R Mbuna
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 2,293
- 5,418
CHADEMA ni demockrasia kwanza hayo mengine yatafuata baadae.Chagademus mmeshabadili gia kama kawaida yenu, mwanzo mlimpongeza Uhuru kwa ushindi na kipenzi chenu EL alijipeleka kushiriki kampeni. Pili mlimuita Uhuru ni Baba Wa DOMOKRASIA lakini leo mahakama imemuona ni MWIZIKRASIA. Sasa baada ya kuona mmeumbuka ndani ya muda mfupi mmeanza kusifia na kupongeza Mahakimu lakini wakati Aliyefungua kesi Raila Odinga mnamruka kama kinyesi sababu tu ni swahiba wa kitambo na JPM ambaye mnakesha kumpinga hadhari wakati ndani ya Mioyoni yenu mnamkubali. Hahaahaahaaa
Ulitaka baada ya tume kutangaza matokeo ya uraisi huko Kenya CHADEMA wapinge matokeo ya nchi ambayo haiwahusu.
Ndio maana hata baada ya mahakama kutangaza kubatilisha ushindi wa Uhuru Kenyatta bado CHADEMA wanamkubali Uhuru kwa kuruhusu hayo yatokee kwa jinsi anavyoheshimu katiba na kuwajali raia wa Kenya.
Unadhani kwa nini raisi wako na mwenyekiti wa chama chako hayupo tayari kubadilisha hii katiba ya kikoloni ambayo inaipa tume ubabe ambao hata mahakama inashindwa kuiingilia utadhani na yenyewe ni muhumili unaojitegemea?
Uhuru Kenyata alikuwa na uwezo wa kuleta ubabe na kuamuru uchaguzi umeshapita na matokeo yameshatangazwa hivyo siasa mpaka 2022 lakini aliwapa kina Odinga haki yao ya kikatiba wakafungua kesi na mahakama kwa sababu zipo huru zimetoa maamuzi kulingana na katika wala si kwa amri toka juu.
Hiyo ndio sababu pekee CHADEMA wapo upande wa Uhuru na wala hawawezi kumkubali Kagame wala Museven wala Kabila wala Nkurunzinza.
Lumumba sometimes muamke vijana msiwe wachumia tumbo hata kwenye mambo yanahusu ustawi wa taifa letu.