suala si binti MREMBO au MSOMI, ukweli uliopo ni kwamba kutokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha(life style) ,dada zetu BAADHI yao au pengine WENGI WAO hawajui kupika na ni wavivu katika kazi za nyumbani. na hili si kosa lao kutojua kupika ila ni mabadiliko ya mfumo wa maisha. binti anaanza chekechea(baby class) mpaka chuo yupo BWENI tu, na akija likizo anakuwa ametingwa na masomo ya ziada, akirudi nyumbani giza limeingia. Je atajifunza kupika saa ngapi? halafu shule za bweni za siku hizi si kama zile za nyakati zetu ambapo elimu ya kujitegemea(self reliance) ilipewa kipaumbele....ni shule za kusoma madesa tu, nyingine mpaka vitanda wanafunzi wanatandikiwa na kina mama wanaofanya usafi mabwenini. binti anakuwa hajui hata kutandika kitanda.
Pia kuna mabinti hawasomi bweni wako shule za kutwa lakini kwa changamoto ya mji kama Dsm binti anatoka nyumbani saa kumi alfajiri,akitoka shule anapita masomo ya ziada.hiyo ni jioni tayari anakwenda kugombania daladala, akifika nyumbani saa mbili tayari kila kitu kimeshapikwa.
NINI KIFANYIKE. wazazi pamoja na changamoto zilizopo za kimaisha lakini ni LAZIMA wahakikishe mabinti wawapo nyumbani hata kama ni kwa likizo ya wiki moja basi wawe wanawajibika ipasavyo kujua yale yanayowahusu wao kama kina dada. Ni aibu kwa mwanamke kutojua kupika au akawa mvivu kupindukia kwa sababu tu hakuzoea kufanya hizi kazi. kwa upande wa mabinti wenyewe nao wajielewe na wawe na ari ya kujifunza. wakiwa na nia hasa,kupika si kugumu,ni suala tu la kuwa na INTEREST nalo basiiiii!. ikiwa binti hujui kupika na unaridhika kabisa hujui na huoneshi juhudi,je watoto wako watakuwaje? halafu maisha yanabadilika,mabinti wasitegemee kuwa watakuwa na uwezo wa kuwalipa madada wa nyumbani kila siku....kuna wakati maisha yanakuwa magumu na hata hiyo hela ya kumlipa house girl usiipate....things do change!!