugu zangu, natumai mko poa kabisa.

Kuna jambo limekuwa linanitatiza kwenye maisha yangu nalo ni chuki aliyonayo kaka yangu juu yangu.

Hili jambo nimekosa wa kumshirikisha ikabidi nililete hapa jukwaani kuna watu wanaweza kunisaidia.

Huyu kaka yangu kaanza zamani kunichukia toka tupo wadogo mpaka alipomaliza chuo na kupata kazi hajawahi kunisaidia kitu chochote .

Mwanzo nilidhani labda ana mambo mengi hivyo kipato hakitoshi ila nikaona mbona anasaidia watu wengine lakini mimi nikimuomba chochote ansema hana kitu. Mpaka naanza masomo yangu ya chuo namaliza bro hakuwahi kunisaidia chochote na nilikuwa nasoma chuo Dar es salaam, hata sehemu nilipokuwa napanga hakuwahi kuja.

Ila kwa watu wengine ambao hawana undugu nae safi tu anwatembelea na kuwasaidia wanapokwama.

Huyu bro ameoa ila alikuwa ananiponda Sana kwa shemeji yangu hata ndugu zake na shemeji. Hii hali imekuwa inaninyima amani japo chuo nilishamaliza na ndio napambana na maisha yawe mtaani ila huyu ndugu yangu anaonekana kunichukia sana.

Kuna kipindi alinipita njiani kama hanijui na mimi ikabidi nimkaushie. Nyumbani tupo watoto sita ila huyu ni kaka yetu mkubwa najiuliza kwa nini ana chuki sana namna hiyo.
 
Natamani nikugawie misimamo yangu

Mtu akionesha kunichukia basi nakaa nae mbali sana, akinikaribia kinafiki Nampa drama za kumfanya akae mbali na mimi.

Unadhani ukilalamika ndio atakupenda? Upo tayari kupewa upendo wa kinafiki?
 
Achna nae huyo, mchukulie kama sio ndugu yako... We unaona kabisa mtu anakuchukia bado unaendelea kujikomba komba mpaka kufungua thread? Jitambue kumbavu ww
 
Natamani nikugawie misimamo yangu

Mtu akionesha kunichukia basi nakaa nae mbali sana, akinikaribia kinafiki Nampa drama za kumfanya akae mbali na mimi.

Unadhani ukilalamika ndio atakupenda? Upo tayari kupewa upendo wa kinafiki?
Nimekuelewa mkuu
 
Kuna watu huwa tunatunza kumbukumbu hata za zaman,yawezakuwa zaman mkiwa wadogo uliwah mfanyia kitu kilichomkaa mpaka leo
 
Back
Top Bottom