Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Naomba Usiruhusu Udhalilishaji Huu Ndani ya Mahakama Zetu!.

kazi kubwa sana kuwaelimisha hawo wote wanao dhalilisha watu.
Kichapo chambwa koko na maneno mengine ya matusi na kutisha ndio yalozoeleka kwa vyombo vya dola.
 
Angalieni mtu alivyodhalilishwa hapa, kumbe hana hatia yoyote!. Pamoja na mtu huyu kuachiwa huru, kama ikitokea bado ana maumivu ya moyoni kutokana na mateso haya na kudhalilishwa huku, then, karma haina mswalia mtume na wahusika!, wanaojua kufuatilia mambo, by now wanajua jinsi karma inavyofanya mambo yake usikute hata naniliu... pia ni karma!.

Baada ya Mzee JR kuachiwa huru bila makosa yoyote, nayadurusu baadhi ya mabandiko yangu kuhusu kadhia hii, and I was 100% right.

Pia najua, itakuwa miongoni mwa masharti ya kuachiwa ni kutoishitaki serikali kudai fidia, lakini hata asiposhitaki, karma ya mateso yake, imeisha washughulikia baadhi ya watesi wake na waliobakia, karma yao inawasubiri.
Naendelea kusisitiza viongozi wetu tendeni haki.

Mzee JR, pole sana kwa mapito uliyopitia. Mungu ni mwema, shukuru kwa yote, karibu uraiani.

Paskali
 
Leo umeamka vizuri kidogo.

Ashukuriwe Mungu asiyewasahau watu wake, hatimaye Rugemarila amekuwa huru.

Mwili wake umeteswa na dharau amepambana nazo.

Amshukuru Mungu aliyeiokoa roho yake pengine kupitia maombi aliyokuwa akiomba na kuombewa na watu wote wenye nia njema.

Mungu alipigana vita yake na mtesi wake kweli hayupo tena.

Mpeni pole sana, Mungu aitunze afya yake.
 
Paskalli ni Kama sumaye kuna mda zinakuja kuna mda zinapotea
 
Sijui mwendazake huko aliko anajisikiaje! Hili jambo la JR tupende tusipende alihusika 100% na haya mateso aliyopitia huyu mzee na Sigh. Pia mamia ya wengine wengi waliteseka kwa amri yake kwa kutumia sheria mbovu.
Natumai atakuwa analambwa bakora huko aliko
 

What makes you think they are both innocent:

(a) is it because the current regime has orchestrated an atmosphere that portrays them innocent?

(b) is it because the concept of justice is way beyond your horizons of the moment?

(c) is it because things are quickly changing, we should therefore allow ourselves to be carried away so blindly by the whirlwind of change?

(d) or, you have to say something almost about anything that vindicates your quasi-relevance in the face of reason?
 
Mtu yoyote atachukuliwa hana hatia hadi itakapothibitishwa vinginevyo pasipo mashaka na mahakama huru.

A person is presumed to be innocent until proven guilty.

The burden of proof is on the one who declares, not on one who denies.
 
Umesahau ni awamu ipi iliyowadhalalisha hao? Sio ya Msukuma mwenzio? Ulikuwa wapi hukukemea wakati huo? Ulipojaribu kujidai kujipendekeza na kujitutumua kwa Msukuma mwenzio, ukashushuliwa na kuitwa "njaa".
 
Umesahau ni awamu ipi iliyowadhalalisha hao? Sio ya Msukuma mwenzio? Ulikuwa wapi hukukemea wakati huo? Ulipojaribu kujidai kujipendekeza na kujitutumua kwa Msukuma mwenzio, ukashushuliwa na kuitwa "njaa".
Kujua sheria raha, mnakaa mnachukua pesa bila idhini ya mwenzako na unampa Rugemalira kununua shares zake.

Ambaye yeye muuza shares anashiriki kupatikana pesa kutoka benki. Hana hatia kwa kutengeneza makaratasi huku zaidi budget ya wizara 5 kwa mwaka katia tumboni.
 
Umesahau ni awamu ipi iliyowadhalalisha hao? Sio ya Msukuma mwenzio? Ulikuwa wapi hukukemea wakati huo? .
Dada yangu FaizaFoxy , sijui ulipotelea wapi?. Swali zuri sana kwamba nilikuwa wapi sikukemea wakati huo. Nilidhani kwa seniority yako humu jukwaani, ukifungua bandiko, unaangalia ni la lini.
Nimekemea mambo mengi sana enzi hizo.
Mwache Bro wangu apumzike kwa amani huko alipo.
P
 
Unapulizia upewe mgawo wako sio?

Hakuna Karma inayofanya kazi kwa muktadha wa tafsiri yako

Wataje ni nani na nani wanaohusika na matokeo hasi ya Karma?

Je, rushwa haikutokea kwenye sakata la IPTL?


Mharifu namba moja dunia ni MWANASIASA
 
Umesahau ni awamu ipi iliyowadhalalisha hao? Sio ya Msukuma mwenzio? Ulikuwa wapi hukukemea wakati huo? Ulipojaribu kujidai kujipendekeza na kujitutumua kwa Msukuma mwenzio, ukashushuliwa na kuitwa "njaa".

Wewe mambo usukuma yanatoka wapi??

Hao ndio mastaa wa movi ya IPTL ba escrow? Hayo mambo yote yaliibuliwa na kujadiliwa na kutajwa bungeni kipindi cha KIKWETE.

Kama udhalilishaji, ulianza hapo.
 
Wewe mambo usukuma yanatoka wapi??

Hao ndio mastaa wa movi ya IPTL ba escrow? Hayo mambo yote yaliibuliwa na kujadiliwa na kutajwa bungeni kipindi cha KIKWETE.

Kama udhalilishaji, ulianza hapo.
Escrow na IPTL ilikuwa ni enzi za Kikwete sio JPM (ReferUchunguzi wa kamati ya Mwakyembe hadi waziri mkuu Lowasa kujiuzulu na mawaziri kadhaa waandamizi kuvuliwa uwaziri kama Tibaijuka nk)

Udhalilishaji ulifanyika kipindi hicho lakini hakuna hatua zilizochukuliwa) baada ya hapo alipoingia madarakani alichukua hatua na baadhi walirejesha fedha rejea aliyewahi kuwa waziri wa nishati na madini Ngereja.

Uovu wote ulipandwa, kustawishwa na kukomazwa enzi za JKM, lakini JPM alipochukua hatua lawama zote anatupiwa yeye maajabu ya dunia ndani ya nchi isiyo ya asili Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…