Kaka na Dada hawa...Mhh!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,725
Hii ishu imetokea live!

Nina majirani zangu ambao nyumba zetu zinatazamana hapa Uswahilini!

Kumetokea kituko cha mwaka ndani ya familia yao!

Kuna mabinti wawili wakubwa wa nyumba hiyo ambao walishaolewa na wana watoto, ambapo pia watoto hao ni wakubwa!

Ilitokea hali ambapo mtoto wa dada mkubwa (mvulana), na mtoto wa dada mdogo (msichana ) walikuja hapo jirani kwa bibi yao, lakini katika hatua ya ajabu, wakaanzisha mambo ya mapenzi, wakatundikana mimba , na binti amejifungua mtoto wa kakake, na walipoulizwa walikubali jambo hilo bila ya shaka wala kurefusha maneno!

Wazazi wa pande zote mbili wamewasusa watoto hao hapo kwa bibi yao, na hawajapita kuwatazama toka ishu hiyo itokee!

Je hali kama hii watai`handle namna gani hawa jirani zangu?
 
Last edited:
hii ishu imetokea live!

Nina majirani zangu ambao nyumba zetu zinatazamana hapa uswahilini!

Kumetokea kituko cha mwaka ndani ya familia yao!

Kuna mabinti wawili wakubwa wa nyumba hiyo ambao walishaolewa na wana watoto, ambapo pia watoto hao ni wakubwa!

Ilitokea hali ambapo mtoto wa dada mkubwa (mvulana), na mtoto wa dada mdogo (msichana ) walikuja hapo jirani kwa bibi yao, lakini katika hatua ya ajabu, wakaanzisha mambo ya mapenzi, wakatundikana mimba , na binti amejifungua mtoto wa kakake, na walipoulizwa walikubali jambo hilo bila ya shaka wala kurefusha maneno!

Wazazi wa pande zote mbili wamewasusa watoto hao hapo kwa bibi yao, na hawajapita kuwatazama toka ishu hiyo itokee!

Je hali kama hii watai`handle namna gani hawa jirani zangu?
sasa kaka wewe ulitaka waume maneno wakati ni kweli walifanya uasherati huo, kwa ujumla ni aibu kwa wao wenyewe na familia zao.
 
Umesahau kule Moshi hivi juzi kijana aitwae BARAKA kamtia mimba dadake waliochangia baba mmoja na kisha kumpa maji ya betri yaliyochanganywa na mwarobaini ili atoe hiyo mimba na kuishia kuiona ahera?Baraka anatafutwa na polisi,yaani hata kaskazini mambo haya yameenea mi nilidhani wao ni biashara na siasa tuu kumbe makubwa haya!
 
Wakuonea huruma ni hao watoto ambao hawana hatia wala makosa yoyote. Watoto ambao watakua na kujua kua baba na mama yao ni kaka na dada. Ndiyo mwanzo wa kua na matatizo ya kisaikologia. Watawaeleza vipi hao watoto?

Hao kaka na dada inabidi wakapimwe akili kusema ukweli. Kama wamefikia umri wa kuweza kumpa na kupata mimba basi ni lazima wawe wanajua kufanya mapenzi kati ya kaka na dada na dhambi kubwa sana.Walicho fanya ni very selfish maana hawa kufikiria kitendo chao kita leta madhara gani.
 
Haya mambo kwa kweli yanasikitisha sana. Nilisoma na binti mmoja ambaye alikuwa bomba sana. Nadhani mama yake ama waliachana na baba yake au alifariki (sikumbuki vizuri) na walikuwa wakiishi Regent. Basi Mzee kila akipita huku na huko na kumuangalia binti yake alivyoumbika akaamua kufanya unyama wake wa kumtaka binti yake. Basi unyama wa yule Baba dhidi ya binti yake hatimaye wakapata mtoto ambaye alizaliwa taahira. Kuna umuhimu wa kuwa na sheria za kuwafungulia mashtaka wazazi (kwa maoni yangu hawastahili kuwa wazazi) kama hawa.
 
