Kumbe ipo sathili nyingine ya "Kaka Jambazi" zaidi ya ile ya BWABWA?...Kweli hii inji chipoko!.Hatukawii kusahau matatizo kwa kuwa tumezaliwa na huruma kuliko "YESU MNAZARETI!"
Tulipoanza tu awamu ya Nne, kelele zilikuwa nyingi sana kuwa chama tawala kimetumia fedha nyingi za umma kwenye kampeni, tukapigwa na changa la macho la "MABILIONI YA JK" ambayo yalipelekea kwa wanyonge kwa staili ya aina yake, yakapelekea kuanzishwa kwa " SACCOS" hewa zenye mfumo tofauti na zile za kawaida za kiushirika, ambazo zilipelekea wajanja "KUKOPA KABLA YA KUWEKA na hatujui sasa kama wamerejesha na uhai wa SACOSS hizo upoje sasa . Wote tupo kimya, hakuna ajue hatima ya hizo fedha za umma zimeipatia jamii faida gani kwa kuwa zilitolewa kwa kivuli cha jina lililojema la Mheshimiwa mwenyewe.
Hatukuweza kuhoji DSA alizotumia mzee wa "RICHI MONDULI" na wapambe wake waliokwenda kutafuta "mvua ya kutengeneza" kule Thailand, na mvua yenyewe isionekane mapka kesho...
Hatujahoji ni vipi "tutafidiwa kwa fedha zilizopotea kwenye ulaghai wa wazi wa RICHMOND na DOWANS kupitia malipo ya gharama za uwezo wa genereta (Capacity charges) ambazo zimetoka na umeme haukuonekana? Tuliambiwa Serikali yetu inalishighulikia na hatima yake imefika kikomo, mjadala umefungwa sasa!....
BEA wamekubalui kurejesha chenji taslimu bila riba. Tumekubali na kuanza kujisifia "kwa hili tumefanikisha" fedha zitaenda kwenye miradi ya maendeleo (hatutaki tena rada wala zana za kijeshi).
Kagoda, MEREMETA na wenzake wamerejesha zile za EPA, tukasema ziende kwenye KILIMO na hapo hapo Mafedhuli wa EPA wakaja na aandiko la Kimradi kwa jina la "KILIMO KWANZA" kwa kivuli cha "MAPINDUZI YA KIJANI (Green Revolution) ambao unahitaji mabilioni ya shilingi ambazo haziwezi kumfikia mkulima zaidi ya hao wabwenyenye!...