Kairuki: Walimu wa sanaa hawataajiriwa

Kairuki: Walimu wa sanaa hawataajiriwa

Hhhhhahhaahha zile ajira elf90 za mwaka unaisha zilipotelea wapi?
na sasa ndio kabisaaa elf52 ni utapeli wa mchana nilidhan kwenye 53 walim watakuwa elfu40
 
Hapa ni kudai katiba mpya na tume huru. CCM itoke madarakani. Hatuwataki
Ivi aliyesema kuwa kila aliyesoma ataajiriwa ni nan?? mm nimehitimu chuo miaka minne sasa na ajira yangu kuuza mihogo na maisha yanaenda mbona?? sasa nyinyi mnataka serikali ijaze watu huko hata kma wamejaa ili tuwalipe na kodi zetu?? hebu tuwen serious bhana
 
Eti hii nchi ndio watu wanategemea itakuwa kwenye uchumi wa kati miaka kadhaa ijayo!
 
Kama mwaka wa fedha 2016/2017 ajira zilikuwa elfu 90 na hazikuonekana hata kwa tochi, itakuwaje kwa mwaka huu wa fedha hizo elfu 50 si itabidi utambikie mizimu ndo uzione.
Daaah hahahahahahahaha
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki amefunguka na kusema serikali kwa sasa haitaweza kuajiri walimu wapya wa sanaa bali itawatumia walimu wa sanaa wa ziada waliopo katika shule za sekondari.


Waziri Angela KairukiAngela Kairuki amesema hayo leo bungeni na kudai kila shule itaweza kupata walimu wa sanaa kulingana na mahitaji yao

"Utafiti uliofanywa na Ofisi ya Rais Tamisemi mwaka 2015/2016 umebaini kuwepo kwa ziada ya walimu wa masomo ya sanaa wapatao 7463 katika shule za sekondari, kutokana na hali hii serikali inaendelea na zoezi la kuwagawanya walimu hao au kuwa 'redeploy' kwa kuzingatia uwiano na mahitaji halisi ya walimu wa sanaa kwa kila mamlaka za serikali za mitaa ili kila shule iweze kupata walimu wa masomo ya sanaa badala ya kuajiri walimu wapya"

-alisema Angela Kairuki Mbali na hilo Waziri Kairuki amesema serikali inaendelea kuajiri watumishi wa kada mbalimbali ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 watumishi zaidi ya elfu tisa wameajiriwa serikalini.


"Katika mwaka wa fedha 2016/17 jumla ya watumishi wa Umma 90721 wamekwisha ajiriwa kwa kuzingatia vipaumbele na mahitaji ya kila mwajiri na katika mwaka wa fedha 2017/18 serikali inatarajia kuajiri watumishi 52436 wa sekta mbalimbali kwa kuzingatia vipaumbele vya taifa pamoja na kuimarisha kila sekta na upungufu mkubwa wa watumishi wa Umma"

-alisema Kairuki



Chanzo : EATV

Ubaguzi huo
 
wp_ss_20170530_0008.png
 
Mengi ya kukarahisha na kuvunja moyo tutayasikia awamu hii
 
Acheni mbwembwe nyie serkal ya Magu, tatzo lenu mnaanzsha hl kabla hamjalmalza mnarukia lile, duh,!!Atari kwelkwel, swala la vyet feki mshaliweka kapuni baada ya kuwapluni watumish wa tamisemi et, achane double standard nyie mbona mashirka ya uma mmeyaacha, kueni basi na dira yan mnatuchanganya wananch ad tunashndwa tufate lp, ama kwel Dereva wa lorry naona yuko spd mbaya hatak shka brek
 
du majanga..ngja nitafute mchumba aliemaliza arts nioe bila mahali..then nimpeleke akalime shamba mana hamna namna...broo kagoma kuajil
 
Na wabiashara pia hawataajiri?maana hata masomo ya biashara kunaupungufu sana.
 
Back
Top Bottom