Last edited:
Nawapa pole wazazi wa watoto hawa! lakini kukimbia tatizo sio utatuzi wa tatizo, kuwasusa hakuwasaidii hao wazazi wala watoto wakosefu. Wajaribu kuwa consult wazee wa jadi wa kabila lao huenda ufumbuzi ukapatikana.
 
Mkuu specify. Unapo wapa pole wazazi wa watoto hawa una wapa pole hao kaka na dada au wazazi wa hao kaka na dada?Maana hapo juu kuna two sets of parents na it's not clear una wapa pole wapi.
 
Haya mambo kwa kweli yanasikitisha sana. Nilisoma na binti mmoja ambaye alikuwa bomba sana. Nadhani mama yake ama waliachana na baba yake au alifariki (sikumbuki viziuri) na walikuwa wakiishi Regent. Basi Mzee kila akipita huku na huko na kumuangalia binti yake alivyoumbika akaamua kufanya unyama wake wa kumtaka binti yake. Basi unyama wa yule Baba dhidi ya binti yake hatimaye wakapata mtoto ambaye alizaliwa taahira. Kuna umuhimu wa kuwa na sheria za kuwafungulia mashtaka wazazi (kwa maoni yangu hawastahili kuwa wazazi) kama hawa.

Tatizo sidhani kama hata sheria zita zuia baadhi ya watu kufanya mambo haya. Kwa sababu mimi I doubt the mental capacity ya watu wanao fikia kufanya mambo kama haya. Mtu mpaka afikie kufanya mapenzi na binti wake, mzazi wake au kaka/dada yake basi huyo mtu ni atakua na matatizo makubwa sana. Je sheria zita zuia watu wenye akili hizi kufanya hivyo?
 
Mwanafaslafa1, Ni kweli sheria haziwezi kuzuia matukio kama haya ya kinyama lakini angalau zinaweza kusaidia kuyapunguza kwa wahusika kuogopa athari za unyama wao.

Tuna sheria za kuwaadhibu wezi, majambazi ambazo pamoja na kuwa hazijazuia matukio zaidi ya ujambazi na wizi angalau labda zimesaidia katika kupunguza idadi ya matukio hayo.
 
In some cultures they would have been banished from the area and home OR even killed.
Incest is abominable and not good for the human race survival.
In-breeding leads to the weak and recessive genes come and manifest themselves.

Do not be surprised that this happens alot more than reported. Some cases are hushed up to protect the family reputation.

All in all it is sad and traumatising.
 
Tatizo sidhani kama hata sheria zita zuia baadhi ya watu kufanya mambo haya. Kwa sababu mimi I doubt the mental capacity ya watu wanao fikia kufanya mambo kama haya. Mtu mpaka afikie kufanya mapenzi na binti wake, mzazi wake au kaka/dada yake basi huyo mtu ni atakua na matatizo makubwa sana. Je sheria zita zuia watu wenye akili hizi kufanya hivyo?
Nadhani anatoa pole kwa grandpa, katika context yoyote huo ni uashereti. Zipo jamii na imani zinakubali mahusiano ya hivyo mf Waarabu. Mtoto wa mkubwa anaweza kuolewa si kuzini na mtoto wa mdogo ila hakuna jamii inayokubali (kwa uelewa wangu baba mmoja na mama mmoja, au waliochangia wazazi) kuona. Kama nipo sahihi hao kaka na dada hawajachangia wazazi bali wazazi wao ni ndugu. Otherwise turefushe mada kwa wale wenye mahusiano na binamu zao inakuwaje???
 
Ni kweli mkuu kuna mila zina ruhusu kuoana mabinamu. Ila kwa reaction ya familia ya hao kaka na dada ni dhahiri ni kitu kisicho ruhusiwa kwao. Sema that also brings up hiyo issue uliyo sema wewe. Je ni uasherati mtu na binamu yake kuzaa?
 
Mwanafaslafa1, Ni kweli sheria haziwezi kuzuia matukio kama haya ya kinyama lakini angalau zinaweza kusaidia kuyapunguza kwa wahusika kuogopa athari za unyama wao.

