Kaja kuomba samahani bila aibu

Kaja kuomba samahani bila aibu

Asabaya

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2012
Posts
1,310
Reaction score
418
Hali zenu wana MMU?

Kuna jambo nashindwa kulielewa, mdogo wangu aliolewa na jamaa ambae hata kazi alikua hana tukamsaidia kumpa mtaji mpaka mambo yake yakawa sawa, alipopata vijisenti akamjeuri kupita kiasi, na muchepuko ndio usiseme.

Yote haikutukera, akapata mwanamke ndio jeuri ikazidi, ikafikia mpaka anampiga mdogo wetu. Kwakweli hapo ustahmilivu ulinishinda, nikakwambia mdogo wangu huyu jamaa ni limbukeni na atakutoa roho bora ufanye maarifa uondoke.

Kabla hata hajajipanga kuondoka jamaa alikuja na mwanamke ndani ya nyumba alopewa zawadi mdogo wetu na Dad siku ya harusi, yule jamaa bila kujali alimfukuza mdogo wetu na kumwambia mie nakupa talaka na sitokurudia wewe labda nilale na mamangu.

Basi mdogo wetu amerudi nyumbani tukamuondoa kwenda Arabuni mwenyezi mungu kamjalia amepata mume anaolewa soon inshallah, huyu bwana sasa fimbo ya mungu imempiga huyo mwanamke alomchukua ni wale wanawake wa type za wadada wa kutunzana; sijui leo kuna kigodoro wapi wanakwenda, mara sare imepita, kwa ufupi jamaa hanaa amerudi kuliko alivyokua mwanzo, na mwanamke kamfukuza.

Cha kushangaza bila aibu jana amekuja nyumbani na kilio tulijua amefiwa kwao, tunashuka chini haya alichojia nini, ooh nimekuja kumrudia mke wangu, mimi ilikua sio akili yangu nilirogwa.

Hivi waungwana, kwa makosa aloyafanya huyu bwana anawezaje kuja kusema nataka kumrejea mke wangu? Wenye ujuzi na mambo kama haya ebu watuambie kama mliwahi kupitia wasohaya kama hawa.
 
arabuni mwenyezi mungu kamjalia amepata mume
Mke wa pili sikai wa tatu ntakaa!!!

Started by Asabaya, 16th September 2012 16:15
[SUB]naana mdogo wangu ameolewa nchi nje
[/SUB]eleweka.Jee waungwana nimekosea kumueleza hayo? Manake ananambia wewe unaona rahisi tuu sababu hayaja kukuta.
Nimeona nije tena hapa kwenye wengi yupo japo mmoja ataweza kunipa jawabu la hekma.....
Kwakweli inaniuma nataka kumsaidia mdogo wangu....[/quote]
...huu mchanganyo wa font mhm!!!
 
Kisirani sana bwana yule ametuchokoa roho zatu vyakutosha.
Labda amejifunza kweli na yuko tayari kumrejea mkewe,lakini kama huyo mwenzie yuko tayari kuoa na mdogo wako hamtaki kweli basi mwelezeni kua rizki imekwisha akajitafutie huko kimanzichana.
 
Mwambie huyo mwanaume aishie hapohapo!!!!!!!!!!!!!!!!!!! asimletee mabalaa binti wa watu. tena mumuulize amaisha lala na mama yake????????????
 
Labda amejifunza kweli na yuko tayari kumrejea mkewe,lakini kama huyo mwenzie yuko tayari kuoa na mdogo wako hamtaki kweli basi mwelezeni kua rizki imekwisha akajitafutie huko kimanzichana.

Shosti hajifunzi yule mshezi wa tabia sana,unaweza kuamini mdogo wetu anakuja nyumbani kuna harusi ya kaka yetu anaoa anakuja na mwanamke mwengine anasema sheria wanne kama si jeuri yakikwao nini.. naende afike......
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom