Kairuki: Walimu wa sanaa hawataajiriwa

Kairuki: Walimu wa sanaa hawataajiriwa

Ngoja namba kila mtu aisome ili tupate akili 2020
 
Duh
Mungu ni wa ajabu sana maana ni kama niliota nikaitosa A level nikawahi kutafuta kazi yaani huwa naufurahia uamuzi wangu mara 100 maana sasa kwa ajira hizi lazima magonjwa yasiyotibika yatawamaliza vijana wetu hasa wale wapenda starehe.
 
Duh hii sasa kali basi bora Serikali iwasamehe walimu wa sanaa ambao wamesomeshwa na Loan Board maana sidhani kama watamudu kulipa madeni yao ambayo nmeambia hayapungui chini ya Mil.10
 
Pole zao, ila iwe fundisho kwa Hawa nyoka walioko secondary wanao endekeza mapenzi na kukimbia Sayansi japo hata hio sayansi nayo baadae itakua mule mule

Wanafunzi hawakimbii sayansi ila mazingira mabovu ndio yanafanya wanafunzi wasisome masomo ya sayansi.

unakuta shule ina walimu wawili wa kemia na mmoja wa biology amabo wanatakiwa wafundishe form I-IV na hakuna mwalimu wa hesabu wala fizikia, Ndio maana wanafunzi wanaishia kusoma Kiswahili na History.

Serikali inalala mwisho wa siku inafanya maamuzi ya kukurupuka yanayoumiza watoto wa masikini, walihamasisha watu wasome ualimu kwa kuwahakikishia kupata mikopo hata wale wenye division three, wakahamasisha vyuo vingi kufundisha ualimu wakaongeza vyuo vya ualimu mfano DUCE na MUCE, leo watoto wa masikini wamehitimu kutoka kwenye hivyo vyuo Serikali inawatupa.

Kipaumbele cha serikali yetu leo ni kujenga uwanja wa ndege Chattle na kununua panga boi.

Serikali Mungu anawaona mjue.
 
Hivi yeye alisoma masomo gani? Kulingana na taaaluma yake
 
Na wabiashara pia hawataajiri?maana hata masomo ya biashara kunaupungufu sana.
biashara nayo ni arts hakuna ajira,tena hao ndo kabisaaaa wakajiajiri kwa taaluma ya biashara waliyonayo
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki amefunguka na kusema serikali kwa sasa haitaweza kuajiri walimu wapya wa sanaa bali itawatumia walimu wa sanaa wa ziada waliopo katika shule za sekondari.


Waziri Angela KairukiAngela Kairuki amesema hayo leo bungeni na kudai kila shule itaweza kupata walimu wa sanaa kulingana na mahitaji yao

"Utafiti uliofanywa na Ofisi ya Rais Tamisemi mwaka 2015/2016 umebaini kuwepo kwa ziada ya walimu wa masomo ya sanaa wapatao 7463 katika shule za sekondari, kutokana na hali hii serikali inaendelea na zoezi la kuwagawanya walimu hao au kuwa 'redeploy' kwa kuzingatia uwiano na mahitaji halisi ya walimu wa sanaa kwa kila mamlaka za serikali za mitaa ili kila shule iweze kupata walimu wa masomo ya sanaa badala ya kuajiri walimu wapya"

-alisema Angela Kairuki Mbali na hilo Waziri Kairuki amesema serikali inaendelea kuajiri watumishi wa kada mbalimbali ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 watumishi zaidi ya elfu tisa wameajiriwa serikalini.


"Katika mwaka wa fedha 2016/17 jumla ya watumishi wa Umma 90721 wamekwisha ajiriwa kwa kuzingatia vipaumbele na mahitaji ya kila mwajiri na katika mwaka wa fedha 2017/18 serikali inatarajia kuajiri watumishi 52436 wa sekta mbalimbali kwa kuzingatia vipaumbele vya taifa pamoja na kuimarisha kila sekta na upungufu mkubwa wa watumishi wa Umma"

-alisema Kairuki



Chanzo : EATV

Futeni kozi za Arts.
 
Back
Top Bottom