Kahama yaangamia kwa Ukimwi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kahama yaangamia kwa Ukimwi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Apr 23, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,655
  Trophy Points: 280
  Kahama yaangamia kwa Ukimwi

  Imeandikwa na Raymond Mihayo, Kahama; Tarehe: 22nd April 2011 @ 23:35 Imesomwa na watu: 102; Jumla ya maoni: 0
  ASILIMIA 70 ya vijana wenye umri kuanzia miaka 20 hadi 49 ambao ndio nguvu kazi ya Taifa wilayani Kahama, mkoani Shinyanga wameambukizwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi, imeelezwa.

  Hayo yamesemwa na Ofisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kahama, Morgan Mwita katika taarifa ya hali ya Ukimwi katika Wilaya ya Kahama mbele ya wadau wa mapambano dhidi ya ugonjwa huo wakiwemo watendaji wa kata na viongozi wa dini.

  Mwita alisema kuwa katika Wilaya ya Kahama, kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo inatisha hasa miongoni mwa vijana ambapo cha mwaka 2009, maambukizi yalikuwa asilimia 7.3, lakini sasa yamefikia asilimia 9.3 hali ambayo ni mbaya.

  Alisema wakati wilaya hiyo ina wakazi 815,175, wakazi 85,342 walijitokeza kupima Ukimwi hadi kufikia Desemba mwaka 2010, na 7,913 waligundulika wameambukizwa virusi vya Ukimwi.

  Mwita alisema kutoka na maambukizi ya ugonjwa huo kuwa makubwa, changamoto wanayoipata wao kama Wilaya ya Kahama ni pamoja na kuendelea kuelimisha jamii kuacha kabisa unyanyapaa na ubaguzi kwa wanaoishi na virusi vya Ukimwi.

  Alisema changamoto nyingine ni pamoja na kutoa elimu kuhusu ugonjwa huo hasa katika maeneo ya vijijini ambako kuna idadi kubwa ya watu ambao hawajapa elimu ya kutosha kuhusu ugonjwa huo hatari.

  Hata hivyo ofisa huyo aliyataka mashirika mbalimbali kuongeza jitihada za kutafuta fedha za kuhudumia watoto walio katika mazingira magumu na hatarishi hasa katika upande wa lishe, elimu, ujasiriamali na afya.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,655
  Trophy Points: 280
  Hizi takwimu zinatia shaka...........................kama maambukizi ni 9.3% inakuwaje walioambukizwa wafikie asilimia 70?

  Kuna mapungufu makubwa ya uchambuaji wa habari hapa..........................
  PHP:
   ASILIMIA 70 ya vijana wenye umri kuanzia miaka 20  hadi 49 ambao ndio nguvu kazi ya Taifa wilayani Kahamamkoani Shinyanga  wameambukizwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwiimeelezwa.  
   
 3. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145

  Mkuu, japo % ipo juu, lakini siyo mbaya kama sehemu nyingine. Hebu rejea hii:

   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mwandishi hakusoma statistics hata kidogo...hakuna hesabu za hivo
   
 5. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2011
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,123
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Hiyo asilimia 70 imetoka wapi? Waliopima 9% positive na hiyo yenyewe hauwezi kuiaply kwa jamii nzima.
   
 6. C

  Chechenya Member

  #6
  Apr 23, 2011
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Lakini ukimwi upo kwa kiwango kikubwa ingawaje takwimu siyo sahihi
   
 7. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,348
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  badilini tabia. Takwimu hazitotokomeza ukimwi
   
 8. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2011
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Takwimu zinatia Shaka sana. Nadhani si sahihi
   
 9. mjunguonline

  mjunguonline Member

  #9
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndio Elimu yetu ya Shule za Kata.Hapo mwandishi hastahili kulaumiwa,kwani huo ndio uelewa wake kwa kuwa ndivyo alivyofundishwa hivyo kuhusu TAKWIMU.Wakulaumiwa hapa ni SERIKALI Kuanzia Shule nyingi za kata bila kujali ubora wa Elimu inayopatikana kwenye shule hizo za KATA.Matokeo yake ndio haya mnayoyaona kwenye "JF".All in all ndugu zangu na hasa vijana.Tuepuke ngono ambazo si salama.Tutumie Kondomu Jamani,sisi ndio nguvu kazi ya TAIFA...
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mji wa Kahama ni kambi kubwa ya madereva wa magari makubwa wenye masafa marefu. Uchunguzi wangu unaonyesha mikoa ya Shinyanga na Tabora imeadhiriwa zaidi katika miji ya Kahama na Nzega. Nyumba za wageni zimejaa madereva wa magari makubwa yaendayo pande za Rwanda na Burundi.

  Iringa nako hali kama hiyo kwani madereva baada ya kulazimisha malori kupanda mlima Kitonga wanajipumzisha Iringa, na wengine kabla ya kujiandaa kuteremsha mlima Kitonga wanajipumzisha Iringa kwanza.

