Si nimetoa AYA HIZO SOMA ZOTE.
za biblia kuanzia aya ya 10.
Bustani ya Edeni ipo nchi gani kwa sasa duniani?
Mungu alipoiumba dunia, alichagua eneo moja, na kulifanya kuwa la kipekee na la kitofauti na maeneo mengine yote aliyoyaumba duniani. Eneo hilo akaliita Edeni. Edeni maana yake ni eneo la furaha kuu, utulivu,paradiso ya Mungu.
Lakini hakuishia hapo tu bali ndani ya hiyo Edeni upande wa mashariki alitengeneza bustani nzuri sana, ambayo inajulikana na wengi kama bustani ya Edeni. Bustani hii ndiyo Mungu aliyomweka mwanadamu wa kwanza hapo aishi (yaani Adamu na uzao wake.)
Lakini kama tunavyosoma biblia, wazazi wetu wa kwanza walipoasi, walifukuzwa kutoka katika bustani ile, na kuanzia hapo, hakuna aliyejua makao halisi ya bustani ya Edeni yalikuwa wapi, vifunguu pekee vinavyotupa taswira ya eneo la bustani ya Edeni ni hivi;
Mwanzo 2:8 “Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.
9 Bwana Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
10 Ukatoka mto katika Edeni wa kuitilia bustani maji, na kutokea hapo ukagawanyika kuwa vichwa vinne.
11 Jina la wa kwanza ni Pishoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Havila, ambako kuna dhahabu;
12 na dhahabu ya nchi ile ni njema; huko kuna bedola, na vito shoham.
13 Na jina la mto wa pili ni Gihoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Kushi.
14 Na jina la mto wa tatu ni Hidekeli; ndio unaopita mbele ya Ashuru. Na mto wa nne ni Frati”.
Kama tunavyoona hapo, kulikuwa na mto uliokuwa unatoa maji kutoka bustanini na baadaye ukagawanyika katika vichwa vinne, na viwili kati ya hivyo (yaani Hidekeli na Frati) vinajulikana mpaka sasa na vipo maeneo ya nchi ya Iraq, ili kusoma na kufahamu zaidi historia yao fungua hapa >>>>
Mto frati na Hidekeli Na hiyo imewafanya masomi wengi wa biblia kudhania kuwa Edeni ilikuwa maeneo ya nchi ya Iraq au kando kando yake.
Lakini vile vingine viwili (yaani Pishoni na Gihoni) havijajulikana bado. Na iyo imewafanya wengine kudhani bustani ya Edeni ilikuwa nchi ya Uturuki ya sasa n.k.
Hivyo, hakuna uthibitisho wa moja kwa moja wa kudhania kuwa Edeni ilikuwa Iraq, au Uturuki au sehemu nyingine yoyote. Na hiyo ni kwasababu ya mabadiliko makubwa ya nchi yaliyokuwa yanatokea wakati wa gharika na ule wakati wa kugawanyika kwa nchi (Mwanzo 10:25). Historia inaonyesha kuwa dunia ilibadilika mwonekano wake kwa sehemu kubwa sana.
Lakini ni wazi kuwa Edeni haikuwa pengine zaidi ya mashariki ya kati, na sio Afrika kama wanasayansi wanavyoamini, nami naamini ilikuwa katika nchi Kaanani (Yaani Israeli ya sasa).