Kajenga katika kiwanja cha mwanamke kinachomtokea utamhurumia

Kajenga katika kiwanja cha mwanamke kinachomtokea utamhurumia

Mshauri jamaa avunje nyumba ataambulia hata mbao na bati akauzia tunaojenga mabanda ya kuku.
Chumba kimoja kinamtosha yeye kwa Sasa.
Mishe mishe atapata hela ya Kodi.
Yaani unaondoka na kila kitu na kuacha uwanja mtupu
Anachofanya Sasa hivi Ni ujinga na upumbavu.
Ndio maana mimi huwa nasema, mwanaume jijali mwenyewe na jali ndugu zako.
Haya mambo ya kujifanya "najenga familia yangu" hujui hata kuwa uko na adui yako ndani.
Sure kabisa navunja nyumba nasepa na vyangu tuone Kama huyo mwanamke ataleta hao wanaume ndani
 
Bado nasisitiza Abomoe nyumba achukue tofali zake,mbao zake,bati zake,madirisha yake na baadhi ya milango yake atajua cha kufanya hapo baadae. Halafu tuone huyo mpumbavu kama atajenga yakwake ..Ila anavyoendelea kuwa mpole yani ndo anampa kiburi huyo mwanamke. Wanaume hatupogo hivyoo
 
. Huu ni wakati ambao huwezi kumkumbuka mama yako mzazi kwamba ndio mwema zaidi kwako zaidi yake

Tupate wadhamini
20190923_165353.jpg
 
Aendelee kumkomesha hivyo hivyo na akiendelea kukaa nae hiyo mwanamke IPO cku atamkata mapumb*

Kwan unamng'angani ni mama yako
 
Sheria inasema hivi Mali za wanandoa ni zile zilizochumwa pamoja au alikuwa nayo mwenza mmoja kabla ya ndoa then baadae ya kuoana mwenza mwingine akashiriki kuitunza au kuiendeleza basi Mali hiyo inakuwa ya wote. Hivyo mshauri huyo mwenzako aende mahakama ya mwanzo afungue kesi ya kuvunja ndoa baada ya hapo mgao utapita hawezi kupoteza haki yake.
 
Imenikumbusha kaka yangu mmoja (kwa sasa ni marehemu),alikutana na janga kama hilo,alijenga nyumba ya zaidi ya milioni 60 kwenye kiwanja cha mkewe, mke akaanza visa na kumtaka bro waachane,brother akashauri nyumba iuzwe wagawane pesa,(tena nusu kwa nusu) mke akakataa,brother akamwambia shem "naondoka na tofali zangu nakuachia kiwanja" shem akajua utani,akamwambia "beba" bro akakaa kimya!

Shem alisafiri kwenda kwao ndani ya wiki moja,aliporudi akakuta nyumba haipo,(bro aliivunja hata tofali za level ya msingi,zilichimbwa,akaenda kuweka kwenye kiwanja chake kingine halafu yeye na watoto wake akaenda kupanga chumba na sebule,akaanza kujenga mdogo mdogo,baada ya mwaka mmoja shem alianza kumuomba msamaha bro kwa mengi aliyomkosea,hakutaka hata kumuona,wazee walimsihi amsamehe walee watoto wao lakini hakuwahi kuwaelewa...

Mpaka leo shem ni mtu wa kutanga tanga tu,kiwanja chake mpaka leo hakina nyumba kwa sababu hana uwezo wa kukijenga!
Kidume hicho
 
Jamaa ni mpumbavu yeye na mke wake!
Hapo kama ni mimi, mke analeta wanaume ndani,
Mimi kila siku naleta wadada "visu" balaa.
Naleta watoto "non stop"
Nikipumzika sana labda mara moja kwa wiki.
Kwanza mwanamke anakuzidi vipi akili mpaka kufikia hatua hizo?
Huenda wanaume tunatofautiana sana.
Wengine ni kama mabinti.

Hauoni kama utakuwa unashiriki kwenye ujinga wa mtu mwingine na kupoteza muda ambao ungeweza kujijenga?
Ukajiweka sehemu nzuri mpaka huyo mwanamke akikuona anasikia aibu?
 
Huyo rafiki yako mwambie awe kidume basi agangamale yuko legelege sana

Hizo sperm nini nini hizo zisimfanye zezeta wanaume wengi tu wanalea watoto wasio wao bila wao kujua

Huyo malaya kajitia jeuri basi huyo rafikiyo nae akachukue bati na tofali zake akaanze upya,, asijiue please please bado wapo wanawake watakaomtunza na kumthamini
 
Jamaa ni mpumbavu yeye na mke wake!
Hapo kama ni mimi, mke analeta wanaume ndani,
Mimi kila siku naleta wadada "visu" balaa.
Naleta watoto "non stop"
Nikipumzika sana labda mara moja kwa wiki.
Kwanza mwanamke anakuzidi vipi akili mpaka kufikia hatua hizo?
Huenda wanaume tunatofautiana sana.
Wengine ni kama mabinti.

cheka sana. Kejeli sana ila omba mungu yasikukute.
 
Back
Top Bottom