  Waambukizaji wakubwa ni madereva na dada zetu victims wanaotafuta cho chote toka kwa madereva kujikimu kimaisha. Na hawa dada zetu wanawaume au marafiki wengine wanakopandikiza walivyovuna kwa madereva.

  Jamani Ukimwi unakwepeka kwa wanaojiamini na kuamua kuaminiana baada ya kujihakikishia usalama wao
   
 11. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #11
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  tasnia ya uandishi wa habari imevamiwa!
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kuna kampuni ya wiliamson ilitoa magari takribani 30, kuwapeleka wafanya kazi wake kwa babu hii ni ishara tosha kuwa hari huko si shwari...
   
 13. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  tatizo siyo madereva tu....hakuna sehemu ambao nilisha wahi kufika ambako ngono inafanyika hovyo hovyo kama mbuguni, utakuta vitoto vya darasa la tano vina mimba hapoa kuna maderva gani...
   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kumpata dada ambaye bikra siku hizi ni chanda cha dhahabu, hali kadhalika kumpata kaka asiyekuwa na uzoefu wa mahusiano ya mapenzi ni imebaki kuwa ndoto ya kufikirika. Masimulizi siku hizi hayakosi kugusa ngono na mbinu za kufanya ngono, hali hiyo huakisi vijana kufanya majaribio ya ngono kwa wajifunzayo kuona na kusikia.

  Mfumo wa media nao unachangia maana hata tu taswiraz nyingi zinahamasisha ngonoz, na watu wanafundishana mbinu chafu zenye kuendekeza mambo mabaya kama hayo kwa uwazi, vyombo vya habari na mitandaoni. Kwa mtindo huu ukimwi vigumu kukwepeka.

  Hata matumizi ya condom sijui kama yana uzito wa pekee wakati watu wanafanya mengine kupita hata silika ya hayawani wa porini kwa kutumia milango mingine ya maumbile ambayo Mungu hakuiweka kwa makusio hayo.

  UCHAFU UCHAFU UCHAFU UNACHEFUA KILA KUKICHA, NA KUAMBIWA UKWELI WANASEMA AJALI KAZINI, SAWA NA KUMPIGIA MBUZI GITAA
   
 15. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,290
  Likes Received: 1,444
  Trophy Points: 280
  ina maana wengi wa kina dada wanazaliwa bila hiyo na wengi wa kina kaka wanapata uzoefu kabla hawajazaliwa?
   
 16. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #16
  Apr 23, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kuna kiongozi mmoja nilimsikia akisema waandishi ni walefailer sijui kweli au
   
 17. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Huu ugonjwa tusiudharau maana bado unatesa watu wengi....elimu na kubadili tabia ndio njia pekee ya kupunguza maangamizi.Kahama pamechangamka sana...hasa baada ya mgodi wa Buzwagi kusogea pale. kwenye wengi kuna mambo mengi pia
   
 18. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #18
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kama unaendesha gari toka Singida ukishaanza kuiacha wilaya ya Iramba na kumaliza mteremko wa mlima Sekenke, kamji kanakofuata endelea hadi Nzega na kisha Kahama ni dhoruba, maana kazi hiyo ni kama ajira ya waliomaliza shule za msingi. Sijajua bado biashara za mikononi kwa vijana wadogo giza likishaingia biashara gani inaendelea, we tulia kidogo maeneo hayo utashtuka, na kama baba mwanao hajakutambua bado utamshtukia, makubwa jamani kinachoendelea duniani hapa.

  Happy Pass Over to all
   
 19. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #19
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Boyfriend & Girlfriend mahusiano yanaanza kabla hawajajua ulimwengu ukoje na bado wananukia maziwa ya utotoni, je hayo yatawafikisha kunako ndoa au ni mfumo wa kuiga tamaduni nyingine ambazo wazazi wetu hawakuzoea?

  Eti siku hizi lazima watu wafanye majaribio kwanza, na wakijaribiana na kuchokana nini kitaendelea? Katika kujaribiana na kuzoeana hatima yake ni kutwishana mimba baadaye kuchokana hatima yake kila mmoja na njia yake huku hakuna uhakika kama walikuwa makini kujiangalia kiafya. Na mapokea kwa waafrika wengi msichana kisha zaa soko la kuolewa huwa adimu kidogo, bora ajenge njia ya kujitegemea mwenyewe.

  Ukimwi unakwepeka kwa wanaojiamini na kuamua kuaminiana baada ya kujihakikishia usalama wao
   
 20. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #20
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,290
  Likes Received: 1,444
  Trophy Points: 280
  asante kwa maelezo haya lakini hujagusia suala la kinadada bikra kuwa nadra, vile vile kina kaka wasio na uzoefu.
   
Loading...