Mheshimiwa Spika,hadi Aprili, 2024
ujenzi wa sehemu ya Kazilambwa – Chagu (km
36) na Urambo Roundaboutkwa kiwango cha
lami umekamilika. Aidha, ujenzi wa sehemu ya
Uvinza – Malagarasi (km 51.1) umefikia asilimia
53.
82.Mheshimiwa Spika,katika barabara ya
Ifakara – Kihansi – Mlimba – Madeke – Kibena
(km 346.43),Mkandarasi wa ujenzi kwa kiwango
cha lami sehemu ya Ifakara – Mbingu (km 62.5)
anaendelea na maandalizi ya ujenzi. Vilevile,
Mkataba wa ujenzi wa sehemu ya Mbingu – Chita
JKT (km 37.5)kwa kiwango cha lami umesainiwa
tarehe 13 Machi, 2024 na Mkandarasi anaendelea
na maandalizi ya kuanza ujenzi. Katika Barabara
ya Njombe (Kibena) – Lupembe – Madeke (km
126); Sehemu ya Kibena – Kidegembye (km 42)
taratibu za manunuzi ya Mkandarasi na Mhandisi
Mshauri kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami
zinaendelea. Aidha, taratibu za manunuzi kwa ajili
ya kumpata Mhandisi Mshauri wa kufanya
Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa
50