caliis
Senior Member
- Aug 3, 2015
- 107
- 117
kuhusu mada husika swala la kaini alimuoa Nani kwa mujibu wa kitabu Cha waislam halina ukakasi Ni very simple kwamba mama Hawa ktk kila uzao wake alikua akizaa mapacha wakike na wakiume na ilikua Ni ruksa kuoana isipokua kwa pacha waliozaliwa pamoja ndo haukuruhusiwa,, kilichotokea Kati ya ndugu Hawa wawili habili alizaliwa akiwa tunasema handsome na pacha wake wa kike alikua wa kawaida,, na kaini alizaliwa kawaida na pacha wake wa kike alikua mrembo hasa hivo kaini akamtamani dada yake I mean pacha wake wakati haikuruhusiwa na habili nae alimpenda pacha wa kaini wakawa na uhasama na chuki Kati yao,,baba yao akamuomba Mungu amuelekeze Cha kufanya baada ya kuona wanae hawaelewani ndipo alipoelekezwa ndugu hao wakatoe sadaka ambaye sadaka yake itakubaliwa ndiye atakaemuoa pacha wa kaini,, kaini alikua mkulima na habili mfugaji kama sijachanganya hivo kaini yeye alipeleka mazao yaliyoharibika na ndugu yake alipeleka nyama ya KONDOO aliyenona Mungu akaikubali sadaka ya habili bado kaini hakukubali akaazimia kuua ndugu yake na akamuua Kisha akaanza kujuta na hakujua Cha kufanya na ule mwili wa ndugu yake akamlilia sana Mungu wake ndipo Mungu akamletea kunguru wawili wa mfano wakapigana yeye akiwa anawataza mpka kunguru mmoja alipomuua mwingine Kisha akaanza kufukua chini na akausukumia mwili wa kunguru aliyekufa na kufukia ndipo kaini akajua Cha kufanya akachimba naye shimo akamzika nduguye,,, long story short nahisi nimevamia mada ya wenyewe Kama ndivo tuvumiliane.