Tuna sheria za kuwaadhibu wezi, majambazi ambazo pamoja na kuwa hazijazuia matukio zaidi ya ujambazi na wizi angalau labda zimesaidia katika kupunguza idadi ya matukio hayo.

I understand you mkuu. Na kama ni hivyo wana stahiri adhabu kali kama za ubakaji na ulawiti.
 
I understand you mkuu. Na kama ni hivyo wana stahiri adhabu kali kama za ubakaji na ulawiti.
Mie ninachoona hao wazazi si kwamba wamewasusa watoto bali wanaona aibu. Hivi kuna tofauti gani gani na mabinamu wanaooana? Maana wale wazazi ni kaka na dada, hawa wazazi ni dada na dada. Bado tu kidhungu ni uncles na aunt. Nadhani tuijadili hii kwenye context ya kibinam na tukubaliane kabisa hata binamu wanaokuwa na mahusiano au wameoana wanafanya makosa. Otherwise wapo right isipokuwa tu WAMEFANYA UZINIFU
 
Msiwe na haraka hivo kuhukumu kuna jamii nyingi tu duniani binamu wanaoana,nimeona Comoro na Indonesia.Nasikia hata Ufaransa ni poa tu.
 
Msiwe na haraka hivo kuhukumu kuna jamii nyingi tu duniani binamu wanaoana,nimeona Comoro na Indonesia.Nasikia hata Ufaransa ni poa tu.
It is true lakini utayari wa kuyakubali yaliyotokea ndio unahitajika. Though kama ulivyosema jamii nyingi na si ya hao yalipotekea. Busara inahitajika.
 
Msiwe na haraka hivo kuhukumu kuna jamii nyingi tu duniani binamu wanaoana,nimeona Comoro na Indonesia.Nasikia hata Ufaransa ni poa tu.
Ni kweli mambo haya yanategemea utamaduni wa watu/jamii. Waarabu na huko ulikokuonesha mabinadamu wanahusiana bila shida hata kufunga ndoa. Lakini tukubai pia kwa jamii/makabila mengi tanzania yanaweka umbali mkubwa katika mahusiano ya kujamiiana. Kwa jamii nyingi mabinamu kujamiiana ni kosa kubwa na la aibu. Halikubaliki. Hii ikiwa pia ni kwa sababu za kiafya. Watu waliokaribu mno kwa damu (undugu) kuna hatari ya kuzaa watoto wakiwa na matatizo ya afya: ulemavu, utaahira, nk.

Kwa mawazo yangu kigezo cha makatazo yaha isiwe tamaduni za wenzetu (Indonesia, nk) bali tamaduni zetu. Tusiseme kwa kuwa kule wanafanya hivi basi nasi tufanye hivyo.

Kisa hiki kinanikumbusha jamaa moja aliyekwenda Vietnamu kwa masomo kwa miaka mingi. Aliporudi akawa anataka kumchumbia dada yake wa kwa baba mdogo. Ukoo haukumuelewa. Alipoitwa na ukoo na kuulizwa kulikoni, jamaa akasema: "kwani nini cha ajabu mbona Vietnam wanaoana tu". Wazee wakashangaa na kumwambia hayo ya Vietnam ni yake tu asiyalete huku. Utamaduni wao hauruhusu hayo. Ikabidi jamaa atulie tu.
 
Well zipo jamii za Kitanzania hata binamu si Tatizo. Ninaamini kama sijakosea naomba nisahishwe hata waislam, wanaruhusu ndoa ya hao jamaa, pia na sheria ya kujamiiana ya Tz hailitaji hilo kama kosa. Kuhusu maradhi hao wanaooana wenyewe kwa wenyewe, sual la maradhi ni sehem ya sababu yao kuu. Kwamba wanaona ukioa nje unaweza kuleta maradhi kwenye familia Mf maradhi ya kurithi. Lakini pia wanaamini wanashikamana zaidi. kwahiyo suala la ulemavu nk na hayo pia ni imani. Nadhani suala hili linaweza kuwa sahihi kutegemeana na context yenyewe
 
Back
Top Bottom